Tafuta

Vatican News
Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Agosti 2019: Mwendelezo wa ufafanuzi wa Kitabu cha Matendo ya Mitume, Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Agosti 2019: Mwendelezo wa ufafanuzi wa Kitabu cha Matendo ya Mitume,   (Vatican Media)

Papa:usiogope wale ambao wanatuamuru kukaa kimya au kutusengenya

Wagonjwa ndiyo wenye upendeleo kwa Kanisa,katika moyo wa makuhani na kwa waamini wote.Siyowa kutengwa na kinyume chake,wao wanapaswa kutibiwa na kutunzwa.Hili ndilo jambo la kujali kikristo.Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyokazia wakati wa Katekesi yake tarehe 28 Agosti 2019 katika mwendelezo wa tafakari ya kitabu cha Matendo ya mitume.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 28 Agosti 2019 wakati wa Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mahujaji na waamini waliofika kushiriki mafundisho yake, katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, ameendelea kufafanua maandiko ya Mtakatifu Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume (Mdo 5,12.15-16). Baba Mtakatifu Francisko amesema, Jumuiya ya Kanisa inayoelezwa katika kitabu cha matendo ya mitume inaishi na utajiri mkubwa ambao Bwana amewawekea. Bwana ni mkarimu! Wanafanya uzoefu wa kuona ongezeko la  idadi kubwa na chachu kuu, japokuwa kuna uwepo wa mashambulizi kutoka nje. Kwa kuonesha uhai huo, Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume anaelekeza hata maeneno muhimu, kwa mfano katika ukumbi wa Solomoni (Mfo 5,12) ilikuwa ni mahali pa kukutana kwa waamini. Ukumbi (stoa) uliokuwa, ulikuwa pia ni mahali pa kimbilio, lakini hata mahalia pa mkutano na ushuhuda, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Luka kwa hakika anasisitiza juu ya ishara na juu ya miujiza ambayo ilikuwa inasindikiza neno la Mitume na juu ya utunzaji maalum wa wagonjwa ambapo mitume walikuwa wanajikita nao.

Jina la Yesu lina nguvu

Katika sura ya 5 ya Matendo ya Mitume, Kanisa linalozaliwa linajionesha kama hospitali katika  kambi, ambalo linapokea watu wadhaifu zaidi yaani wagonjwa. Mateso yao yanawavuta Mitume ambao hawana kitu, wala fedha au dhahabu ( Mdo 3,6) kama Petro alivyo mwambiakiwete,lakini jina laYesu lina nguvu. Katika macho yao kama yalivyo macho ya wakristo wa kila nyakati, wagonjwa ndiyo wenye kuwa na nafasi mwafaka ya kutangaziwa habari ya Ufalme, ni ndugu ambao Kristo yumo ndani mwao kwa namna ya pekee ili kuacha watafutwe na uwapata wote. ( taz Mt 25,36.40) Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza  tena na kusema: Wagonjwa ndiyo njia mwafaka kwa ajili ya Kanisa, kwa ajili ya moyo wa padre na kwa ajili ya waamini wote. Siyo wa kubaguliwa, kinyume chake ni wa kutunzwa na kutibiwa! Na hili ndilo jambo la kujali kikristo,Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza!

Petro ndiye kiongozi kutokana na kupewa madaraka na Mfufuka

Kati ya mtume anajitokeza Petro ambaye ndiye kiongozi wa kikundi cha kitume kwa sababu ya ukuu (Mt 16,18) na utume alipewa na Mfufuka (Yh21,15-17). Ni yeye anayetoa uamuzi wa kutangaza kerygma  katika siku ya Pentekoste (Mdo 2,14-41) na hata katika mtaguso wa Yesualemu kwa namna ya kuelekeza na kuendesha Kanisa ( Mdo 15 na Gal 2,1-10).  Petro alikaribia vitanda na kupitia kati ya wagonjwa  kama alivyokuwa anafanya Yesu kwa kuchukua udhaifu na kubeba magonjwa (Mt 8,17; Is 53,4). Na pia  Petro mvuvi wa Galilaya, anapita tu, lakini anaacha mwingine ajioneshe, na ambaye  kwamba awe Kristo aliye hai na anayetenda! Shuhuda kwa dhati ni yule anayeonesha Kristo, iwe katika maneno au katika uwepo wa kimwili na ambaye anaruhusu kuwa na uhusiano kwa  muda mrefu  na lile Neno lililofanyika mwili katika historia, Baba Mtakatifu Francisko amefafanua!

