Baba Mtakatifu ameadhimisha Misa takatifu mjini Vatican katika maadhimisho ya Siku ya wahamiaji na wakimbizi 2019 Baba Mtakatifu ameadhimisha Misa takatifu mjini Vatican katika maadhimisho ya Siku ya wahamiaji na wakimbizi 2019 

Papa Francisko:ukosefu wa haki unazaa ubaguzi.Hatuwezi kubaki na sintofahamu!

Katika Misa ya maadhimisho ya Siku ya 105 ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka2019,iliyoongozwa na Papa Francisko Jumapili,tarehe 29 Septemba,kati ya mahubiri anasema,sambamba na zoezi la upendo wa dhati kwa jirani,Bwana anataka tutafakari juu ya ukosefu wa haki unaozaa ubaguzi hasa kuhusu fursa za walio wachache.Hatuwezi kubaki na sintofahamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 29 Septemba 2019 ameongoza misa Takatifu katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican katika fursa ya kuadhimisha Siku ya 105 ya  Wahamiaji na Wakimbizi duniani. Uwanja wa Mtakatifu Petro ulionekana rangi za kila nchi na watu mbalimbali katika madhimisho hayo, kwa nyimbo na furaha na vifijo! Wakati  wa  mahubiri yake ameanza  kusema  kuwa Zaburi imekumbusha kwamba Bwana anasaidia wamahamiaji pamoja na wajane na yatima. Mzaburi anatoa sauti kwa niaba ya kuwakilisha wale ambao kwa namna ya pekee ni waathirika  na mara nyingi wanabaguliwa. Wahamiaji, wajane na yatima ni wale wasio kuwa na haki, wanaobaguliwa na kuwekwa pembezoni ambao  na ambao Bwana kwa namna ya pekee anakuwa ndiye msaada wao. Kwa maana hiyo Mungu anawaomba Waisraeli wawe na umakini maalum kwa ajili yao.

Katika kitabu cha Kutoka Bwana anawaonya watu wasiwatendee kwa namna yoyoye ili mbaya wajane na yatima, kwa maana yeye anasikiliza kilio chao (Kut 22,23). Onyo hilo pia limetumiwa mara mbili katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati 24,17;27,19, Baba Mtakatifu anaongezea kusema kuwa  Wahamiaji ni kati ya wale wanostahili kulindwa. Na sababu ya onyo hilo imeelezwa wazi katika kitabu hicho. Mungu wa Israeli ni yule ambaye anamtendea haki yatima na mjanae, anampenda muuhamiaji na kumpatia chakula na mavazi (10,18). Wasiwasi wa upendo huo kwa wasio na fursa unawakilishwa na tabia ya Mungu kwa Israeli, hata kufanya kuwaombea kama uwajibu wa kimaadili na kwa watu wote ambao wanataka kuwa sehemu ya watu wake.

Kutokana hiyo  Baba Mtakatifu Francisko anaasema ndiyo maana ya kuweza kuwa na umakini kwa namna ya pekee kwa wahamiaji kama ilivyo pia kwa wajane, yatima na wote wanaobaguliwa katika nyakati zetu. Katika Ujumbe wa Siku ya 105 Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa mwaka 2019, anasema, kuna kiitikio cha  mada isemayo  Si Wahamiaji peke yao. Na hiyo ni kweli kwamba si wahamiaji  peke yao, kwa maana hii inagusa hata wakazi wote wa pembezoni mwa maisha  ya jamoo ambapo pamoja  na wahamiaji na wakimbizi ni waathirika wa utamaduni wa ubaguzi. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba, Bwana anatutaka kujikita  katika matendo ya upendo wa dhati mbele yao; anaomba uwezo wa kukarabati ubinadamu pamoja na uhuru bila kubagua mtu na bila kuacha yeyote nyuma. Lakini sambamba na zoezi la upendo wa dhati, pia Bwana anatuta kutafakari juu ya ukosefu wa haki ambao unazaa ubaguzi, kwa namna ya pekee kuhusu fursa za walio wachache ambazo zinawanyima walio wengi. Huu ni ukweli unaoleta uchungu katika  Dunia ya sasa ambayo kila siku iko na  wasomi zaidi, wakatili  pamoja na waliobaguliwa. Nchi zinazoendelea zinabaki kuchukua rasilimali za asili na ubinadamu kwa ajili ya faida ya walio wachache tu kwenye masoko yenye bahati.

