Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amehitimisha hija yake ya kitume nchini Mauritius kwa kuwashukuru watu wa Mungu katika kisiwa hiki cha amani kwa ukarimu na upendo wao kwake! Papa Francisko amehitimisha hija yake ya kitume nchini Mauritius kwa kuwashukuru watu wa Mungu katika kisiwa hiki cha amani kwa ukarimu na upendo wao kwake!  (Vatican Media)

Hija ya kitume ya Papa Francisko Mauritius: Utunzaji wa mazingira

Papa Francisko Kabla ya kuondoka kurejea tena mjini Antananarivo, Madagascar, alipata nafasi ya kukutana na kusalimiana na viongozi mbali mbali wa kidini na kwa pamoja kama kumbu kumbu endelevu ya ujio wa Baba Mtakatifu nchini Mauritius wakapanda miti na baadaye, Baba Mtakatifu akaelekea kwenye Uwanja wa ndege wa Port Louis na hatimaye kuwasili majira ya saa 2:10 za usiku.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Francisko, Jumatatu tarehe 9 Septemba 2019 amehitimisha hija yake ya kichungaji nchini Mauritius iliyokuwa inaongozwa na kauli mbiu “Hujaji wa amani”. Kabla ya kuondoka kurejea tena mjini Antananarivo, Madagascar, alipata nafasi ya kukutana na kusalimiana na viongozi mbali mbali wa kidini na kwa pamoja kama kumbu kumbu endelevu ya ujio wa Baba Mtakatifu nchini Mauritius wakapanda miti na baadaye, Baba Mtakatifu akaelekea kwenye Uwanja wa ndege wa Port Louis na hatimaye kuwasili majira ya saa 2:10 za usiku.

Baba Mtakatifu akiwa njiani kurejea nchini Madagascar amemtumia salam na ujumbe wa matashi mema Bwana Barlen Vypoory, Rais wa kipindi cha mpito nchini Mauritius akimshukuru kwa ukarimu na upendo alioonjeshwa na watu wa Mungu nchini Mauritius. Anawaombea heri na baraka tele, ili Mauritius iendelee kuwa ni “Kisiwa cha amani”. Alipokuwa anapita kwenye anga la Visiwa vya Rèunion, Baba Mtakatifu amemtumia salam na matashi mema Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, akiwaombea furaha na amani wananchi wote wa Rèunion.

Papa: Salam
10 September 2019, 14:46