Petro ni nani? Ni yule anayetimiza matendo ya Mwalimu

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ufafanuzi wake amesema, Petro ni yule anayetumiza matendo ya Mwalimu (Yh14,12):  kwa kumtazama yeye kwa imani, anamtazama Kristo mwenyewe. Aliyejazwa na Roho ya Bwana, Petro anatembea bila kufanya lolote lile na wakati, kivuli chake kinageuka kuwa kitulizo, chenye kuponya, kinatangaza afya, kinasambaza huruma ya Mfufuka ambaye anainamia wagonjwa na kuwarudishia maisha, wokovu na hadhi. Kwa namna hiyo Mungu anajionesha ukaribu wake na kuyafanya majeraha ya watoto wake kuwa “sehemu ya taalimungu ya huruma yake.” (taz. tafakari ya Papa katika Kanisa la Mtakatifu Marta 14.12.2017).

Katika majeraha ya wagonjwa na magonjwa kuna uwepo wa Yesu

Baba Mtakatifu Francisko kwa kufafanua zaidi amesema katika majeraha ya wagonjwa, ma katika wagonjwa unaozuia kwenda mbele katika maisha, daima kuna uwepo wa Yesu, na jeraha la Yesu. Yupo Yesu ambaye anaita kila mmoja wetu kuwatunza na kuwasaidia wagonjwa ili wapone. Lakini matendo ya uponyaji wa Petro inasababisha chuki na wivu wa masadukayo ambo waliwafunga mitume baada ya kuwa na mshituko wa maajabu ya kukombolewa kwa watu na wanawakataza wasifundishe!. Baba Mtakatifu Francisko anasema, watu hawa walikuwa wanaona miujiza ya kweli iliyofanywa na mitume bila kwamba ni  mazingaombwa, lakini ni kwa kutimia jina la Yesu! Japokuwa kwa bahati mbaya hawa hawakutaka kukubali na wanaamua kuwafunga jela mitume na kuwapiga viboko. Lakini Mitume hawa walikombolewa kimiujiza, japokuwa mioyo ya  masadukayo ilikuwa migumu sana na hawakutaka kuamini kile ambacho walikuwa wanaona.

Petro anatoa jibu kama ufunguo wa maisha kikristo!

Baba Mtakatifu Francisko amethibtisha ya kwamba kutokana na hali ya ugumu huo wa masadukayo ndipo Petro sasa anawajibu kwa kuwa anao ufunguo wa maisha kikristo. Jibu lake ni kwamba: “Ni lazima tumtii Mungu na siyo binadamu  (Mdo 5,29), na hii ni kutokana na upande wa masadukayo waliokuwa wanasema kuwa, “ nyinyi msiende  mbele na mambo hayao  na walai msiponyeshe. Lakini Petro anasema: “Mimi nina mtii  Mungu kwanza kabla ya binadamu”. Hili ndilo  jibu kubwa la kikristo, ameongeza kusema Baba Mtakatifu Francisko kwa kukazia. Na zaidi amasema hii ina maana ya kusikiliza Mungu bila kubakiza, bila kuchelewa, bila kuhesabu; kwenda kwake ili kuweza kuwa na uwezo na agano naye na kwa yule ambaye tunakutana naye katika njia zetu. Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha katekesi yake akiwasihi wote kuomba  Roho Mtakatifu nguvu ya kutokuwa na hofu yoyote mbele ya yule ambaye anatuamuru kunyamaza na anaye tusengenya hadi kufikia kujaribu maisha yetu! Tumwombe atuongezee nguvu za kina ili tuweze kuwa na uhakika wa uwepo wake wa upendo na faraja ya Bwana karibu nasi.

28 August 2019, 13:20