Tarehe 5 Oktoba 2019 wamesimikwa Makardinali 13 wapya wa Kanisa katika kanisa Kuu la Mtakatifu petro Vatican Tarehe 5 Oktoba 2019 wamesimikwa Makardinali 13 wapya wa Kanisa katika kanisa Kuu la Mtakatifu petro Vatican  

Papa Francisko:Shuhudia huruma ya Yesu iliyotiwa mhuri mioyoni mwenu!

Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake Jumamosi,jioni tarehe 5 Oktoba 2019 wakati wa kuwasimika Makardinali 13 amesisitizia juu ya kuwa na uhuruma ya Mungu ambayo kama makardinali wanapaswa kuwa na utambuzi hasa kutokana na vazi jekundu wanalopewa kama ishara ya umwagaji damu kwa ajili ya Kristo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumamosi jioni, tarehe 5 Oktoba 2019, limejazwa na makardinali, maaskofu wakuu, maaskofu, mapadre, mashemasi, watawa wa kike na kiume na waamini wote ili kushuhudia Baba Mtakatifu Francisko akiwasimika Makardinali 13 aliowateua hivi karibuni. Ni maadhimisho yaliyo fanyika katika mkesha wa ufunguzi wa Sinodi Maalum ya Maaskofu kuhusu Amazonia. Baba Mtakatifu Francisko Francisko akianza mahubiri yake amesema, kiini cha somo la kiinjili iliyo sikilizwa (Mk 6,30-37 a) kuna huruma ya Yesu. Huruma ambayo ni  ufunguo wa Injili iliyoandikwa katika moyo wa Kristo na imeandikwa daima katika moyo wa Mungu. Katika Injili mara nyingi tunamwona Yesu anashikwa na  huruma kwa ajili ya watu wanaoteseka. Kadiri tunavyo soma na kutafakari, ndivyo tunatambua zaidi kwamba huruma ya Bwana siyo tabia ya muda mfupi tu ba isiyo na na kina, bali ni yenye msimamo na ndiyo imejikita ndani ya huruma hiyo ya Mungu .

Mwinjili Marko anamtaja Yesu anapoanza utume wake wa kwenda Galiya huku akitangaza na kufukuza pepo wabaya na wakati huo alifika mkoma akapiga magoti huku akiomba kama anaweza kutakasika (Mk 1,40-42). Katika ishara  hiyo na maneno hayo  upo utume wa Yesu mwokozi wa mwanadamu, anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Ni mwokozi wa huruma. Yeye anajikita ndani mwake  mapenzi ya Mungu na kutakasa mwanadamu dhidi ya ugojwa wa ukoma wa dhambi. Yeye ni mkono ulifunguliwa wa Mungu unaogusa mwili ulio ugua na kutimiza matendo yake akituliza giza la mahangaiko. Yesu anakwenda kutafuta mtu aliye baguliwa, na wale ambao hawana tena matumaini, kama  yule kiwete ambaye alikuwa hawezi kwa muda wa miaka thelathini na minane, amelala karibu na Mlango Bethzatha, akisubiri mtu aweze kumsaidia kuingia ndani ya maji ya birika ( Yh 5,1-9)

Huruma hiyo haikutokea ghafla tu katika historia, bali ilikuwepo kwa Mungu na imewekwa mhuri ndani ya  moyo wa Baba. Inaonesha katika historia ya wito wa Musa, Mungu alipozungumza kutoka katika kichaka kinacho waka moto  na kusema “ nimeona mahangaiko ya watu wangu huko Misri, na nimesikia kilio chao (…) ninatambua mateso yao ( Kut 3.7). Upendo wa Mungu kwa watu wake ni ndiyo kila kitu hadi kufikia kuwa na uhusiano wa agano, na kwa maana ya kile kilicho cha Mungu ni huruma ambapo kwa bahati mbaya kwa binadamu hali hiyo inakosekana na kuonekana hiko mbali sana amesema Baba Mtakatif . Hali hiyo anasema  Mungu mwenyewekwamba: Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuponya, Israeli? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja(…) Kwa maana mimi ni Mungu, si mwanadamu mimi; mimi ndiye aliye Mtakatifu katikati yenu; wala sitaingia ndani ya mji. (Hos 11,8-9).

