Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa II wa Wana wa Mtakatifu Paulo Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa II wa Wana wa Mtakatifu Paulo 

Papa: Hata katika hali tete na nyeti, Injili inaweza kutangazwa!

Kutoka nje na kwenda kwa haraka,hasa kujikita katika njia ya kuelekea kwa wanaume na wanawake leo hii . Ushauri wa Papa aloioutoa alipokutana na Mabinti wa Shirika la Mt. Paulo. Miito inapungua, wazee wanaongezeka, lakini kwa njia ya Roho Mtakatifu inawezekana kutangaza Habari Njema hata katika nyakati ngumu na nyeti kwenda kila pembezoni mwa maisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawashiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wana wa Mtakatifu Paulo ambao  amewakaribisha wote kutoka mabara yote matano ili kushiriki Mkutano mkuu wa 11 wa Shirika hilo. Pia shukurani kwa Mama Mkuu wa Shirika kwa maneno yake. Mada waliyo chagua katika tafakari ya Mkutano wa Mkuu wao ni “amka na endeni ninyi, mkamtumikie Bwana (Dt 10,11) na amini ahadi zake”, Baba Mtakatifu anathibitisha, ni mada yenye nguvu ya kibiblia na ambayo inakumbusha uzoefu wa Musa na uzoefu wa Ibrahimu, kwa ujumla ni uzoefu wa watu wa Mungu. Historia ya wokovu iwe binafsi au ya watu inasimika mizizi katika uwezekano wa kuondoka, kuacha yote na kujiweka katika safari na si kwa ajili ya anzisho binafsi bali kama jibu la wito na kuamini ahadi. Ni uzoefu wa neema  tuliyopewa katika Yesu Kristo kama asemavyo Mtakatifu Paulo. Aidha "Siyo ninyi mlio nichagua mimi, bali mimi nimewachagua ( Yh 15,16)".  Hii inahusu si tu kwa ajili ya wito peke yake,  lakini hata kwa ajili ya uwepo wetu na wakati endelevu, kwa maana “ bila mimi hamwezi kufanya kitu (Yh 15,5)".

Baba Mtakatifu akiwatazama watawa kwamba katika nyakati hizi ngumu kama alivyo kuwa anasema Mtakatifu Yohane Paulo II katika Wosia wake wa Kitume wa Maisha ya Kitawa kifungu cha 13, kwamba kuna ulazima wa kuwa na imani. Wengi wanasema kwamba, maisha ya kitawa yanapitia wakati mgumu wa baridi kali. Baba Mtakatifu amesema, "inawezekana kuwa hivyo kwa sababu miito inapungua miaka inazidi kupita, na uaminifu wa shughuli ya kiakufu haiendani ambayo inapaswa iwe". Katika hali hiyo changamoto kubwa ni ile ya  kupitia kipindi cha baridi kali  na ili kuweza kufikia kuchanua na kutoa matunda. Baba Mtakatifu anatoa mfano kwamba , ubaridi katika jamii na wakati mwingine hata ndani ya Kanisa na katika maisha ya kitawa unatusukuma kwenda katika mizizi na kuiishi mizizi hiyo. Kipipwe kikali hata katika Kanisa na katika maisha ya kitawa, siyo kipindi cha utasa na kifo, lakini ni kipindi muafaka ambacho kinaruhusu kurudi katika mambo  yaliyo ya muhimu. Na kwa upande wao, Baba Mtakatifu Francisko anawashauri watafuta mabao yaliyo muhimu unabii wa Paulo, ili kugundua upya mchakato wa kitume na kimisionari, ambao hauwezi kukosekana kwa mtoto wa Mtakatifu Paulo, kwa namna ya kuweza kuishi katika pembezoni mwa mawazo na pembezoni mwa maisha.

Shirika lilizaliwa kwa ajili ya kutangazia wote njia ya mwanga wa maisha ambayo ni Injili ya Yesu Kristo na wao wanachukua vinasaba vya shauku ya kimisionari. Baba Mtakatifu anawashauri wasipunguze kamwe shauku hiyo kwa utambuzi kuwa aliye mstari wa mbele katika utume ni Roho Mtakatifu. Ni imani yake kwamba Mkutano wao mkuu unaweza kuwa ni fursa ya kujiuliza kwa jinsi gani wanafafanua unabii wa Mtakatifu Paulo katika kutoa jibu la wito ambao unakuja kutoka katika nyakati hizi?Hii inahusu kujiweka katika safari kwenye barabara ya ulimwengu  ukiwa na mtazamo wa kutafakari na kujazwa uelewa wa wanaume na wanawake wa nyakati zetu, wenye kuwa na njaa ya Habari njema ya Injili. Kuhisi kufanya kuwa sehemu ya Shirika linalotoka nje katika utume.

“amka na kuanza safari. Neno kuamka katika kigiriki “anastasis” maana yake ni ufufuko. Ni neno la Pasaka. Na ni neno la arusini  kama ilinavyoonekana katika Wimbo ulio bora ( 2,10.13) Amka na ujiweka katika safari ni kama Maria Magdalena siku ile asubuhi ya ufufuka ( Yh 20,1-2,); kama Petro na mfuasi mwingine walikimbia kwenda kaburini( Yh 20,3-4); na awali ya yote kama Maria alivyo kwenda kwa binamu yake Elizabeth (Lk 1,39). Kuanza safari kwa ari inatokana na roho Mtakatifu na ubunifu ambao ndiyo tabia ya mwanzisho wao.

Baba Mtakatifu amehitimisha kwa kuwakumbusha juu ya kila ambacho amesisitiza “ kutoka nje, kwenda kwa haraka kama Bikira Maria na Mtakatifu Paulo, na ndiyo wanavyo alikwa  wao kutangaza kwa maisha na matendo ya dhati ya kitume, Habari njema kwa wanawake na wanaume wa leo. Hakuna muda wa kupoteza “ ole wangu nisipoitangaza Injili (1Kor 9,16). Mtakatifu Paulo Mtume wa watu awasindikize, hata baraka yake kutoka rohoni mwake.

04 October 2019, 13:23