Tafuta

Vatican News
Hii ni picha ya  Papa Francisko na Kardinali Achille Silvestrini aliyeaga dunia tarehe 29 Agosti 2019 akiwa na umri wa miaka 95 Hii ni picha ya Papa Francisko na Kardinali Achille Silvestrini aliyeaga dunia tarehe 29 Agosti 2019 akiwa na umri wa miaka 95 

Papa Francisko:Salam za rambirambi na sala kwa ajili ya roho ya Kard.Silvestrini

Baba Mtakatifu Francisko ametuma telegram yake kwa dada wawili,Maria Luisa na Angela kufuatia na kifo cha kaka yao Kardinali Achille Silvestrini,aliyekuwa ni Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.Kifo chake kimetokea tarehe 29 Agosti 2019 katika hospitali ya Gemelli Roma akiwa na umri wa miaka 95.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kufuatia na kifo cha Kardinali Achille Silvestrini aliyekuwa ni Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashari kilichotokea tarehe 29 Agosti 209, Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambirambi kwa njia ya telegram  kwa  dada zake Maria Luisa na Angela Silvestrini, akionesha masikitiko yake ya  kuondokewa na ndugu yao. Anatoa salam za rambirambi kwa familia nzima ikiwa ni pamoja na wale wote  wote waliomjua na kama ilivyo haya jumuiya nzima ya Jimbo Faenza huko Modigliana alipozaliwa Kardinali Silvestrini na kwamba, wanamkubuka hata kati ya watoto wake kiroho. Aidha Baba Mtakatifu Francisko anaonesha kumbukumbu hasa ya ushirikiano wake kwa miaka mingi katika mji wa Vatican katika huduma zaidi ya saba za kipapa, huku akitaja baadhi kama vile ya ukatibu wa Vatican, Rais wa Mahakama Kuu ya Kitume Vatican na rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.

Marehemu Kardinali Silvestrini anaacha kumbukumbu hai

Kardinali Silvestrini anasema Baba Mtakatifu Francisko, anaacha kumbukumbu ya maisha yake aliyojikita nayo kwa kutimiza wito wake kama padre mwenye umakini kwa mahitaji ya lazima ya wengine; mwenye uwezo wa kidiplomasia, mpole, mchungaji mwaminifu wa Injili na Kanisa anathibitisha. Na kwa maana hiyo anasali kwa ajili ya roho ya marehemu kwa Bwana ili ampokee katika furaha na amani ya milele, huku akiwatumia Baraka ya kitume ili iwatulize wote  wanaomboleza kufuatia kifo chake.

Kuhusiana na kifo chake

Tarehe 29 Agosti  2019 ameaga dunia Kardinali Achille Silvestrini, akiwa na  umri wa miaka  95. Kufuatia na kifo cha kardinali huyo kwa sasa baraza la makardinali wanabaki 215 kwa jumla na kati yao 118 ni wenye kuchaguliwa na 97 hawana kura ya kuchaguliwa. Kardinali Achille Silvestrini alikuwa ni mtu makini na mwenye macho ya mtazamo kwa upnade wa vijana. Amejikita kwa miaka mingi katika shughuli za kidiplomasia za Vatican. Na alikuwa anashirikiana kwa karibu na wahudumu wa  katibu wa Vatican Domenico Tardini na Amleto Giovanni Cicognani wa wakati ule. Aidha kati ya mambo mengi aliyo yafanya amesafiri sana akiwa  wakati huo na Askofu Agostino Casaroli katika kipindi cha Ostpolitik na kuongoza michakato mbalimbali na viongozi wa Italia kwa ajili ya kutazama kwa upya mikataba ya Laterano

Padre kijana kutoka mkoa wa emilia Romagna

Alizaliwa huko Brisighella, katika jimbo la Faenza kunako tarehe 25 Oktoba 1923 na kujinga na semina ya jimbo akiwa na umri wa miaka 19 . Alipewa daraja la upadre kunako tarehe 13 Julai 1946 na Askofu Giuseppe Battaglia. Alijiunga na Chuo Kikuu katika cha Bologna katika kitivo cha falsafa na kupata shahada katika masomo ya lugha maalum kwa utetesi wa Thesis yake kuhusu "Misingi ya hati muhimu za Kanisa Takatifu".  Alitumwa Roma kunako mwaka 1948 kujiunga na Seminari ya Kipapa katika masomo ya Sheria katika  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Apolinari, pia kuendelea na Chuo Kikuu la Laterano ambapo alipata shahada ya Matumizi ya sheria.

