Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekazia juu ya uvuguvugu wa kiroho na ili usiegeuze maisha kama ya makuburini mahali pasipo maisha Baba Mtakatifu Francisko amekazia juu ya uvuguvugu wa kiroho na ili usiegeuze maisha kama ya makuburini mahali pasipo maisha  (ANSA)

Baba Mtakatifu Francisko:Uvuguvugu wa kiroho hubadili maisha yetu kuwa makaburi!

Tuombe Bwana neema ya kutokuwa nusu wakristo kwa kufurahia kukaa na amani ya uongo ndani ya mioyo yetu ambayo haizai matunda.Bwana anataka uongofu wa haraka na siyo kusubirisha kesho.Ndiyo sala ya Baba Mtakatifu Francisko,wakati wa mahubiri kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican tarehe 26 Septemba 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi 26 Septemba 2019 katika mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican amejikita kutafakari juu ya Somo la kwanza linalopendekezwa na Liturujia ya siku, yaani  kutoka katika Kitabu cha nabii  Hagai. Ni kitabu kigumu anasema ambacho katika hali ngumu anayopitia nabii huyo, kupitia kwake, Bwana anawashauri watu wake watafakari namna yao ya kuishi na kujibidisha ili wabadilike na kuweza kujenga Nyumba ya Mungu.

Akiendelea na tafakari hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa nabii Hagai alikuwa akitafuta namna ya kuwafanya watu washituke mioyoni mwao na waondoe uvivu waliokuwa nao wa kuishi namna hiyo kwa kushinda bila kufanya kazi. Hekalu la Mungu lilikuwa limeharibiwa lote na watu walikuwa wamekaa miaka mingi hivyo hadi Bwana alipomtuma mteule ili waweze kujenga hekalu kwa upya. Lakini mioyo yao ilikuwa imekata tamaa, hawakuwa na utashi wa kujikita kazini. Walikuwa wakisema hapana na hatuwezi kwenda mbele labda tuna danganywa na  bora kusithubutu, tubaki namna hiyo.

Watu hao walikuwa hawana utashi wa kuamka tena na kuanza upya, hawakutaka kuisaidiwa na Bwana ambaye alitaka waamke na huku wakitafuta hata sababu kwamba “huo sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujengwa nyumba ya Bwana”. Hili ndilo lilikuwa janga la watu hawa Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza na kuongeza, “hata sisi pia tunapokuwa  na roho ya ugumu, tunaposhikwa na uvuguvugu wa maisha, tunasema,  “ndiyo Bwana”, lakini “Bwana  pole pole” na wakati huo huo  kujiachia hivyo, ukidai  kesho nitafanya kazi na kumbe  kesho hiyo inaita kesho kutwa, inaita mtondo na mtondogoo…kwa namna hiyo yanageukua kuwa  maisha yanayo subiri bila  kutoa maamuzi wa uongofu wa moyo na kubadili maisha.

Uvuguvugu wa kiroho ni amani ya makuburini: Baba Mtakatifu Francisko  akiendelea juu ya suala la uvuguvugu anasema ni moto kidogo kidogo ambao mara nyingi unajificha nyuma ya kutokuwa na uhakika na kusubirisha hadi siku nyingine. Kwa njia hiyo watu wengi wanapoteza bure maisha yao na kuishia kuwa kama  kitambaa kichakavu kwa sababu hawakufanya lolote, bali kubaki kuhifadhi uongo wa  amani na utulivu ndani yao. Lakini hiyo “ni amani ya makaburini”. Tunaposhikwa na moto mdogo mdogo kama huo yaani kuwa na  tabia  ya uvuguvugu wa kiroho, tunageuza maisha yetu kuwa kama makuburini, kwa maana hakuna maisha. Kilichopo ni kufungwa tu na matatizo hayaingii kama ilivyokuwa  kwa watu hao wakidai kwamba, ndiyo tuishi katika magofu, lakini bora tusithubutu. Ni bora kuishi hivyo kwa maana tumezoe!

Bwana anaomba leo hii uongofu wetu:Kwa kuhitimisha hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko ameonya kwamba mambo hayo yanatokea kwetu sisi kutokana na mambo madogo madogo ambayo hayaendi vizuri na wakati Bwana anataka tuyabadili. Yeye anatuomba uongofu na sisi tunatoa jibu la kesho. Kutokana na jibu hilo ndiyo wito wa mwaliko wa sala, ili tuombe Bwana  atupatie neema ya kutodumbukia katika roho ya nusu ukristo au kama wasemavyo wazee “wakristo maji juu ya rose, yaani bila dutu, na kuwa wakristo wema, lakini wanaofanya kazi sana, kwamba “mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo. Haya ni maisha yaliyotoa ahadi nyingi na mwisho wake hawakufanya lolote. Bwana atusaidie kuamsha roho zilizo na joto kidogo ili kuweza kupambana dhidi ya ubaridi huo wa maisha ya kiroho.

26 September 2019, 13:23