Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kuhusu nia za maombi ya sala kwa mwezi Septemba 2019 ambapo anawakumbusha kusali watu wote kwa ajili ulinzi wa bahari na visiwa Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kuhusu nia za maombi ya sala kwa mwezi Septemba 2019 ambapo anawakumbusha kusali watu wote kwa ajili ulinzi wa bahari na visiwa 

Papa Francisko:Uumbaji ni mpango wa upendo wa Mungu

Katika nia za maombi kwa mwezi Septemba 2019,Baba Mtakatifu Francisko anaelekeza sala hizo katika ulinzi wa bahari na visiwa kwa ujumla ambapo leo hii anathibitisha kuwa vinatishiwa kwa sababu tofauti.Anawaomba viongozi wa kisiasa,wanasayansi na wanauchumi kufanya kazi pamoja kwa lengo la ulinzi wa vyanzo vya maji kwa ujmla!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kama ilivyo kila mwezi kuwa na nia za maombi ya Baba Mtakatifu Francisko, kwa mwezi Septemba 2019, nia zake ni kwa ajili ya wanasiasa, wanasayansi na wanauchumi ili wafanye kazi pamoja kwa ajili ya kulinda bahari na visiwa. Baba Mtakatifu anatoa ushauri kwa njia ya video, huku akikumbusha kwamba uumbaji ni mpango wa upendo wa Mungu kwa binadamu na ambapo leo hii bahari na visiwa, ambavyo vinahifadhi sehemu kubwa ya maji mengi ya sayari na hata aina mbambali za viumbe hai, zinatishiwa kwa sababu tofauti”. Na kwa maana hiyo anaongeza kusema kuwa: “ushirikiano wetu na nyumba yetu  ya pamoja unazaliwa katika imani yetu”.

Nia za Papa kwa ajili ya mazingira ni muhimu

Padre Frédéric Fornos, mkurugenzi wa Utume wa Sala kimataifa katika mtandao kwa ajili ya sala ya Papa duniani na ambao unaunganisha vyama vya kitume kwa ekaristi vya vijana anakumbusha kwamba, mwaka jana katika fursa ya Siku ya Kuombea Mazingira, Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza juu ya masuala ya maji kwa namna ya pekee kutazama bahari na visiwa, mahali ambapo ulinzi wake unawakilisha leo uwajibakaji wa lazima. “Hatuwezi kuruhusu kuwa bahari na visiwa vinajazwa na plasitiki nyingi kupindukia” anasema Baba Mtakatifu. Vile vile anasema kuwa  katika dharura hiyo, sisi sote tunaalikwakwa na jitihada katika akili na  kusali kama vile kila kitu kinategemea na Mungu na kufanya kazi kama vile yote yanategemeana na sisi”

Pafu la blu duniani : Bahari inasongwa na plastiki

Kila mwaka zaidi ya tani miliono 8 zinatupwa baharini, na kusababisha kati ya mamboi mengine vifo karibia 100,000 vya aina za viumbe. Uchafuzi wa baharini utokanao na plastiki ni tatizo la dunia na mipaka ambayo inahitaji uwajibikaji wa pamoja na mkakati wa kawaida wa pamoja. Malengo ya Maendeleo Endelevu, ya Umoja wa Mataifa imejiwekea malengo kadhaa ya kuweza kukabiliana ili kuweza kuthibiti hali hii kwa utambuzi kuwa bahari ambayo ni pafu la blu, hutoa rasilimali asili msingi kama chakula, dawa, mafuta ya mimea na bidhaa zingine; Huchangia kuondoa taka na uchafuzi wa mazingira; na mifumo ya ikolojia katika pwani hufanya kupunguza uharibifu unaosababishwa na dhoruba kali.

31 August 2019, 16:02