Tafuta

Ziara ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko Jimbo Katoliki la Albano, Roma Ziara ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko Jimbo Katoliki la Albano, Roma 

Salam kutoka kwa askofu Semeraro kwa niaba ya waamini wa jimbo la Albano

Mara baada ya Misa takatifu ya Baba Mtakatifu Francisko katika uwanja wa Pia huko Albano,Askofu wa Jimbo katoliki Semeraro ametoa salam kwa niaba za waamini wote,huku akitoa shukrani na kuelezea maana ya tukio la maadhimisho hayo na hasa katika kufanya kumbukumbu ya siku ya kutabarukiwa Kanisa Kuu la Albano.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya Misa Takatifu, Askofu Marcello Semeraro wa Jimbo la Albano ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la makardinali 6 washauri wa Baba Mtakatifu ametoa salam kwa niaba ya wanajimbo huku akikimbuka matukio mawili ambayo yamewatia moyo kuomba ziara hiyo. Kwa upande mmoja tarehe 21 Septemba ambayo inakumbukwa sikukuu ya Mtakatifu Matayo, ambayo kwa hakika yanakumbusha hata wito wa Papa hadi kuw kuweka sentensi ya Mtakatifu Beda kwenye nembo yake ya kitume inayo tafakari wito wa Mtakatifu matayo. Sentensi hiyo inasema “Miserando atque eligendo” maana yake kuwa “alimtazama kwa hisia za upendo na kumchagua akisema nifuate”. Aidha tarehe hiyo pia inakumbusha ziara ya kichungaji aliyofanya Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kunako mwaka 2008, wakati wa fursa ya kutabaruku Kanisa kuu hilo na tangu wakati huo imekuwa tarehe ya kuadhimisha siku ya kumbukumbu yake.

Na kwa upande mwingine, Askofu Semeraro amesema ni kutaka kuimarisha uhusiano wa nguvu kati ya Jimbo katoliki la Albano na Roma, ambalo linasimika mizizi yake katika historia ya ukristo. Askofu amesema haya kama hawawezi kupata suluhisho la matatizo yote, lakini jitihada zao angalau ni kuacha ishara za matumaini, hasa kwa mtazamo wa matatizo ya wa watu na familia zenye matatizo. Kadhalika amekumbuka jitihada za Kanisa kwa wazalendo wa Mkoa wa Lazio ili kufikia pembezoni mwa maisha ya jamii za nyakati zetu, katika shughuli za kichungaji, na zaidi kwa kujikita katika mtindo wa kimisionari, ulioombwa na Baba Mtakatifu katika Wosia wake wa “Evangelium gaudium” yaani  Furaha ya Injili na ambayo ni mpango maalum wa utumishi wa Baba Mtakatifu Francisko.

Kadhalia askofu Semeraro hakukosa kuelezea juu ya jitihada zao za kutaka kuwa na moyo ulio wazi japokuwa na udhaifu wao katika kupindi cha mwaka wa kichungaji unao anaanza na kumwombaBaba Mtaktifu Francisko awaombee na kuwabariki shughuli. Amemshukuru kwa mara nyingine tena ujio wake katika mji huo na Kanisa la Albano.

22 September 2019, 10:40