Baba Mtakatifu Francisko anampongeza Kardinali Bassetti kwa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu, hasa huduma yake miongoni mwa maskini! Baba Mtakatifu Francisko anampongeza Kardinali Bassetti kwa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu, hasa huduma yake miongoni mwa maskini! 

Papa ampongeza Kardinali Bassetti: Miaka 25 ya Uaskofu

Baba Mtakatifu Francisko amemshukuru Kardinali Gualtiero Bassetti, kawa bidii aliyoionesha katika maisha na utume wake amemtakia baraka za kitume katika jubilei yake na kumwombea neema ya Mwenyezi Mungu ili ziendelee kumwongoza katika utume wake, na aweze kuendelea kushuhudia upendo wa Mwenyezi Mungu katika huduma ya upatanisho! Huduma kwa maskini ni muhimu!

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni katika adhimisho la Misa takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Lorenzo huko Perugia, amempongeza Kardinali Gualtiero Bassetti kwa kuadhimisha jubilei ya dhahabu ya miaka ishirini na mitano ya uaskofu. Katika salamu zake za pongezi Baba Mtakatifu ameeleza hisia zake za kibaba akiguswa na sadaka kubwa ya utume inayotolewa na Kardinali Gualtiero Bassetti katika maisha na  utume wa Kanisa. Ikumbukwe kuwa, Kardinali Gualtiero Bassetti alizaliwa Marradi tarehe 7 Aprili 1942 katika jimbo Katoliki la Faenza Italia. Alilelewa na kupewa daraja ya upadre mnamo tarehe 29 Juni 1966. Baada ya upadrisho alihudumu katika Parokia ya Mtakatifu Mikaeli San Salvi kama msaidizi wa Paroko, na mwaka 1972 aliwekwa kuwa Gambera wa Seminari ndogo ya Firenze, mwaka 1990 akawa mkuu wa kanda na mwaka 1992 akawa makamu wa Askofu huko Firenze.

Katika kupitia historia ya maisha ya Utume wa Kardinali Gualtiero Bassetti, Baba Mtakatifu amempongeza kwa kazi nzuri alizozifanya katika malezi ya vijana wa Seminari ndogo na uzoefu wake kama makamu wa Askofu na mnamo tarehe 7 Julai 1994 aliwekwa wakfu kuwa Askofu na Mtakatifu Yohane Paulo II na kusimikwa kuwa Askofu wa Massa Marittima Piombino. Manamo tarehe 16 Julai 2009 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alimteua kuwa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Perugia, na tarehe 22 Februari 2014 aliteuliwa kuwa Kardinali na Baba Mtakatifu Francisko akisimamia Kanisa la Mtakatifu Sesilia. Katika kumbukumbu hiyo Baba Mtakatifu amemshukuru kawa bidii aliyoionesha katika utume wake amemtakia baraka za kitume katika jubilei yake na kumwombea neema ya Mwenyezi Mungu ili ziendelee kumwongoza katika utume wake, na aweze kuendelea kushuhudia upendo wa Mwenyezi Mungu katika huduma ya upatanisho.

Kwa upande wake Kardinali Gualtiero Bassetti akitoa salaam zake za shurani, amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa moyo wake wa ubaba pamoja na kujikabidhi mikononi mwa Mama Bikira Maria, mama wa neema ya Mungu. Aidha amewashukuru wakleri watawa na waamini wote kwa ushirikianao waliomuonesha katika kipindi chote cha utume wake. Akielezea furaha aliyoipata katika utume wake wa miaka 28 kama Padre amesema, alikumbana na vipingamizi vingi lakini vyote hivyo alivikabidhi mikononi mwa Mungu. Akiwataja baadhi ya Makardinali waliogusa kwa namna ya pekee moyo wake, alimtaja Kardinale Silvano Piovanelli aliyemweka wakfu kuwa Askofu. Akiwa mwingi wa shukrani kwa familia ya Mungu, amejikabidhi mikononi mwa ulinzi wa Mungu akiwaombea mwanga wa mapendo ya Kristo uwaangaze wakristo wa Firenze wadumu katika upendo wa kidugu.

Naye Kardinali Gualtiero Bassetti katika kuhitimisha hotuba yake amewakumbuka maskini, waliotengwa na jamii, wasio na matumaini kama sehemu ya utume wake akiiomba jamii kuwasaidia katika shida zao.  Tukio hilo limehitimishwa na salaam kutoka kwa Maaskofu zilizotolewa na mwakilishi wao Askofu msaidizi Marco Salvi ambaye ameeleza furaha kubwa waliyonayo Maaskofu katika kumpongeza kwa jubilei yake ya dhahabu ya Miaka 25 ya uaskofu. Aidha Askofu Marco Salvi amesema, tangu aondoke Massa Marittima kwenda Arezzo na baadaye Perugia, familia ya Mungu huko kote alikoishi inampongeza na kumshukuru sana kwa sadaka na majitoleo yake aliyoyaonesha. Aidha kwa namna ya pekee, Maaskofu wamemshukuru kwa utumishi wake uliotukuka kama Rais wa baraza la Maaskofu Katoliki la Italia.  Akipembua mada hiyo amesema, hakika Kardinale Gualtiero Bassetti amefanya kazi ya ziada, na kubwa katika Kanisa Katoliki zinazostahili pongezi na shukrani nyingi. Maaskofu wanaona kuwa ni wajibu wao kumpatia kardinale Gualtiero Bassetti iliyo haki yake. Katika kuelezea hali amesema, hawezi kusahau kazi kubwa aliyoifanya katika malezi ya mapadre, mashemasi na watawa.

Kardinali Bassetti
20 September 2019, 09:00