Tafuta

Vatican News
Kila Dominika ya III ya kipindi cha kawaida cha mwaka,Kanisa litakuwa linaadhimisha, linatafakari na kutangaza Neno la Mungu kwa mujibu wa Papa Francisko na Barua ya motu proprio Kila Dominika ya III ya kipindi cha kawaida cha mwaka,Kanisa litakuwa linaadhimisha, linatafakari na kutangaza Neno la Mungu kwa mujibu wa Papa Francisko na Barua ya motu proprio 

Barua ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Motu proprio, Aperuit Illis

Itakuwa ni Dominika ya III ya kipindi cha kawaida cha mwaka ambayo imechaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuadhimishwa,kutangazwa na kutafakari Neno la Mungu.Katika Barua ya Motu Proprio “Aperuit illis” ya tarehe 30 Septemba Baba Mtakatifu anasisitiza sababu ya kutangaza hati hiyo,ikiwa pia ni kugundua kwa upya maana ya Pasaka na wokovu kwa njia ya Neno la Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika barua ya kitume yenye mtindo wa Motu proprio “Aperuit illis”, maana yake ni “vizuri sisi kuwapo hapa”, Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha kwamba Dominika ya tatu  ya kipindi cha kawaida cha mwaka itakuwa ni kufanya maadhimisho, tafakari na kutangaza Neno la Mungu. Barua hii imetangazwa tarehe 30 Septemba 2019 ikiwa  mama Kanisa anafanya kumbukumbu ya Mtakatifu Gerome, ikiwa ni mwanzo wa kufanya kumbu kumbu ya miaka 1600 tangu kifo chake, na ambaye anayejulikana sana kutokana na kuwa  ndiye aliye tafsiri Biblia katika lugha ya kilatino na ambaye anasema “kutojua maandiko matakatifu, ni kutojua Kristo”.

Baba Mtakatifu Francisko katika barua ya motu proprio  proprio “Aperuit illis anaelezea uamuzi wa kufanya hivyo kwamba ni kutokana na maombi mengi  yaliytokana na watu wa Mungu ili katika Kanisa waweze kuadhimisha Dominika ya Neno la Mungu.  Katika Barua hiyo Baba Mtakatifu anaanza na neno kutoka  Injili ya Luka (Lc 24,45) ambapo Yesu baada ya kufufuka aliwatokea mitume wakati wameungana pamoja  na yeye akaumega mkate na kuwafungua akili za Maandiko Matakatifu. Watu wale waliokuwa na hofu na kukuta tamaa na kwa maana hiyo anawapa maana ya mafumbo ya Pasaka, yaani kwa mujibu wa mpango wa ndani ya Baba, kwamba Yesu alitakiwa ateseke na kufufuka katika wafu ili kutoa uongofu na msamaha wa dhambi. Vile vile anatoa ahadi ya Roho Mtakatifu ambaye atatoa nguvu kwao na kwamba watakuwa mashuhuda wa Mafumbo hayo ya wokovu.

Baba Mtakatifu Francisko barua yake anakumbuka Mtaguso Mkuu wa   II wa Vatican  ambao ulitoa mwamko mkubwa katika kugundua kwa upya kwa  Neno la Mungu kwa njia ya Hati ya “Verbum Dei”, ihusuyo ufunuo wa Kimungu na ile ya Baba Mtakatifu Mstaafu  Benedikto wa XVI aliyeitisha Sinodi kunako 2008 ikiongozwa na kauli mbiu “Neno la Mungu katika maisha na katika utume wa Kanisa,”  na kuandikia Wosia wake wa Kitume “Verbum Domini” akikazia umuhimu wa Neno la Mungu katika Liturujia ya Kanisa,maadhimisho ya Sakramenti na mafumbo mbali mbali ya Kanisa, ambayo ni mafundisho muhimu katika jumuiya yetu. Aidha katika barua hiyo inaonesha tabia ya hali haisi ya Neno la Neno la Mungu hasa inapokuwa katika maadhimisho ya matendo ya liturujia na kujionesha katika sakramenti. “Domimika ya Neno la Mungu” anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko inajikita katika kipindi cha mwaka ambacho kinawaalika kuongeza nguvu ya mahusiano na wayahudi na kusali kwa ajili ya umoja wa kikristo. Hii si kwa bahati mbaya katika, maadhimisho ya Dominika ya Neno la Mungu kwa maana inajieleza kwa namna ya kiekumene, kwa sababu Maandiko matakatifu, yanaelekeza kwa wale wanaojikita katika kusikiliza katika safari ya kuendelea ili kufikia umoja wa dhati na msimamo.

