Tafuta

Mwenye heei Padre Alfredo Cremonesi alitangazwa mweheheri tarehe 19 Okotba 2019 huko Jimbo Kuu Crema, Italia Mwenye heei Padre Alfredo Cremonesi alitangazwa mweheheri tarehe 19 Okotba 2019 huko Jimbo Kuu Crema, Italia  

Mwenyeheri Padre Alfredo asaidie kuwa na chachu ya huduma kimisionari!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu amekumbuka kutangazwa mwenyeheri Mfiadini Padre Alfredo Cremonesi,padre mmisionari wa Taasisi ya Kitume ya Wamisionari wa Nje.Yeye aliuwawa huko Birmania kunako 1953,lakini alikuwa na mtume wa amani na shuhuda hai wa Injili hadi kufikia kumwaga damu yake anasema Baba Mtakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari yake na sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko tarehe 20 Oktoba 2019 kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro amewakumbusha kuhusu siku ya Jumamosi, ya kutangazwa mwenyeheri  Mfiadini Padre Alfredo Cremonesi, padre mmisionari wa Taasisi ya Kitume ya Wamisionari wa nchi za  Nje. Yeye aliuwawa huko Birmania kunako mwaka 1953, lakini alikuwa na mtume wa amani na shuhuda hai wa Injili hadi kufikia kumwaga damu yake, anasema Baba Mtakatifu. Kwa njia ya mfano  wake usaidie kuwa na msukumo wa kuwa  wahudumu wa kidugu na wamisionari jasiri  kwa kila mataifa. Na kwa njia ya maombezi yake yasaidie wale wote  wenye kuwa na ugumu wa kupanda mbegu ya Injili duniani. Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu ameomba watu wote wampigie makofi Mwenyeheri Alfredo!. ...

Msalaba wa Bwana wetu wa miujiza

Aidha amewageukia na kuwakaribisha mahujaji wote kutoka Italia na sehemu mbalimbali za dunia, huku akiwataja kwa namna ya peekee Jumuiya ya watu kutoka Peru wanaoishi Roma ambao walikuwa wamekusanyika kutokana na maadhimisho yao ya kila mwaka  kuhusu Picha ya Bwana wetu wa Miujiza (Señor de los Milagros); Baba Mtakatifu amewambia (conserven siempre la fe y las tradiciones de su pueblo (daima imarisheni imani na tamaduni za watu wenu)

Chama cha vijana katoliki Italia

Kadhalika katika salam zake Baba Mtakatifu Francisko hakusahau kuwakumbuka vijana wa  chama katoliki waliofika kutoka majimbo yote nchini Italia katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa  kwa chama cha vijana Wakatoliki Italia. “ wapendwa vijana ninyi mko mstari  wa mbele wa uinjilishaji, kwa namna ya pekee kati ya vijana rika lenu. Kanisa linawatumainia; nendeni mbele kwa furaha na ukarimu!  amesema Baba Mtakatifu. Na kwa wote amewatakia dominika njema huku akikazia  wasisahau kusali kwa ajili yake.

20 October 2019, 13:00