Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Chama cha Italia cha Mtakatifu Cecilia (Scholae Cantorum)  yaani Shule ya nyimbo za kilatino kutoka pande zote za Italia Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Chama cha Italia cha Mtakatifu Cecilia (Scholae Cantorum) yaani Shule ya nyimbo za kilatino kutoka pande zote za Italia 

Papa Francisko:Muziki mtakatifu hujenga madaraja ya mbali

Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na Chama cha Italia cha Mtakatifu Cecilia (wanakwaya)amewakumbusha kwamba kufanya muziki katika Kanisa ni zawadi ya Mungu pia ni namna ya kuwasaidia waelewe ujumbe kikristo wale walio walio mbali.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican tarehe 28 Septemba 2019 na Scholae Cantorum  (Shule ya nyimbo) ya Chama cha Italia cha Mtakatifu Celicilia ambapo anashukuru Rais wa Chama hicho Monsinyo Tarcizio Cola kwa hotuba, Baraza la chama hicho, wanakwaya, waimbishaji wapiga vyombo vya muziki na anapongeza chama hiki cha Italia waliofika kutoka pande zote, ambacho ni cha kizamani kilichoundwa miaka 140 iliyopita na hadi leo hii kiko hai kinafanya kazi kwa mapenzi ya kuhudumia Kanisa. Baba anabainisha kuwa matokeo yake na pongezi kwao vilevile zimetolewa  mapapa kwa Chama hiki, kwa namna ya pekee Mtakatifu Pio X aliyeridhia kuanzisha kiungo hiki katika mantiki ya Muziki Mtakatifu na Motu Proprio:Tra le sollecitudini ya  22 Novemba 1903.

Naye Mtakatifu Paulo VI alitaka kupyaisha na ubunifu wa muziki ambao unafungamana na liturujia ambao unatoa maana na tabia yake msingi. Siyo muziki wote ule anasema Baba Mtakatifu , bali ni muziki mtakatifu kwa sababu watakatifu ni ibada; ni sanaa, kwa sababu Mungu anapaswa asifiwe vema; na  ulimwenguni kwa sababu wote waweze kutambua na kuadhimisha liturujia. Na zaidi liturujia iwe tofauti na ile ambayo inatumika kwa malengo mengine. Baba Mtakatifu anawahamasisha kukuza maana ya Kanisa kwa  kufanya mang’amuzi katika liturujia. Kuna msemo usemao, siyo kila kitu kina faa na wala kuwa halali na siyo kila kitu ni chema. Kwa maana hiyo muziki mtakatifu lazima ufike katika hali nzuri na ya umoja kwa maana ya kusali vizuri (Hotuba kwa watawa kuhusiana na wimbo wa liturujia, 15 Aprili 1971).

Aidha ameelzea kwamba Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliwashauri wasisahau urithi wa muziki wa wakati uliopita, kuupyaisha na kuukuza katika mitungo mipya. Na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko pia anawatia moyo wa kuendelea katika njia hiyo. Kuwa chama maana yake ni rasilimali inayowasaidia kujiunda katika utajiri wa kuhudumia liturujia vema. Ni  Chama ambacho siyo cha kujiweka kimbele mbele na ambacho hakina muziki wake binafsi, bali chenye kuwa na  mpango mmoja wa upendo na uaminifu wa Kanisa. Kwa pamoja wanaweza kujitahidi katika wimbo kama sehemu fungamani ya kiliturujia huku wakifuata mtindo wa kwanza ambao ni wa nyimbo za kilatino. Kwa pamoja kama wanavyo jiandaa vema katika sanaa na liturujia, wanahamasisha uwepo wa kwaya kila jumuiya ya Parokia,kuimba katika muungano wa misa na kurudia kwake  ambayo ni sauti muhimu ya kiroho, ya umoja, ya tamaduni na utamaduni wa liturujia Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu ameisistizia juu ya kusaidia watu wa Mungu ili kuimba na kushiriki huku wakiwa na utambuzi hai wa liturujia. Jambo hili ni muhimu hasa kwa ukaribu wa watu wa Mungu!

Jambo jema la muziki ni zana mwafaka kwa ajili ya kukaribia aliye juu na mara nyingi muziki unasadia kutambua vema ujumbe hata kwa yule ambaye amejisahau na yuko mbali. Baba Mtakatifu Francisko aidha anatambua shughuli yao ya kujiandaa ilivyo ya kujitoa sadaka kwa kuzingatia muda wa mazoezi, na kuwahusisha watu hasa wakati wa siku za sikuu na labda marafiki zao wanapokuwa wamewaalika kwenda kutambea. Lakini anasema kujitoa kwao kwa ajili ya  liturujia na katika muziki mtakatifu unawakilisha njia ya uinjilishaji kwa ngazi zote, kuanzia kwa watoto na watu wazima. Liturujia ni mwalimu wa kwanza wa katekisimu na wasisahau hilo amesisitiza. Pia muziki mtakatifu unayo kazi nyingine ya kuimarisha umoja wa  historia ya kikristo, kwani katika liturujia kuna nyimbo za kilatino, mchanganyiko na nyimbo za kisasa. 

Baba Mtakatifu Francisko ansema hii utafikiri kwamba wakati wa kusifu Mungu, kuna kizazi kilichopita na kilichopo kila mmoja na hisia zake. Na siyo tu muziki mtakatifu Baba Mtakatifu amesema, lakini muziki hata muziki kwa ujumla ambao unajenga madaraja na unaleta ukaribu wa watu hata walio mbali; muziki haujuhi mipaka ya kitaifa, kikabila, rangi ya ngozi, bali unaunganisha wote katika lugha kuu, na uwezesha  mara nyingi kuwaweka pamoja watu na makundi kutoka mbali na tofauti zao kubwa. Muziki mtakatifu unapunguza umbali hata kwa wale ndugu ambao mara nyingi tunahisi wako mbali. Kwa njia hiyo kila parokia katika kikundi chao ni kikundi ambacho kinauwezo wa kuonja uwezekano wao na msaada wa pamoja. Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru na kuwatia moyo ili Bwana awasaidie daima katika jitihada zao. Kanisa linapongeza huduma yao wanayoitoa katika jumuiya mbali mbali. Wanasaidia kuhisi uvutio na uzuri , katika  kuamsha nyoyo kwa Mungu pia  kuunganisha mioyo huku wakisifu huruma ya Mungu.

28 September 2019, 13:08