Baba Mtakatifu Francisko anatoa ushauri wa kuishi domiika hiyo kama siku ya sikukuu. Itakuwa muhimu (…) ambapo katika maandhsimisho ya ekaristi inawezeakana kuweka pia somo takatifu, na kwa maanaa hiyo kuwawezesha waamini wote thamani ya kawaida ambayo neno la Mungu linabeba (…) Maaskofu katika Dominika hiyo wanaweza kuadhimisha ibada ya masomo au kuwakabidhi wahudumu wengine ili kukazia umuhimu wa kutangaza Neno la Mungu katika liturujia. Ni vema ya kwamba  jitihada zisipunguke kamwe ili kuwaandaa baadhi ya waamini kuwa watangazaji wa kweli wa Neno la Mungu wakiwa na maandalizi yakutosha (…) maparoko wanaweza kutafuta mtindo mwingine  kwa ajili ya kutoa Biblia au kitabu chao kwa watu wote kwa namna ya kufanya uonekane ule umuhimu wa kuendelea kusoma.

Katika maisha yao ya kila siku, kutafakari na kusali kwa njia ya  Maandiko matakatifu na kwa namna ya pekee hata  kutoa katekesi.Biblia, Baba Mtakatifu Frncisko anaandika haiwezi kuwa urithi kwa baadhi tu na wala kuwa mkusanyiko wa vitabu kwa ajili ya walio wachache (…) Hata hivyo anabainisha kuwa mara nyingi inaonesha tabia ambayo inatafuta kuhodhi maandiko matakatifu kwa kuyasoma kwa baadhi ya vikundi vidogo au vilivyojichagua. Haiwezekani kuwa hivyo, Baba Mtakatifu anasisitiza! Biblia ni kitabu cha watu wa Bwana ambapo katika kusikiliza ndipo inawezekana kutawanyika na kugawa umoja. Japokuwa Neno la Mungu linaunganisha waamini na kuwafanya wawe wamoja tu.

Hata katika fursa ya barua hii, Baba Mtakatifu anasisitiza umuhimu wa kuandaa mahuburi. Wachungaji wanao uwajibu mkubwa wa kufafanua na kuwezesha watu wote watambue Maandiko Matakatifu (…) Kwa kutumia lugha rahisi na inayofaa kwa yule anayesikiliza (…) Kwa walio wengi wetu, kaka na dada zetu kwa dhati ndiyo fursa waliyo nayo ya kupokea uzuri wa Neno la Mungu na  kuona kwamba linaelezea maisha yao ya kila siku (…) Haiwezekani kutafakari maandiko Matakatifu kwa ghafla, bali inahitaji muda wa kutafakari kwa kina Neno la Mungu. Kwa upande wa makuhani wanatakiwa jitihada zaidi ya kutohubiri kwa muda mrefu sana na wala masuala ambayo ni tofauti na Neno la Mungu. Unapokaa kitambo na kutafakari kwanza na  kusali katika andiko takatifu, ndiyo kuna uwezekano wa kuzungumza kutoka moyoni ili kufikia ujumbe ndani ya moyo wa watu ambao wanasikiliza.

Baba Mtakatifu Francisko katika hati yake ya Aperuit illis”,anakumba tukio  hata la mitume wakiwa njiani kuelekea Emau, hivyo anabainisha juu ya uhusiano uliopo kati ya Maandiko Matakatifu na Ekaristi.  Kwa maana hiyo anataja Hati ya Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican ya  Verbum Dei ambayo  inaonesha hatima ya wokovu, ukuu na mwanzo wa Mungu kufanyika Mwili katika maandiko Matakatifu. Biblia siyo mkusanyiko wa vitabu vya hisptia tu  na wala makala  ya magazeti, bali ni kitabu kinachoelezea kwa ujumla juu ya wokovu fungamani wa mtu. Kukataa mzizi wa kihistoria wa vitabu ambavyo vinaunda maandiko matakatifu, isiwafanye kusahau hata hatima ya kwanza yaani ya wokovu wetu. Yote hayo yanaelekeza katika hatima ya mwisho iliyopo katika asili ya Biblia na ambayo imeundwa kama historia ya wokovu kwani Mungu anazungumza na kutenda ili kuweza  kwenda kukutana watu wote na kuwaokoa na mabaya na kifo.

Ili kuufikia mwisho wa  wokovu huo, Maandiko Matakatifu chini  mwongozo wa kazi ya Roho Mtakatifu inabadili Neno la Mungu  katika maneno ya watu waliyo andika kwa namna ya kibinadamu. Nafasi ya Roho Mtakatifu katika Maandiko Matakatifu ni muhimu. Bila nguvu yake, ipo hatari ya kubaki yamefungwa katika andiko tu na hatari ya kuweza kutafisiwa vibaya na kutupeleka mbali nasi kwa kusaliti mwendo na tasaufi zilizoko zinazobebwa na takatifu. Na kama anavyokumbusha Mtume Paulo: maana sheria iliyoandikwa huleta kifo , lakini Roho huleta uhai (2Cor 3,6)”.

30 September 2019, 12:30