Mitume wa Yesu wanajionesha mara nyingi hawana huruma kwa mfano katika kesi hii, mbele ya tatizo la watu wengi wanaotaka kushibishwa. Baba Mtakatifu anatoa mfano: Mitume labda  walisema watajijua… Hii ni tabia ya kawaida iliyomo katika ubinadamu, kwani “ hata kwa  watu wa dini na zaidi wale wa ibada. Nafasi ambayo wanayo haitoshi ya kuwafanya wawe na huruma. Ni kama inavyojionesha tabia pia ya kuhani na Mwandishi ambao walimpita mtu aliyekuwa amejeruhia barabarani na majambazi, walitazama sehemu nyingine ( Lk 10,31-32). Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri amesema, si hajabu walisema, hii hainihusu, maana daima kuna kutafuta sababu. Kama vile hata  suala la watu wenye ukoma, ambao walifikiri ni lazima wabaki nje na ni haki. Katika tabia hizi za kibinadamu zinaleta hata miundo ambayo haina huruma.

Baba Mtakatifu kwa maana hiyo anaomba kujiuliza maswali kama wao je wanayo huruma ya Mungu? Amesema hayo hasa akiwalenga makardinali na wale ambao wangetakiwa kuwa makardinali.  Je utambuzi huo wa kwanza daima umewaweza kusindikizwa na huruma?Vile vile anaonesha mfano kwamba, utambuzi huo ulibaki daima katika  moyo wa Bikira Maria ambaye alisifu Mungu kama  "Mtumishi wake mdogo aliyetazamwa kwa unyenyekevu wake ( Lk 1,48)". Vile vile amekumbuka sura ya Nabii Ezekieli inayoelezea upendo wa Mungu kwa Yerusalemu isemayo: “Nami nitaweka imara agano langu nawe; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; upate kukumbuka, na kufadhaika, usifumbue kinywa chako tena, kwa sababu ya aibu yako; hapo nitakapokusamehe yote uliyoyatenda (Ez 16,62-63).  Pia Osea hata Hosea anasema: “nitakupeleka jangwani na nitazungumza katika moyo wako(…) pale utanijibu kama siku za ujana wake na kama ulivyotoka katika nchi ya Misri.”

Kwa mfano huo, ndipo maswali ya Baba Mtakatifu Francisko akiuliza:Je! Ufahamu wa huruma hii ya Mungu ni hai kwetu? Na hi siyo suala la hiari, wala kusema ni ushauri wa kiinjili. Hapana. Hili ni hitaji muhimu. Ikiwa sihisi  kitu cha huruma ya Mungu, sielewi upendo wake”. Siyo ukweli ambao unaweza kufafanuliwa, anabainisha Baba Mtakatifu. Labda ninahisi au sihisi. Na ikiwa sihisi, ninawezaje kuitangaza, kuishuhudia, na kuitoa?  Kwa dhati, je ninamwonea huruma kaka huyo, Askofu yule au padre yule? Au daima ninaharibu kwa sababu ya tabia ya kuhukumu na sintofahamu?

Utambuzi huo unategemea hata uwezo wa kuwa halisi katika utoaji wa huduma binafsi. Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba hata hao makardinali kwani, wezekano wa Kardinali kutoa damu yake inayomaanishwa na rangi nyekundu ya nguo yake. Ni uhakika hasa kwa kusimika mizizi katika dhamiri ya kupokea huduma na katika uwezo wa kuwa na huruma. Kinyume na hiyo huwezi kuwa halisi. Tabia nyingi sizizo halisi za watu wa Kanisa zinategemea na kukuza maana ya huruma waliyoipokea au mazoea ya kutazama sehemu nyingine, mazoea ya kuwa na sintofahamu.  Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha akiomba kwa maombezi ya Mtakatifu Petro neema ya kuwa na moyo wa huruma  ili  kuwa mashuhuda wa Yule ambaye aliwatazama kwa huruma, aliwachagua na kuwaweka wakfu na kuwatuma wapeleke Injili yake ya wokovu.

05 October 2019, 17:16