Tafuta

Vatican News
  Baba Mtakatifu amepanda mti wa Assis katika Bustani za Vatican Baba Mtakatifu amepanda mti wa Assis katika Bustani za Vatican   (ANSA)

Baba Mtakatifu amepanda mti kutoka Assisi katika Bustani za Vatican!

Tarehe 4 Oktoba 2019 ikiwa ni kumbukumbu ya Mtakatifu Francisko wa Assisi,katika Bustani za Vatican,Baba Mtakatifu Francisko amepanda mti kutoka katika ardhi ya Assisi kama ishara ya ekolojia fungamani.Tukio hili limefuatia sala ya kuombea Sinodi Maalum ya Maaskofu kuhusu Amazonia na kuikabidhi chini ya maombezi ya Mtakatifu Francisko wa Assisi ili mchakato uweze kuzaa matunda.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Katika kuadhimisha Siku kukuu ya Mtakatifu Francisko wa Assisi Tarehe 4 Oktoba 2019, Baba Mtakatifu Francisko ameshiriki maadhimisho yaliyof anyika katika Bustani za Vatican, kwa ishara ya kupanda mti kutoka  ardhi ya Assisi Italia  kama ishara inayo onekana ya ekolojia fungamani. Tukio hili limefuata sala ya kwa ajili ya Sinodi kuhusu Amazonia  itakayo anza siku mbili  zijazo huku wakilikabidhi chini ya maombezi ya Mtakatifu Francisko wa Assisi. Sikukuu ya Mtakatifu Francisko wa Asisi inafunga kipindi cha maadhimisho ya Kazi ya Uumbaji ambayo imekuwa sasa ya kila mwaka kuanzia tarehe 1 Septemba na ambayo kwa mara ya kwanza ilitangazwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya Kanisa Katoliki 2017.

Kard Turkson:ecolojia ya kulinda kwa utambuzi na hekima

Baada ya wimbo kutoka Amazonia usemao "nimepiga mbizi, nimepiga mbizi"katika Bustani za Vatican, Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma na Maendeleo Fungamani ya watu amejikita tafakari  yake kuhusu dharura ya uongofu wa kiekolojia. “Wasi wasi wetu amesema ni kujibu kipeo hiki cha kiekolojia ambacho lazima kisaidiwe kutokana na dhamiri na hekima kama alivyo shauri Baba Mtakatifu Francisko”. Kardinali Turkison aidha akiwangaziwa  na Wosia wa Laudato si amesema “Iwapo tunataka kweli kujenga ekolojia ya kweli tunapaswa kuruhusu ukarabati wa kila kitu ambacho tumeharibu" na kwa maana hiyo hakuna tawi lolote la kisayansi, hakuna mtindo wa hekima ambao unaweza kudharauliwa, hata ule wa kidini na lugha yake yenyewe.

Kardinali Hummes:kuweka wakfu Sinodi chini ya Maombezi ya Mtakatifu Francis

Naye Kardinali Cláudio Hummes, Askofu Mkuu mstaafu wa Mji wa Mtakatifu Paulo nchini Brazil na Rais wa tume ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya Amazonia kwa upande wa Maaskofu wa Brazail, amekumbusha uhusiano uliopo kati ya Papa, Sinodi kwa ajili ya Amazonia na Mtakatifu Francisko wa Assisi.Kwa maana hiyo amesema, "kuweka wakfu Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya Amazonia chini kwa Mtakatifu Francisko wa Assisi ni ishara ya upendo na yenye maana kubwa". Hata hivyo amesema yote hayo kwanza yamefungamana na jina la Francisko ambalo, Baba Mtakatifu alichagua tangu siku ya kwanza ya uchaguzi kama Papa na sehemu ya pili ni maneno yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro Oktoba 2017 akitangaza ujio wa tukio hili la Sinodi maalum.

Askofu Mkuu Hummes amesema: “Tunapoweka wakfu Sinodi hiyo kwa Mtakatifu Francisko tunakumbuka hasa wimbo wake wa kusifu  viumbe ambayo inashehereka na kuimba udugu wa ulimwengu kwa viumbe vyote vya Mungu”. Mauricio López Oropeza, katibu mtendaji wa Mtandao wa Kanisa wa (Repam), ndiye aliyesoma sala ya kuweka wakfu Sinodi kwa Maskini wa Assisi Francis. Na katika maneno ya sala inaanza hivi : “Tunakusifu wewe Bwana kwa uzuri, kwa ajili ya mvua nyororo ambayo inaonekana kwa macho yetu tu, mvua inayoleta maisha na kutuliza kile ambacho umekiumba kwa wororo wako na utulivu. Matone ambayo yanaongezeka taratibu katika mtitiriko wa maji ni yale ambayo yataonekana kuzaliwa kwa mito. Mito ambayo, ikiunganija itatoa uwepo wa wasiwasi mkubwa kwa ajili ya  Amazonia  na ambayo ni chanzo cha maisha tele kwa wote.

Kupanda mti katika bustani za Vatican 

Kabla ya kupanda mti huo, watu nane wakiwakilisna  watu asilia na hali halisi nyingine kati ya hizo, uhamiaji,na maendeleo endelevu, wamepeleka gunia dogo na ndani ya gunia hilo kulikuwa na udongo unaotoka katika maeneo tofauti, na kati ya  ishara hizo ni Amazonia, India  na  Assisi na kuweka chini ya miguu ya mti. Na baadaye wameweze kupanda mti huo. Aliye upanda mti  ni BabaMtakatifu pamoja na wawakilishi wawili asilia , Kardinali  Hummes na Kardinali  Baldisseri. Hii ni ishara rahisi na ya kina, ambayo inaamanisha uongofu wa kiekolojia fungani wakati huo walikuwa wakisindikizwa na wimbo wa Sifa kwa Muumba. Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa sala ya Baba Yetu kwa kuongozwa na Baba Mtakatifu Francisko.

Maadhimisho hayo

Hata hivyo pia ni madhimisho yanayo fanyika  wakati wa kukaribia miaka 40 tangu kutangazwa Mtakatifu Francisko kama Msimamizi Ekolojia kunako tarehe 29 Novemba 1979 na Mtakatifu Yohane Paulo II. Vile vile Baba Mtakatifu Francisko alikuwa alikwisha panda mti mwingine katika Bustani za Vatican kunako tarehe 8 Juni 2014 wakati wa fursa ya Mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya Amani ya Nchi za Mashariki, ambapo walikuwa ni rais wa Israeli, Palestina na Patriaki Bartholomeo I. Mpango huo pia  umeweza kuwashirikisha hata viongozi asilia na wa Kanisa, ulioandaliwa na Shirika la ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko, Mtandao wa Kanisa wa Amazonia(Repam) na Chama cha katoliki ulimwenguni cha  harakati za kupambana na tabianchi (Gccm).

 

04 October 2019, 14:58