Na sisi je mienendo yetu ikoje kwa ndugu zetu hasa wale wasiyo kuwa wakristo? Sisi ni kizingiti chao cha kukutana na Mungu?Tunazuia kukutana kwao na Baba au tunawawezesha? Na sisi je mienendo yetu ikoje kwa ndugu zetu hasa wale wasiyo kuwa wakristo? Sisi ni kizingiti chao cha kukutana na Mungu?Tunazuia kukutana kwao na Baba au tunawawezesha? 

Papa Francisko:uinjilishaji ni njia mwafaka ya kukutana na Mungu!

Acha ushangazwe na Mungu bila kumwekea vikwazo katika ubunifu wake.Ndiyo neema ambayo Baba Mtakatifu Francisko ameiomba asubuhi wakati wa tafakari ya Katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro Vatican, arehe 16 Oktoba 2019,huku akiongozwa na Neno la Mungu kutoka somo la Matendo ya Mitume,ambapo ametazama sura ya Petro(Mdo 10,34).

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Safari ya Injili duniani ambayo Mtakatifu Luka anasimulia katika Kitabu cha  Matendo ya Mitume imesindikizwa na ubunifu mkuu wa Mungu ambaye anajionesha kwa namna ya kushangaza. Hilo ndilo kusudi hasa kushinda vile vikwazo na kujifungulia wigo la wokovu  ulimwengu, kwa sababu Mungu anataka kuokoa kila mtu. Wote waliozaliwa kwa maji na Roho, wamebatizwa na wanaalikwa kutoka nje binafsi na kujifungulia kwa wengine; kuishi ukaribu na kuwa na mtindo wa maisha ya kuishi pamoja ambayo yanabadilisha kila uhusiano kati ya mtu kuwa na uzoefu wa kindugu (Wosia wa Evangelii gaudium, 87). Ndiyo mwanzo wa Tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi wakati mwendelezo wa Katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro Vatican, tarehe 16 Oktoba 2019, mara baada ya ksomwa Neno la Mungu kutoka  somo la Matendo ya Mitume,lilijikita kutazama sura ya Petro  (Mdo 10,34).

Ushuhuda wa kidugu

Ushuhuda wa mchakato wa kidugu ambao Roho anautaka uwe katika historia ni Petro, aliye mstari wa mbele katika Kitabu cha Matendo ya Mitume pamoja na Paulo. Petro anaishi tukio ambalo ni muhimu  la kubadili kuishi kwake. Kwani wakati alikuwa anasali, ilimtokea maono ambayo yalimfanya kuwa kama kichochezi cha kimungu, ili kumfanya abadilishe mawazo yake, amesema Baba Mtakatifu. Aliona kitambaa kirefu kikishuka toka juu kikiwa na kila aina zote za wanyama wenye miguu minne, wale watambaao na ndege wa angani,  na kisha sauti ikamjia, kuwa aondoke achinje na ale nyama ile. Yeye alikuwa ni Myahudi mkeleketwa wa kweli kwa maana alikataa asile kitu kilicho kichafu au najisi kwa mujibu wa Sheria ya Bwana (Walawi 11). Kwa maana hiyo ndipo sauti kwa nguvu tena ikamwambia “vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi. (Mdo 10,15). Katika tukio hilo, Baba Mtakatifu Francisko anasema, Bwana anataka Petro hasitathimini tena matukio na watu kwa mujibu wa aina ya usafi na uchafu, lakini kwamba ajifunze kwenda mbali zaidi,  ya kumtazama mtu na nia ya moyo wake. Kinachomfanya mwanadamu kuwa mchafu kiukweli, hakitoki nje, bali ni kutoka ndani ya   moyo wa mtu (Mk 7,21), anasema Yesu waziwazi.

Roho Mtakatifu anashuka katika nyumba ya kipagani

Mara baada ya maono hayo, Baba Mtraktifu ameendelea kusema, Mungu alimtuma Petro kwenda katika nyumba ya  mgeni  Kornelio, aliyekuwa akida, lakini mtu mwenye haki na mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, na ambaye alikuwa anatoa sadaka kwa watu na kusali daima kwa Mungu (Mdo 10,1-2), lakini hakuwa Myahudi. Katika nyumba hiyo ya kipagani Petro alihubiri Kristo msulibiwa na mfufuka na anayeondoa dhambi kwa kila amwaminiye. Wakati Petro anazungumza, juu ya Kornelio na familia yake Roho Mtakatifu alishuka. Na petro aliwabatiza hapo kwa jina la Yesu Kristo (Mdo 10,48). Tukio hilo maalum lilikuwa kwa mara ya kwanza kutokea na kujulikana  huko Yerusalemu, ambapo ndugu,walishtushwa na tabia ya Petro na  wakamkemea vikali (Mdo 11,1-3).

Petro alikwenda mbali zaidi ya kasumba na sheria

Petro alifanya jambo ambalo alikwenda mbali zaidi na kasumba au mbali na sheria, na ndiyo maana walikuwa wakimkemea. Lakini baada ya mkutano na Kornelio, Petro alikuwa huru binafsi na zaidi ya muungano na Mungu na wengine, kwa sababu aliona mapenzi ya Mungu kwa njia ya matendo ya Roho Mtakatifu. Kwa maana hiyo, Petro anaweza kuelewa kuwa uchaguzi wa Israeli, siyo thawabu ya sifa ya kustahili, bali ni ishara ya wito wa bure wa kuwa mpatanishi wa baraka ya kimungu kati ya watu wa kipagani. Baba Mtakatifu Francisko aidha amesisitiza kuwa, kutokana na  msingi wa Matendo ya Mitume, sisi sote tujifunze kuwa Uinjilishaji hauwezi kuwa na kuzuizi cha ubunifu wa Mungu ambaye anataka watu wote wakombolewe,(1Tm 2,4), badala yake  ndiye anayekuza  mkutano wa mioyo na Bwana! Lakini, swali linakuja kutoka kwa Baba Mtakatifu. “Na sisi je mienendo yetu ikoje kwa ndugu zetu hasa wale wasiyokuwa wakristo? Sisi ni kizingiti chao cha kukutana na Mungu? Tunazuia kukutana kwao na Baba au tunawawezesha? Kwa kuhitimisha amesema : “Tuombe leo hii neema ya kuacha kushangazwa na Mungu na bila kuzuia ubunifu wake, badala yake tuweze kutambua na kukuza njia mpya daima ambazo Mfufuka anavuvia Roho wake katika dunia na kuvuta mioyo na ili kuwafanya wajue kwamba Bwana ni wa wote(Mdo10,36).

16 October 2019, 12:25