Tafuta

Vatican News
Sala ni pumzi ya maisha mapya ndiyo kichwa cha kitabu kipya cha Papa Francisko Sala ni pumzi ya maisha mapya ndiyo kichwa cha kitabu kipya cha Papa Francisko  

Papa:sala ya wakristo iwe pumzi ya Kanisa!

Kitabu ambacho bado hakijatangazwa cha Papa Francisko kinasisitiza umuhimu wa sala katika maisha ya kikristo.Ni maandishi ambayo yametolewa dondoo zake kwenye Gazeti katoliki la Avvenire na ambapo kichwa cha kitabu ni “Sala.Pumzi ya maisha mapya”, toleo la Lev. Kinakusanya hotuba za Papa kuhusu sala na kitatangazwa tarehe 24 Oktoba 2019 Italia na Ufaransa kina utangulizi wa Patriaki Kirill wa Moscow.

Kitabu cha Papa Francisko

Kitabu ambacho bado hakijatangazwa cha Papa Francisko kinasisitizia umuhimu wa sala katika maisha ya kikristo. Ni maandishi ambayo yametolewa dondoo zake kwenye Gazeti katoliki la Avvenire na ambapo kiini cha kitabu hicho ni kuhusu  “Sala. Pumzi ya maisha mapya” , toleo la Lev. Kitabu hicho kiliwakilishwa hata katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vatabu huko Frankfurt, ambacho kinakusanya hotuba za Baba Mtakatifu kuhusu sala na kwa namna ya pekee kuhusu “Baba Yetu” na kitabu hicho kitatangazwa tarehe 24 Oktoba 2019 nchini Italia na Ufaransa chenye kuandikwa utangulizi na Patriaki Kirill wa Moscow.

Ubatizo ni mwanzo wa maisha mapya. Je nini maana ya kusema maisha mapya?

Maisha mapya ya ubatizo siyo mapya kama tunavyo badilisha kazi au kuhamishwa kutoka mji mmoja na kusema, nimeanza maisha mapya. Katika kesi hii maisha yanabaidilika, labda hata sana, ni tofauti na yale ya kwanza. Bora au mabaya, yanayopendeza au yenye ugumu, kulingana na hali halisi hiyo. Hali, mantiki, wafanyazi wenzako, watu unawaowafahamu na hadi kufikia marafiki, nyumba, mshahara ni vitu tofauti. Lakini yote hayo siyo maisha mapya,  ni maisha yale yale ambayo bado yanaendelea. Maisha mapya katika Kristo ni tofauti  hata namna ya kuishi kwa mabadiliko ya kina ya hisia zetu  hasa wakati wa kupenda au kukata tamaaa, wakati wa ugonjwa na dharura muhimu.  Mambo kama hayo yanaweza kutukia kama tetemeko la ardhi, ndani na nje: inawezekana kubadili thamani, uchaguzi wa kina kama vile upendo, kazi, afya, huduma ya wengine… Na labda kwanza ni kufikiria kazi na baadaye kuanza kujitolea, au zaidi kufikia kujitolea maisha binafsi kama zawadi ya wengine!  kwa mfano kwamba,  hapakuwapo na wazo ya kujenga familia na baadaye ni kufanya uzoefu wa upendo wa wana ndoa na familia.

Hata mambo hayo yenye kuwa na mabadiliko makubwa na  maalum, lakini bado tu yanaendelea kuwa ni mabadiliko. Ni mabadiliko ambayo yanatuongoza kwenye maisha mazuri zaidi na yanayo endelea, au magumu zaidi na kidogo. Tunaweza kusema ndiyo yametuwezesha kuishi vizuri zaidi na furaha na kuwa wenye upendo zaidi. Je ni kwa sababau gani tunaendelea kulinganisha kati ya mambo zaidi au kidogo yanayofanana na hayo. Utafikiri ni kama tunapima mambo katika ngazi yenye thamani: Maisha kabla yalikuwa na furaha 5, na sasa ni furaha 7; kwanza afya ilikuwa 9 na sasa ni 4. Namba zinabadilika lakini hazina thamani ya maisha! Maisha mapya ya ubatizo siyo maisha tu, kulingana na wakati uliopita wa maisha  ambayo yametangulia maisha ya kwanza. Upya hauna maana ya kusema hivi karibuni, kwamba kuna yaliyokuwapo na kurekebishwa katika mabadiliko.

