Papa Francisko:mchezo ni mkondo maalum kwa umasishaji wa amani!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Tarehe 27 Septemba 2019 katika salam za Baba Mtakatifu Francisko alipokutana mjini Vatican na Shirikisho la Kimataifa la mchezo wa Hockey kwenye barafu amebainisha juu ya Kanisa kupongeza mchezo kama uwanja ambao unaweza kuhamasisha fadhila ya busara, unyenyekevu, ujasiri, uvumilivu na ushuhuda wa kukutana na hali halisi nzuri na ya furaha. Katika mkutano karibu na wajumbe 176 wa Shirikisho la Kimataifa la mchezo wa Hockey, Baba Mtakatifu amethibitisha kwamba Mchezo ni mkondo kwa dhati maalum wa kuhamasisha amani na umoja.
Na wakati huo huo anamekumbusha umuhimu wa kisheria na kuheshimu washindani.Tabia za kisasa wakati mwingine zinapelekea shughuli za michezo kwenye njia mbaya, japokuwa inabidi kuzingatia kwamba sheria zipo kwa ajili ya kuhudumia ili kufikia lengo lake kwa kuepuka kudumbukia katika machafuko. Wanariadha huheshimu mchezo mzuri sio tu wanapofuata sheria, lakini pia wanapofuata haki na heshima kwa wapinzani wao ili washindani wote waweze kushiriki kwa amani kwenye mchezo huo.
Baba Mtakatifu akikumbuka ugeni uliomtembelea mwezi Mei mwaka huu wa shirikisho wakati wa kutolewa idhini ya kanuni zilizosasishwa, anathibitisha furaha yake ya kwamba kamati mpya ya maadili iliingizwa. Kama mchezo wa timu, Hockey ni mfano mzuri pia mchezo ambao unaweza kujifafanua kwa maana ya kukaa pamoja hata katika fursa ya furaha ya kukutana kati ya watu wa Nchi Tofauti kwa mfano kukutana na mashindano ya michezo duniani. Kwa njia hiyo mchezo ni nafasi ya kukua na katika maendeleo fungamani. Kwa upande mwingine, mchezo kwa kawaida unasaidia watu kuwa bora zaidi ndani mwao na kukuza uhusiano wa kirafiki.
Ki ukweli kufanya mazoezi ya hockey kwenye barafu inahitaji nguvu na ustadi, usawa, kwa kufuata maelekezo, kuanguka na kuamka tena baada ya kuteleza na kuanguka. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amewatia moyo ili lengo la viongozi wa mchezo wa Hockey kwenye barafu usiwe tu ni kudhibiti sheria, lakini ni kuifanya ujumuishe na kuonekana ulimwenguni kote. Na ndiyo hiyo njia ambayo wote wanaalikwa kuifuata,amehitimisha.