Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito wake mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa ajili ya kuzima moto kwa haraka unaoendelea kurarua msitu wa Amazonia,ujulikanao kama pafu la sayari hii! Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito wake mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa ajili ya kuzima moto kwa haraka unaoendelea kurarua msitu wa Amazonia,ujulikanao kama pafu la sayari hii! 

Wito wa Papa kwa ajili ya Amazonia kwa ajili ya kuzima moto kwa haraka!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito wa nguvu kwa ajili ya kuweza kuzima katika msitu wa Amazonia.Moshi umetanda zaidi ya kilomita za mraba 2,250 hadi kuonesha wingu jeusi katika mji wa Mtakatifu Paulo nchini Brazil.Na vuguvugu la kimataifa linazidi kuongezeka katika meza ya nchi saba tajiri duniani(G7)!

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 25 Agosti 2019, katika dirisha,  mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ameomba kwa nguvu zote jitihada kwa wote kwa ajili ya kusimamisha moto unaoendelea kurarua kwa miezi hii msitu wa Amazonia na ambao kwa siku hizi umezidi kuongezeka kipimo chake hadi kufikia kuonekana kwa kilometa 2,250 za mraba na kwa wakati huo huo kufanya wingu kubwa la moshi mzito angani  katika mji wa Mtakatifu Paulo nchini Brazil. Baba Mtakatifu Francisko amesema,"tuna wasiwasi kufuatia na moto ambao unazidi kuongezeka huko Amazonia.Tuombe ili jitihada za wote, ziweze kweli kuzima moto kwa haraka. Mapafu hayo ya msitu ni maisha kwa ajili ya sayari yetu”.

Dharura juu ya meza ya G7

Ni Jumamosi tarehe  24 Agosti 2019  tu walipoweza kuweka mpango wa dharura wa kuzima moto na kupelekwa kwa askari zaidi ya elfu 44 wanaoungwa mkono na ndege za anga,  au baharini na ardhi. Sehemu za misitu zilizoathirika zaidi ziko katika sehemu ya  Randonia, Bolivia, Brazil, lakini sasa moto pia umefika nchini Paraguay. Katika kipeo cha mazingira ambacho kitakuwa na athari kubwa juu ya mfumo mzima wa mazingira duniani, ndiyo mtazamo mkuu wa Baba Mtakatifu Francisko  na ambao amewashauri sana wakuu wa nchi na serikali na kutoa njia ya uhamasishaji wa kimataifa wa raia, ambao pia wamweza kushuka barabarani  wakiandamana dhidi ya rais wa Brazil Bwana Bolsonaro ambaye alishtumu nchi jirani "kutokujali", hadi kufika huko Biarritz, nchini Ufaransa kwenye meza ya G7 ambayo pia inaweza kuleta vikwazo vya kimataifa dhidi ya nchi ya Brazil.

Tangu Januari maeneo 72,000 yemechomwa 

Kwa mujibu wa Rais Bolsonaro moto ulioweza  kuchoma kwa wastani katika miaka 15 iliyopita, lakini kulingana na takwimu kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Nafasi ya Brazil, kuanzia Januari hadi leo, katika msitu wa mvua kumekuwa na maeneo ya moto  72,000 kwa ongezeko la asilimia 84% ikilinganishwa na zile ya 2018. Na sababu kubwa msingi au asili ya moto huo utafikiri daima unatokana na ukataji hovyo wa miti kila wakati na ambapo utumia moto kawaida kwa kutaka kupata shamba kubwa la haraka iwezekanavyo.

Wito wa maaskofu wa Amerika Kusini

Katika hali halisi hii ya dharura, imewasukuma hata Baraza la Maaskofu wa Brazili kushuka katika viwanja kwa makusudi. Ni dharura ya kwamba serikali za nchi za Amazoni hasa Brazil ziweze kuchukua hatua ya dhati ili kuweza kuokoa kanda kutokana na msimamo wa usawa wa ekolojia ya syari hii. Hata hivyo "sio wakati tena wa kutokuwa na hisia au kuwa na hukumu na maneno". Wanatoa sauti hata maaskofu wa Mexico na wale wa Paraguay, mahali ambapo hadi sasa Ekari 40,000 zimekwisha teketea kwa moto na vichaka na malisho katika Kanda ya Chaco. Hatari kwa pafu ya ulimwengu, ambayo peke yake hutoa oksijeni asilimia 20 katika sayari na asilimia 10% ya viumbe hai, haitazami tu mimea na wanyama, lakini pia watu na makabila ya asili, ambao wamelazimika waliolazimika kuacha hata msitu wao na wakati huo hata suala la kuongezeka kwa joto duniani.

26 August 2019, 09:40