Huduma za kidiplomasia kwa kusikiliza na mazungumzo na umakini wa maisha ya Kanisa

Kunako mwaka 1952 alijiunga na Taasisi ya Kipapa ya Kanisa ,na baadaye akaingia desemba 1953 katika huduma ya kidiplomasia kwenye kitengo cha shughuli za Kanisa maalum za Vatican. Ameweza kuhudumia huko Vietnam,  China, Indonesia na kwa ujumla Bara la Asia kusini mashariki na tangu 1958-1969 alikuwa kati ya wahudumu wa Katibu wa Vaticani akiwa na Domenico Tardini na Amleto Giovanni Cicognani. Kunako mwaka 1973 alichaguliwa kuwa Katibu msaidizi wa Baraza la shughuli za umma za Kanisa mahali ambapo baadaye akapewa ukatibu huo kunako tarehe 4 Mei 1975. Alipewa ngazi ya uaskofu mkuu wa Novalcina kunako tarehe 4 Mei 1979 katika mikono ya Mtakatifu Yohane Paulo II .

Shughuli hii ilimpelekea kuongoza kunako mwaka 1979 uwakilishi wa Vatican katika kutazama kwa  upya juu ya  Mikataba ya Lateranno pamoja na viongozi wa italia hadi kufikia  sahini ya Makataba kunako tarehe 18 Februari 1984 Nicaragua na  El Salvador (1983); Poland (1983); Stokholm na  kama kiongozi mwakilishi wa Vatican katika toleo la ufunguzi wa Baraza la kusitisha silaha Ulaya (1984); aidha huko Helsinki kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 10 ya kutiwa sahini kwa Hati ya mwisho ya Baraza la usalama na ushirikiano Ulaya; bado tena kwenda Malta kwa ajili ya kufafanua makubaliano juu ya shule ya Kanisa  (1985);  Lebanon na  Siria (1986); Polonia (1987). Ni idadi kubwa ya utume wa kidiplomasia alio ufanya kwa kipindi cha miaka yote, kwa mfano kuwa hata kuwa mwakilishi tena wa Vatican huko Madri katika Mkutano kwa ajili ya usalama na ushirikiano barani Ulaya (1980-83); Buonos Aires kwa ajili ya kipeo cha Malvine-Falklands (1982);

Mtazamo wa umakini juu ya dunia ya vijana

Ni mtakatiu Yohane Paulo II aliyemteua tarehe 28 Juni 1988 kuwa kardinali na abaadaye kumtangaza kuwa Rais wa Mahakama  kuu ya kipapa. Tangu tarehe 24 Mei 1991 hadi  25 Novemba  2000 alishika nafasi ya kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki. Kati ya huduma zake amejikita kwa nguvu zote katika matendo katikati ya vijana wa “Villa Nazareth”, ambayo ni taasisi iliyoundwa kunako mwaka 1945 na Kardinali Tardini. Tangu 1969 aliongoza jumuiya iliyoundwa kutokana na wanafunzi waliomaliza chuo kikuu na kupata shahada mbalimbali, wataalam na marafiki wa Villa Nazareth. Kutokana na hilo kunako mwaka 1986 kikazaliwa chama cha Jumuiya ya Domenico Tardini”(ambaye alikuwa ni Kardinali mwanzilishi), na ambacho kilikabidhiwa Chama cha Familia Takatifu ya Nazareth kuwa wawajibikaji wa shughuli za mafunzo na uendeshaji wake. Vyama vyote viwili vilikuwa chini ya uongozi wa Kardinali Silvestrini kama rais wake.

 

 

30 August 2019, 10:47