Tafuta

Papa amekutana mjini Vatican na wajumbe wa Kongamano la Chama kwa ajili ya Haki za  kisheri za Makanisa ya Mashariki Papa amekutana mjini Vatican na wajumbe wa Kongamano la Chama kwa ajili ya Haki za kisheri za Makanisa ya Mashariki 

Papa Francisko kwa Makanisa ya Mashariki:tafuteni njia za kuekelea katika umoja kamili!

Majadiliano ya kitaalimungu ya sasa kati ya Kanisa Katoliki na Makanisa ya Kiorthodox yanatafuta uelewa wa pamoja katika ukuu wake na upamoja wa huduma ya umoja wa Makanisa.Ndiyo mada kuu ya mkutano wa Baba Mtakatifu Francisko na washiriki wa kongamano kwa ajili ya Haki za kisheria za Makanisa ya Mashariki,aliokutana nao mjini Vatican,tarehe 19 Septemba 2019

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 19 Septemba 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Kongamano lililoandaliwa na Chama cha Haki ya kisheria ya Makanisa ya Mashariki. Katika hotuba yake amesema shughuli ya mafunzo ni msingi wa kusadia majadiliano ya kiekumene ambayo yamesadia kwenda mbele Chama hicho, kinacho unganisha wataalam kutoka makanisa mbalimbali ya nchi za Mashariki, Kanisa katoliki na  Kanisa la Kiorthodox. Akiendelea na hotuba hiyo kwa karibia washiriki 80 na ambao wanaadhimisha pia miaka 50 tangu kuanza kwa Chama hicho amesema ni mambo mangapi tunaweza kujifunza kwa kila mmoja nyanja  zote za maisha ya Kanisa, kuanzia taalimungu, hadi kufikia katika maisha ya kiroho; kuanzia liturujia hadi  kufikia maisha ya shughuli za kuchungaji, hata katika nyanja za haki za sheria. Hata hivyo kuhusiana na suala la haki ya sheria amesisitiza umuhimu wa majadiliano na ambayo yanasaidia kwa mara nyingine tena kuweka bayana kwa namna ya kuishi na kutenda.

Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko ameangazia mada ya Mkutano wao iliyo waongoza katika Taasisi ya Kipapa ya Makanisa ya Mashariki, ambayo ilikuwa inasema: “Miaka 50 ya kukutana kati ya makanisa ya Mashariki: kuna haki ya sheria katika kuchangia majadiliano ya kidini.” Kwa upande mwingine inawezekana kujifunza kutokana na uzoefu wa mikutano na tamaduni nyingine, hasa za Makanisa ya mashariki na kwa upande mwingine, Baba Mtakatifu amesisitiza, ni kwa namna ipi Kanisa linaishi ki-muungano na ambapo ni muhimu kwa ajili ya uhusiano wake na wakristo wengine. Hii ni changamoto ya kiekumene na ambayo jitihada za kujenga Kanisa la upamoja zinahitajika sana, kwa  kuangazia hotuba yake kunako 2015 wakati wa fursa ya maadhimisho ya  miaka 50 ya tangu kuanzishwa  kwa Taasisi ya Sinodi ya Maaskofu

Kwa kutazama kwa kina juu ya urithi wa pamoja wa sheria ya kwanza ya millenia, majadiliano ya kitaalimungu ya sasa kati ya Kanisa katoliki na Kanisa la Kiorthodox Baba Mtakatifu  amejaribu kuweka wazi uwelewa wa pamoja katika ukuu na ule upamoja kati ya huduma za umoja wa Kanisa. Kadhalika amebainisha juu ya mafunzo yao kwa jinsi yalivyokuwa na ukuu wa kisinod , kwa maana wao wanatembea kwa pamoja katika kusikilizana, kukabiliana kuhusu tamaduni na uzoefu wao ili kuweza kupata njia za kuelekea katika mchakato wa umoja kamili. Baba Mtakatifu ameonesha furaha ya kazi yao ambayo ana uhakika kwamba inaweza kuwa msaada mkubwa na siyo tu kwa ajili ya maendeleo ya haki ya sheria lakini zaidi ya yote kwa ajili ya ukaribu katika utimilifu wa sala ya Bwana:“ Ili wote wawe wamoja ,… na dunia ipate kuamini”. (Yh 17, 21). Na katika Chama hiki, Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha kwa kukibariki kwa Baraka takatifu na kuwakabidhi chini ya ulinzi wa Bikira Maria.

19 September 2019, 13:22