Maisha ya Mungu ni muungano na tumepewa kama rafiki

Maisha mapya anayozungumza Mtakatifu Paulo, katika barua zake zinatukumbusha amri mpya ya Yesu (Yh 13, 34); anatukumbusha divai mpya ya Ufalme (Mk 14, 29), wimbo mpya wa waliokombolewa na wako mbele ya kiti cha Mungu (Ap 5,9): hali haki ya mwisho na kwa jina la kitaalimungu (eschatological). Kwa maana hiyo tunatambua kwamba, siyo rahisi maisha mapya kuyalinganisha. Inawezekana kulinganisha maisha na kifo au maisha ya kwanza na baada ya kuzaliwa? Kristo hakufanyika mtu na sisi, hakuishi mateso ya Pasaka yake, kifo na ufufuko kwa ajili ya kuboresha maisha yetu, ili kuyafanya yawe mazuri zaidi, yenye utamu, yenye kurefuka, yenye kina, rahisi au furaha. Yeye amekuja –kama alivyotueleza ili tuweze kuwa na maisha tele (Yh 10,10)

Hayo ndiyo maisha mapya, maisha ambayo Mungu Baba anatuzawadia katika ubatizo. Ni mapya kwa sababu ni maisha mengine kulingana na ya kwetu, kwa sababu ni ya kwake, ni maisha yake  Mungu mwenyewe. Ndiyo zawadi kubwa ambayo aliifanya na anatufanyia Yesu! Kushiriki upendo wa Mungu, wa Baba na wa Roho Mtakatifu. Kushiriki kwa upendo walionao kwa watu wote na kwa ajili ya uumbaji wote. Maisha mapya ni maisha ya Mungu aliyotolewa kwetu.

Kila wakati wakristo tumekuwa tukitafuta picha na ishala ya kuelezea zawadi hii kubwa. Sisi ni wengi, tofauti, licha ya hayo sisi ni kitu kimoja, ni Kanisa. Na muungano huo ndiyo upendo ambao haulazimishi, haunyenyekezi auzuii, bali unaongeza nguvu na kutujenga sisi sote pamoja na kutufanya tuwe marafiki. Yesu anasema jambo moja zuri katika Injili: Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma (Yh 17, 3). Ni yeye mwenyewe anatueleza kuwa maisha ya kweli ni kukutana na Mungu; na kukutana na Mungu ndiyo kutambua Mungu. Pia tunatambua kutoka katika Biblia kuwa,huwezi kujua mtu tu kwa utumia kichwa, kwa sababu ili kujua maana yake ni kuomba. Na hii ni maisha ya Mungu aliyotupatia kuwa upendo ambao ungekuwa  wetu na kidog kidogo kufanya ukue kwa neema ya Roho Mtakatifu (Rm 5, 5), na unaangaziwa hata na ishara zetu ndogo kama vile: “asante, hodi? samahani za kila siku.

Ingawa maneno hayatoshelezi lakini, tunaweza kusema kuwa maisha mapya ni kujigundua Mtu, ni mali ya Mtu na katika Yeye ni mali ya wote. Kuwapo inamaanisha kuwa kila mtu ni kwa ajili ya mwingine. Hiyo inanikumbusha kile ambacho  kinarudiwa kusika katika wimbo ulio bora, “mpenzi wangu ni wangu na mimi ni wake (Ct 2, 16).” Na tazama siku hadi siku, Roho Mtakatifu anaendelea kutimiza ukamilifu wa sala ya Yesu: “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. (Yh 17,20-21). Moja ya sura ya kizamani sana iliyotumiwa na Mtakatifu Paulo kueleza uwepo huu katika maisha ni ile ya mwili ambapo kiongozi mkuu ni Kristo na sisi ni viungo vyake: “Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake (1Cor 12, 27).”

Alama ya mwili

Katika mwili kuna baadhi ya sehemu nyingihufanya kazi kama vile mapigo ya moyo na pumzi. Ninapendelea kufikiria kuwa sala binafsi na ya kijumuiya kati yetu wakristo iweze kuwa pumzi,mapigo ya moyo wa Kanisa  na mbayo yanasambaza  nguvu zake katika huduma kwa yule  anayefanya kazi, anasoma, anafundisha; na kuleta mafao ya utambuzi wa watu walioelimika  na unyenyekevu kwa watu rahisi: naambao wanato matumaini kwa wale ambao wanapatanania haki ya usawa. Sala ni yetu ya kuweza kusemandiyo kwa Bwana, kwa upendo wake unaotufikia: ni kupokea Roho Mtakatifu ambaye hachoko kamwe kuvuvia upendo na maisha juu ya wote.

Alikuwa anasema Mtakatifu Serafino wa Sarov, mwalimu mkubwa wa kiroho katika Kanisa la Urusikwamba, " kupata  Roho wa Mungu ndiyo lengo la mwisho wa maisha yetu ya kikristo, hadi kufikia kuwa sala, mikesha, kufunga, sadaka, na matendo mengine ya fadhila yanayofanywa kwa Jina la Kristo yawe ndiyo zana kwa ajili ya lengo hili la mwisho.  Mtu daima hajuhi kuwa anapumua kila wakati, lakini ndiyo hali halisi ya kuwa mtu hawezi kuacha kupumua.

 

20 October 2019, 08:43