Tafuta

Baba Mtakatifu akiwabariki watoto mara baada ya katekesi yake  Jumatano 30 Oktoba 2019 Baba Mtakatifu akiwabariki watoto mara baada ya katekesi yake Jumatano 30 Oktoba 2019 

Baba Mtakatifu:Roho Mtakatifu ni kiongozi wa utume wa Kanisa!

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko,tarehe 30 Oktoba 2019 amejikita kutafakari juu ya ukristo barani Ulaya na kukumbusha kuwa Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wa utume wa Kanisa kwa sababu anafungua mioyo na kuifanya imani iwe thabiti.Ameongozwa na somo la Matendo ya Mitume na kuona watu waliotajwa katika somo hilo,Paulo Sila,Lidia na askari Gereza.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kusoma  kitabu cha Matendo ya mitume inaonesha ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu yuko mstari wa mbele katika utume umisionari wa Kanisa. Ni yeye anayeongoza hatua za uinjilishaji kwa kuwaonesha wao njia za kufuata. Hiyo inaonesha wazi wakati mtume Paulo amefika Troa na kupokea maono, kwa maana alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi na kumwambia, “vuka, uje Makedonia utusaidie” (Mdo 16,9).  Ndiyo mwanzo wa takafakari ya Baba Mtakatifu katika katekesi yake ya kila Jumatato tarehe 30 Oktoba 2019 kwa mahujaji na waamini waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, n amara baada ya kusoam somo kutoka katika matendo ya mitume 16, 9-10.

Watu wa wamekedonia wanajivunia kuhubiriwa na Mtakatifu Paulo

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari hiyo amesema, watu wa Makedonia ya Kaskazini wanajivunia hilo, wanajivunia sana kumuita Paulo kuwa ndiye aliyekwenda kutangaza Yesu Kristo.Hata hivyo amewakumbuka juu ya watu hao walio mpokea kwa shauku kubwa wakati wa hija yake nchini humo  na ambao  amethibtisha bado wanaonesha  imani kubwa sana ya  kuhubiri na Paulo! Mtume Paulo  hakujizuia, alikwenda huko makendonia, akiwa na uhakika kwamba ni Mungu anamtuma akafika  Filipi, lililo kuwa ni koloni la Warumi” (Mdo 16,12) na ili kuhubiri Injili. Paulo alisimama hapo kwa siku. Hata hivyo Baba Mtakatifu amebainisha kwamba ni matuki matatu yaliyotukia akiwa Filipi na muhumu katika maisha yake.

Matukio matatu kwa  Paulo akiwa Filipi

Tukio la kwanza lilikuwa ni uinjilishaji na ubatizo wa Lidia na familia yake; Pili kukamatwa na kupigwa bakora pamoja na Sila, baaada ya kumtoa pepo kijakazi aliyekuwa amepagawa na akinyonywa na mabwana zake; na hatimaye tukio  la tatu ni  uongofu  na ubatizo wa askari gereza na familia yake. Haya ndiyo matukio matatu ya maisha ya Paulo huko Filipi. Kwa maana hiyo  uwezo wa Injili unajieleza awali ya yote kwa wanawake wa Filipi kwa namna ya pekee Lidia aliyekuwa ni mfanya biashara ya kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa  mji wa Thiatira, mcha Mungu ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo (Mdo 16,14). Kiukweli Lidia anampokea Kristo, amesema Baba Mtakatifu na kuendelea, anapokea ubatizo pamoja na familia yake na kuwapokea wale wote ambao ni wa Kristo kwa anamna ya kuwakarimu Paulo na Sila katika nyumba yake.

Ushuhuda unaingia Barani Ulaya

Baba Mtakatifu Francisko anasema kufuatia na tukio hili ndipo hapa ushuhuda unaonekana kuingia ukristo katika bara la Ulaya. Mwanzo wa mchakato wa utamadunisho na ambao unaenelea kudumu hata leo hii, ulioingia Makedonia. Baada ya uzoefu wa ukarimu uliofanywa  katika nyumba ya Lidia, Paulo na Sila walijikuta wanakabiliana na ugumu wa gereza. Na hii ni kuonesha kuwaa walitoka katika faraja   na uongofu wa Lidia na familia yake, na sasa  inajitokeza upweke katika gereza mahali ambapo walitupwa ndani humo, mara baada ya kumtoa pepo kwa jina la Yesu kijakazi aliyekuwa na pepo wa uaguzi na  aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua (Mdo 16,16).

