Tafuta

Vatican News
Chama cha Mwenye heri Padre  Carlo Gnocchi wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 31 Oktoba 2019 Chama cha Mwenye heri Padre Carlo Gnocchi wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 31 Oktoba 2019  (Vatican Media)

Chama cha Gnocchi ni wajumbe wa huruma kwa wadhaifu!

Msichoke kamwe kuhudumia walio wa mwisho katika mpango wa wagonjwa na walemavu.Ndiyo ulikuwa moyo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko kwa wajumbe wawakilishi wa Chama cha Mwenyeheri Padre Don Gnocchi,aliokutana nao mjini Vatican 31 Oktoba 2019.Chama hiki kimepeleka mbele urithi wake kama talanta muhimu katika kazi ya utume na uaminifu wa Injili.

Na Sr. Angela Rwezaul- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Chama cha Padre Carlo Gnochi kinachojikita katika hali halisi ya kutoa msaada wa kutunza na kijamii. Katika salam anakumbuka mwanzo wa chama hiki ambacho kimebubujika kutoka katika moyo wa padre wa kiambrosi. Aidha amakumbuka katika mahubiri wakati wa kutangazwa kwake kuwa  Mwenyeheri, Katika  misa iliyofanyika huko Milano miaka 10 iliyopita, Kardinali Tetamanzi alimtaja Padr ehuyo kama mwana shauku wa kutafuta Mungu na jasiri wa kutafuta mtu na maisha yake yote yalijikita katika kutafuta uso wa Kristo ambao ambao umo ndani ya uso wa kila binadamu.

Kwa  hakika Baba Mtakatifu amesema  yeye ni mtume wa huruma na upendo, mtumishi kwa namna ya kishujaa kwa watoto, vijana, masikini na wanaoteseka, tangu wakati wake wa kuanza huduma yake ya kikuhani akiwa na ari ya kufundisha. Aidha amesema jinis alivyojikita katika usimamizi wa Kanisa la kijeshi  ambaye alitambua ukatili wa vita ya Pili ya Dunia mapema akiwa mapakani wa Ugiriki na Albania, baadaye,Tridentina na janga la kikundi cha kijeshi kutoka  Urusi. Katika harakati za miaka mingi, chama hiki kimepeleka mbele urithi wake kama vile talanta muhimu na kuzidi maradufu katika kazi yake ya utume na uaminifu wa Injili.  Baba Mtakatifu Francisko anawapongeza kwa hilo, wakurugenzi na wahusika wa vituo mbalimbali madaktari, wahudumu, watu wa kujitolea na marafiki.

Aidha wao walikuwa pamoja na wagonjwa wao, ambao wanatunzwa katika vituo mbalimbali na familia zao ili kuthibitisha jitihada zao za kusaidia jirani katika mateso ya watu walio wadhaifu zaidi, kwa mtindo kama wa msamaria mwema na kwa njia ya mfano wa Mwanzilishi wake. Amewasihi sana wasichoke kuhudumia watu walio wa mwisho mbele ya magonjwa magumu na ulemavu, pamoja na tiba na manedeleo ya kifundi kwa ajili ya mwili, wajitoa wote kwa matumaini katika vituo vyao na majengo yao wakiwa ni madaktari wa kiroho kwa maana ya kufariji kwa huruma ya Mungu.

Mada muhimu na yenye  thamani ya kitaaluma ya afya na kila huduma kwa mdugu mgonjwa inajionesha dhahiri katika uwezo wa kujikita kutibu kwa mambo mawili mawili ambayo ni  ujuzi na huruma. Ujuzi ni kufanya  maandalizi yao na uzoefu wa kujisasisha: na yote hayo ni sasabu ya nguvu katika utoaji wa huduma kwa jirani anayeteseka. Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo  waendelee na safari yao katika jitihada ya kukuza ubinadamu na ambao ni mchango mkubwa unaohitajika katika utume  wa kuijilisha katika Kanisa. Kiukweli anasema tangazo la Injili ni zaidi sna aminifu kutokana na upendo wa dhati ambao mfuasi wa Yesu anajikita nao kushuhudia kwa imani Yeye. Ushuhuda wa kibinadamu na kikristo wa Mwenyeheri Padre Carlo Gnocchi, unayo tabia ya upendo kwa ajili ya watu walio wadhaifu,hivyo uwaongoze daima uchaguzi wao na shughuli zao. Bwana awawezeshe daima na kila mahali kuwa wajumbe wa huruma yake na faraja. Anawasindikiza kwa sala zake na kuwabariki.

31 October 2019, 14:01