Baba Mtakatifu amesema, vita vinatazama baadhi ya kanda za dunia, lakini silaha za vita hivyo zinatengenezwa na kuuzwa katika kanda nyingine ambazo matokeo yake  wanakataa kubeba mzigo wa wakimbizi  ambayo ni matokeo ya migogoro hiyo. Hata hivyo wanaoteseka mara nying ni wadogo, masikini na walioathirika zaidi na ambao wanazuiwa kukaa mezani na kuwachiwa angalau mabaki ya chakula mezani (Ujumbe wa siku ya 105 ya wahamiaji na wakimbizi duniani). Kutokana suala hili,  inawezekana kuelewa maneno magumu ya nabii Amosi yaliyosomwa katika Somo la Kwanza (6,1.4-7). “Ole wao wanao starehe katika Sayuni”, Baba Mtakatifu anaongezea, ambao hawaangaikii uharibifu wa watu wa Mungu, wakati huo huo yote hayo yapo machoni pa wote. Watu hao hawashituki juu ya uharibifu wa Israeli kwa sababu wanahangaikia sana kuwa na uhakika wa  ustawi wao ili kuishi vema kama vile, chakula cha hali ya juu na kunywa vinywaji safi. Ni jambo la kushangaza sana amesema Baba Mtakatifu, kuona kwa  umbali wa karne 28, ilizopita bado onyo kama hilo linagusa hata nyakati za sasa! Hata leo hii utamaduni wa ustawi (…) unatupelekea kujifikiria sisi binafsi na kutojali kilio cha wengine (...) unatupelekea kuwa na sintofahamu kwa wengine, na zaidi inatupelekea katika utandawazi wa sintofahamu (Mahubiri, Lampeduza, 8 Julai 2013).

Na mwisho wake Baba Mtakatifu anasema, kuna hatari ya kugeuka kama vile tajiri anayeelezwa kwenye Injili ya siku kuhusu kumtunza maskini Lazaro aliyekuwa amefunikwa na madonda na mwenye njaa huku akila makombo yaliyokuwa yanabaki mezani ( Lk 16,20-21). Ilikuwa rahisi kwa kununua nguo maridadi na kuandaa meza, tajiri katika Injili hakutazama mateso ya Lazaro. Hata sisi kutokana na kujali ustawi wetu, tuna hatari ya kutojali kaka na dada wenye mtatizo. Baba Mtakatifu amebainisha kwamba, kama wakristo hatuwezi kuwa tofauti mbele ya majanga ya kizamani na umaskini mpya, giza la upweke zaidi, madharau, ubaguzi kwa yule hasiye husika katika  kikundi mahalia. Hatuwezi kubaki tofauti na moyo wa ubaridi mbele ya majanga ya wengi wasio kuwa na hatia. Hatuwezi kuacha kulia. Hatuwezi kutofanya lolote. Tumwombe Bwana neema ya kulia machozi yanayoleta uongofu wa moyo mbele ya dhambi hizi.

Akiendelea kusisitiza Baba Mtakatifu Francisko amesema iwapo tunataka kuwa wanaume na wanawake wa Mungu, kama anavyotaka Mtakatifu Paulo kwa Timoteo, “tunapaswa kuilinda amri pasipo mawaa pasipo lawama”  (1Tm 6,14); na amri ya upendo ni kumpenda Mungu na kumpenda jirani. Hatuwezi kuitenganisha! Na kumpenda jirani kama nafsi yako, ina maana hata ya kuwajibika kwa dhati kwa ajili ya kujenga dunia iweze kuwa ya haki na mahali ambapo wote wanaweza kunufaika kwa mali ya ardhi; mahali ambamo wote wanaweza kujikamilisha kama mtu na kama familia; na mahali ambamo wote wanahakikishiwa haki msingi na hadhi. Kumpenda jirani maana yake nikuhisi huruma ya mateso ya kaka na dada, kuwakaribia, kuwafunika madonda yao  huku ukishirikishana nao historia ya katika  kuonesha kwa dhati, huruma ya  Mungu mbele yao.

Kuwa karibu na wasafiri waliopigwa na kuachwa katikati ya barabara ya dunia  ili kutuliza majeraha yao na kuwapeleka kwenye nyumba ya mapokezi, mahali ambamo wanaweza kusaidiwa mahitaji yao. Amri hiyo takatifu, Baba Mtakatifu Francisko amesema,  Mungu aliwapatia watu wa Mungu, aliweka muhuri kwa damu ya mwanae Yesu ili iwe kisima cha baraka kwa ubinadamu wote. Na ili wote tuweze kujikita katika ujenzi wa familia ya kibinadamu kwa mujibu wa mpango asili, uliooneshwa katika Yesu Kristo kwa ndugu wote na wana Baba Mmoja. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu amesema, leo hii tunamwitaji hata Mama, tumkabidhi mama Maria wa njia , katika njia nyingi za uchungu, tumkabidhi yeye wahamiaja na wakimbizi pamoja na wakazi wote wanaoishi pembezoni mwa dunia na wale ambao wanawasindikiza katika safari yao.

29 September 2019, 14:30