Baba Mtakatifu anasema mabwana hawa walikuwa wanapata faida sana na kijakazi huyo masikini aliyekuwa akiendelea na uaguzi  kwa kuwatabiria watu wakati ujao huku akiwatazama mikono yao. Ametoa mfano mmoja wa kukumbuka kuwa katika jimbo lake anakotoka , zamani katika uwanja mkubwa sana kulikuwapo na meza zaidi ya 60 ambazo walikuwa wanakaa wale ambao wanasema ni watabiri wa kike na kiume huku wakisoma mikono ya watu na watu waliamini mambo haya! Na walilipa. Kwa maana hiyo hii hata hali kama hiyo ilikuwa inatokea nyakati za Mtakatifu Paulo. Baada kupneshwa huyo kijakazi mabwana  walimshitaki Paulo na kuwapeleka mitume mbele ya wakuu wa mji na makadhi kwa kuwasingiza uongo kuwa wanachafua mji na na wanatangaza habari zisizokuwa halali.

Lakini ni kitu gani kilitokea

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na takafari yake anasema, je ni kitu gani kilitokea? Wakati Paulo yuko gerezani kulitokea jambo la kushangaza. Alikuwa na upweke lakini siyo wa kulalamika. Paulo na Sila walianza nyimbo za kusifu Mungi, na sifa hii iliweza kufungua nguvu na kuokoa. Wakati wa sala yao, waksikia mtetememo wa misingi ya gereza,  milango na minyororo yao ikafunguka ( Mdo 16,25-26). Ilikuwa kama vile sala ya Pentekoste, hata hii iliyokuwa inafanyika ndani ya gereza ilisababaisha miujiza hiyo. Askari gereza akifikiri wafungwa wamekimbia, alikuwa karibu ajiue mwenyewe kwa sabababu walinzi walikuwa lazima walipe gaharama ya  maisha yao iwapo ingetokea mfngwa kutoroka na kukimbia: lakini Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa (mdo 16,27-28). 

Na kwa maana hiyo akawaleta nje akasema, “yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? (Mdo16, 30).  Jibu ni “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na familia yako (Mdo 16, 31-32). Na wakati huo huo ikatokea mabadiliko, katika moyo wa usiku, askari alikuwa anasikiliza Neno la Bwana pamoja na familia yake, na wakawapokea mitume na kuwasafisha majeraha yao, kwa sababu walikuwa wamepigwa bakora  na kwa pamoja wakapokea ubatizo; Paulo na Sila  katika nyumbani yake, waliwaandalia chakula, wakafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, (Mdo 16, 34), Hiki ni kipindi cha faraja ! anasema Baba Mtakatifu. Katika moyo wa usiku,  askari asiyejulikana jina, katika mwanga wa Kristo anaangazwa na kuondoa giza nene. Minyororo ya moyo inaanguka na kuchanua yeye na familia yake ile furaha ambayo hawakuwahi kuipata.

Kuomba roho mtakatifu ili kuwa na moyo wazi, nyeti, ukarimu, imani na ujasiri

Baba Mtakatifu Francisko akihitimisha anasisitiza zaidi kwamba tuombe roho Mtakatifu anayefanya umisionari tangu mwanzo  wa Pentekosta na kuendelea;  ni yeye aliye mstari wa mbele katika utume wa Kimisionari. Ni yeye anayetupeleka mbele na hivyo inahitaji kuwa waaminifu wa wito ambao Roho Mtakatifu anatuonesha kufanya na kupeleka mbele Injili. Kwa maana hiyo tumwombe hata sisi leo hii Roho Mtakatifu atufanye tuwe na moyo uliofunguka, nyeti kwa Mungu na wa ukarimu kwa ndugu zake, kama ule wa  Lidia na imani thabiti kama ile ya Paulo na Sila, pia moyo uliowazi, kama ule wa askari gereza aliyejiruhusu kuguswa na Roho Mtakatifu.

30 October 2019, 13:08