Tafuta

Vatican News
Tarehe 28 Septemba 2019 katika salam za Papa kwa vijana wa Praga kutoka Ureno amewaalika wasiwe na hofu ya kufanya mapinduzi ya huruma Tarehe 28 Septemba 2019 katika salam za Papa kwa vijana wa Praga kutoka Ureno amewaalika wasiwe na hofu ya kufanya mapinduzi ya huruma  (ANSA)

Papa Francisko:msiwe na hofu ya kufanya mapinduzi ya huruma!

Wakati wa kukutana na vijana wageni wa Kituo cha Kijamii cha Padre David de Oliveira Martins wa Braga,nchini Ureno,tarehe 28 Septemba 2019 katika salam zake amewaalika wasiwe na hofu ya kushiriki katika kufanya mapinduzi ya huruma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuwasalimia vijana wageni wa Kituo cha Kijamii cha Padre David de Oliveira Martins wa Braga, nchini Ureno, tarehe 28 Septemba 2019 mjini Vatican huku akiwaweka wote katika mawazo na sala watu wote ambao wanasaidia mradi ambao tangu mwaka 1958 unahesabu na kutekelezwa kwa zaidi ya nyumba 70 za kupokea masikini katika kuwasaidia kutatua matatizo yao ya kuishi na zaidi kutafuta namna ya kushinda  sababu za uwepo wa  majengo ya yatima. Wakiwa wamesindikizwa na Padre Manuel Joaquim, Mkurugenzi wa Kituo hicho karibu ya vijana 60 wameweza kujibu kwa shauku kubwa maswali na kusikiliza maneno ya Baba Mtakatifu Francisko tangu alipoanza na salam zake za kushukuru Padre huyo.

Mabalozi wa upendo

Baba Mtakatifu akianza na salam amesema kwamba kutoka Roma wao wataweza kupeleka salam zake kwa watu ambao wamewasaidia, ambao ni walimu wa mafunzo na kila aina ya huduma inayotolewa kwa watoto, vijana,  masikini na wazee. Ni kama mabalozi wa upendo walio nao kwa Kanisa, kwa ajili ya wema ambao wanataka yeye atende na wamewaza kuwatuma wadogo hao. Anamshukuru Padre Manuel Joaquim!

Kristo ni ufunguo wa kukabiliana na wakati uliopo na wakati ujao

Kama baba mkarimu na imara, Baba Mtakatifu Francisko amewakaribishi vijana hao na kama kuwapatia ufunguo wa kufungulia mioyo yao katika matumaini ya wakati ujao ili waweze kutambua maana ya maisha yao. Ufunguo ni Kristo anasema Baba Mtakatifu, “anayetembea karibu nasi na kutuongoza”. Safari yao imewapelekee kutazama kwa pamoja wakati endelevu na kwa maana hiyo wasijitazame wao peke yao binafsi. Kama anavyo fundisha Mtakatifu Paulo kwamba, wakati uliopo au ujao vyote ni vyake”. Ninyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu”. Hii ina maana ya kina katika historia ya maisha yao hadi leo, lakini zaidi ni ufunguo wa kukabiliana na wakati endelevu. Kwa wakristo daima kuwa katika sala na utunzaji wa ndugu kaka na dada walio wadogo zaidi. Aidha wasiwe na hofu ya kushiriki katika kufanya mapinduzi ambayo ni ya huruma. Kristo anatembea na anawaongoza.

Wabebaji wa huruma na upole

Katika kuhitimisha mazungumzo na vijana hao, Baba Mtakatifu Francisko anawashauri japokuwa ushauri huo ni kwa kila maisha ya kila kijana aliyekuwapo na wengine wote. Kamwe wasiruhusu  mambo ya zamani yawe ndiyo yanatoa uamuzi wa maisha yao ya sas ana endelevu. Wasubiri daima kwa shuku na matumaini. Wafanye kazi na kupambana ili kuweza kupata vitu ambayo wanatamani. Na kwamba hakuna yeyote kati yao ahisi kuwa peke yake; badala yake, ni juu ya kila mtu, aliyeumbwa kwa sura ya Kristo kuwa karibu na wengine. Na Mungu awapatie neema hiyo ya kuwa wabebaji rehema zake, huruma na upendo kwa wengine!

28 September 2019, 15:04