Tafuta

Vatican News
Baba Mtatifu ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa Club ya Amerika ya Mexico katika fursa ya kuadhimisha miaka 103 tangu kuanza kwake Baba Mtatifu ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa Club ya Amerika ya Mexico katika fursa ya kuadhimisha miaka 103 tangu kuanza kwake 

Ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video kwa Club ya Amerika!

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya Video kufuatia na tukio la maadhimisho ya miaka 103 tangu kuanza kwa timu ya mpira wa miguu nchini Mexico, kwa njia hiyo anawashauri wasali kwa ajili ya Mexico ili waweze kutembea katika njia fungamani na katika wema wa pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya video kwenye fursa ya maadhimisho ya miaka 103 ya Club ya America nchini Mexico, anasali kwa ajili ya umoja wa watu wa Mexico. Baba Mtakatifu anawakumbusha kuwa katika Timu ya Mexico inaunganisha mchezo na ufungamanisho kijamii kwa njia ya kuanzisha mambo mengi ya mshikamano.Wakati endelevu haujengwi na malalamiko, bali kwa njia ya maamuzi kama ya kwao, amesisitiza.

Umoja wa watu wa Mexico

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya salam zake kwa wanaclub wote wapendwa wa Jamhuri ya nchi ya Mexico na maeneo yote ya nchi kwa nafasi mbalimbali, mawazo yake yamejikita juu ya utafiti wa wema wa pamoja na njia ya  ufungamanishwaji kwa ajili ya kuimarisha umoja wa watu wa Mexico. Kutokana na hilo amesema kwamnba anasali kwa ajili ya watu wa Mexico ili mpendwa Bikira Maria wa Guardalupe aendelee kuwafunika chini ya vazi lake wasije kuangukia katika kupenda maslahi ya vikundi vidogo, bali zaidi wafurahie utajiri mkubwa wa  tamaduni na maono  ambayo yanapatikana katika ardhi yao nzuri ili  wapate  kuunganishwa vizuri. Na kwa kufanya hivyo Baba Mtakatifu amesema ni njia ya kushinda na kuweza kutafuta kwa pamoja ule wema ambao ni maalum kama ule ujumuishwaji kwa walio sahaulika.

Kutunza nyumba yetu ya pamoja

Baba Mtakatifu anafurahi sana kwamba katika maadhimisho ya mwaka huu Kardinali Carlos Aguiar Retes, Askofu Mkuu wa Mji kuu katoliki la Mexico amebariki kiota cha Tai na ili kuendeleza kuwa Tai halisi ambayo ni ishara ya Timu hiyo, na hivyo Baba Mtakatifu Francisko ametumia fursa hiyo kutoa nia yake hasa ya kuwaalika watunze nyumba yetu ya pamoja na kwamba ishara hiyo kwa niaba ya bioanuwai iweze kusaidia kujua hitaji la dharura la kutunza nyumba yetu ya pamoja. Iwe mazingira au watu, bila kutenga mtu yeyote, lakini ikiwa ni ni leo la utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja na katika kujaliana mmoja na mwingine!

28 September 2019, 16:18