Katekesi ya Baba Mtakatifu tarehe 18 Septemba 2019 Katekesi ya Baba Mtakatifu tarehe 18 Septemba 2019 

Papa Francisko:Kinachotokana na mapenzi ya Mungu kinadumu!

Ujasiri wa mitume unatokana na Roho Mtakatifu na ndiyo ujasiri huo huo unawasaidia wafiadini leo hii.Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko,katika safu ya katekesi za kila siku ya Jumatano katika mwendelezo wa tafakari ya kitabu Matendo ya mitume.Kiini cha katekesi ya tarehe 18 Septemba 2019 imejikita kutazama zawadi ya mang’amuzi na maana ya kusikiliza Roho Mtakatifu ili kuona hatua za Mungu katika historia ya mwanadamu.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Katika mwendelezo wa Katekesi kuhusu Kitabu cha Matendo ya Mitume, tarehe 18 Septemba 2019 kwa waamini na mahujaji waliofika uwanja wa Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu anasema, vizuizi vya wayahudi ili wasiweze kufundishe kwa jina ya Yesu Kristo, Petro na Mitume wanajibu kwa ujasiri kwamba, hawawezi kutii anayetaka kuzuia safari ya Injili. Baba Mtakatifu Francisko amejikita katika tafakari yake kupitia somo linalomtaja mfarisayo mmoja aitwaye  Gamalieli aliyekuwa na uwezo wa kung'amua au kuwa na mamlaka katika kikao na kumtetea Petro na mitume wenzake ambao walikuwa wanataja Neno la Yesu katikati ya watu. Baba Mtakatifu anakumbusha jinsi ambavyo mitume hawa hawakutishiwa na  kuzuizi cha wayahudi wasihubiri hasa baada ya pentekoste, kwa njia  ya Roho Mtakatifu. Mitume kumi na mbili walionesha uwezo wao wa kushuhudia kwa imani na ambapo unajionesha hata kwa waamini wote (Rm 1,5). Na zaidi kuanzia siku ya Pentekoste, watu hako peke yao, anasisitiza Baba Mtakatifu, kwa maana wanashuhudia mkakati maalum ambao wanahisi kusema kuwa, “sisi na Roho Mtakatifu (Mdo 5,32) au Roho Mtakatifu na sisi (Mdo 15,28).

Roho Mtakatifu akiwa ndani mwetu

Huu ni ujasiri wa kipekee walio kuwa nao. Lakini ni lazima kufikiria ni kwa jinsi gani walivyo kuwa wajanja, kwa maana hawa wote walikimbia siku ile ambayo Yesu alikamatwa na askari, Baba Mtakatifu amebainisha. Lakini kutoka katika ujanja  huo, wao wanakuwa wajasiri. Je ni kwa nini namna hiyo? Ni kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa nao. Na hiyo inatokea hata kwetu sisi. Iwapo tunaye Roho Mtakatifu ndani mwetu, tutakuwa na ujasiri wa kwenda mbele, ujasiri wa kushinda mapambano, lakini si kwa njia yetu  tu bali kwa njia ya Roho Mtakatifu aliye ndani mwetu amekazia Baba Mtakatifu Francisko.

Ujasiri wa ushuhuda wa leo hii

Hata hivyo ushuhuda wa mitume wale, ni sawa swa na shuhuda wa wafiadini wa nyakati zetu, amebainisha Baba Mtakatifu na kutoa mfano kwamba : wafiadini , wanatoa maisha na  hawafichi kuwa wakristo. Fikirine ika kadhaa hata leo hii, wapo wengi, fikirieni miaka minne iliyopita, wakristo wa kikoptiki, wafanyakazi wa kweli katika fukwe za Libia: wote hao walinyongwa. Lakini neno la mwisho walilokuwa wanasema ni Yesu, Yesu. Hawakuuza imani yao, kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nao.

Kitokanacho na mapenzi ya Mungu kinadumu

Msimamo wa mitume unafanya kutetemeka mifumo ya kidini ya kiyahudi na kuzuka matendo ya kutumia vurugu na nguvu kama inavyojionesha hata leo hii katika sehemu ambazo wanapambania ukristo, Baba Mtakatifu amefananua. Katikati ya mahakama anaendelea, Gamalieli anaonesha ndugu zake ni kwa  jinsi gani ya kufanya utamaduni wa mang’amuzi hasa mbele ya hali halisi, ambayo inashinda mifumo ya kasumba, na  kuwakumbusha wao jinsi gani mpango wa kibinadamu hata kama mwanzo wake ni wa kusifiwa, lakini hatima yake itatoweka, wakati huo huo kwa chochote kitokanacho na mapenzi ya Mungu kitadumu. Mipango ya binadamu daima inashindwa, ina wakati kama sisi. 

Akitoa mfano Baba Mtakatifu wa kufikiria miradi na mipango ya kisiasa  na jinsi gani inavyo badilika kwa upande mmoja na mwingine  na katika nchi zote. "Fikirieni  falme kubwa, fikirieni udikteta wa karne iliyopita. Hawa walikuwa wanahisi kuwa wenye nguvu sana ya kutawala dunia nzima. Lakini baadaye wote walianguka. Fikirieni hata sasa falme za leo; zitaanguka iwapo Mungu hayupo pamoja nao kwa sababu nguvu za binadamu walizonazo peke yao siyo za kudumu. Ni nguvu ya Mungu peke yake iliyo ya kudumu! Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha hata katika historia ya Kanisa. Licha ya dhamiri nyingi na kashfa nyingi, Kanisa halikuweza kuanguka kwa sababu Mungu alikuwapo pale. Sisi ni wadhambi na mara nyingi tunatoa kashfa. Lakini Mungu yupo pamoja nasi. Mungu anatuokoa kwanza na baadaye wengine, lakini Bwana daima anaokoa.

Kuomba neema ya zawadi ya kujua ishara za Mungu

Gamalieli aliwaonya watu wa mahakama kusubiri na wasiwatese mitume ili wasijikute wanapambana dhidi ya Mungu, na kwa hakika mitume wa Yesu wa Nazareth waliamini mchungaji, ambapo wao walitakiwa wapotee kwa mujibu wa wahahudi. Meneno ya utabiri wa Gamalieli, anasema Baba Mtakatifu yanatoa vigezo ambavyo vinatambua Injili kwa sababu vinaaliaka kutambua mtu kutokana na matunda yake na kupata matokeo yaliyo tarajiwa.  Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha kwa kuwaalika wote ili kuomba Roho Mtakatifu zawadi ya kufanya mang’amuzi. "Tuombe Bwana ili kutambua kutazama umoja wa historia ya wokovu kwa njia ya ishara za hatua za Mungu katika nyakati zetu hizi; katika uso wa aliye kandoni mwetu na ili tuweza kujifunza  kuwa wakati na nyuso  za wanadamu ndiyo wajumbe wa Mungu aliye hai.

 

18 September 2019, 13:00