Tafuta

Vatican News
Baraza la Maaskofu Katoliki Poland limezindua maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II, kilele chake ni mwaka 2020. Baraza la Maaskofu Katoliki Poland limezindua maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II, kilele chake ni mwaka 2020. 

Maadhimisho ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mt. Yohane Paulo II

Baraza la Maaskofu Katoliki Poland limezindua maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II, aliyesimama kidete kudumisha Injili ya familia inayofumbatwa katika Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo! Maaskofu wametumia maadhimisho haya, ili kuwaafahamisha vijana wa kizazi kipya ushuhuda wa utakatifu uliotolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, amewashukuru na kuwapongeza waamini wa Kanisa Katoliki nchini Poland ambao, Jumapili tarehe 13 Oktoba 2019 wameadhimisha Siku ya Ukarimu wa Papa. Maadhimisho haya yameongozwa na kauli mbiu “Simameni, Tuanze kutembea”. Baba Mtakatifu anawashukuru kwa sala na mchango wao wa hali na mali katika maisha na utume wa Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuwasaidia maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Mwaka 2018, Poland ilikusanya kiasi cha Euro milioni 1, 875 kwa ajili ya Injili ya upendo na huruma kwa vijana, maskini na wale wote wanaotoka katika mazingira magumu.

Baraza la Maaskofu Katoliki Poland limezindua pia maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II, aliyesimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha Injili ya familia inayofumbatwa katika Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo! Maaskofu nchini Poland wametumia maadhimisho haya, ili kuwafahamisha vijana wa kizazi kipya ushuhuda wa utakatifu uliotolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II. Kilele cha maadhimisho haya ni hapo mwaka 2020. Maaskofu wanakazia umuhimu wa sala katika maisha ya ndoa na familia; upendo kwa Kanisa la Kristo pamoja na kuendelea kukuza Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa. Maaskofu wanawataka watu wa Mungu nchini Poland kupambana na changamoto za maisha yao kwa kujikita katika ujasiri, busara, hekima na nguvu ya maisha ya kiroho, huku wakiendelea kujiaminisha kwa nguvu tendaji ya Roho Mtakatifu.

Jubilei 100 JPII

 

15 October 2019, 12:03