Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anaalika Wametodisti na Wavaldese na wote kuendelea na jitihada katika safari ya kujuana kwa pamoja,kuelewana na kushirikiana kwa ajili ya kushuhudia Yesu na Injili ya Upendo. Papa Francisko anaalika Wametodisti na Wavaldese na wote kuendelea na jitihada katika safari ya kujuana kwa pamoja,kuelewana na kushirikiana kwa ajili ya kushuhudia Yesu na Injili ya Upendo. 

Papa anaomba kuwa na msimamo wa roho ya kiekumene na umoja wa Makanisa!

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa Sinodi ya Wametodisti na Wavaldesi,iliofunguliwa Jumapili tarehe 25-30 Agosti huko Torino Italia.Baba Mtakatifu anaungana katika sala kuweza kuwa na msimamo wa roho ya kiekumene kati ya wakristo katika kukua kwa umoja kati ya makanisa.Aidha anawakumbusha kuwa na mtazamo wa masikini na walio wadhaifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 25 Agosti 2019 Baba Mtakatifu Francisko ametuma barua ya matashi mema ya Sinodi ya makanisa ya Wametodisti na Wavaldesi katika fursa ya Sinodi yao ya kila mwaka ambayo imefunguliwa Jumapili 25 - 30 Agosti 2019 huko Torre Pellice (Torino),Italia. Katika ujumbe wake Baba Mtakatifu amesema: “Ndugu kaka na dada, Sinodi ya Muungano wa Makanisa ya Kimetodisti na Valdesi ni fursa ya kweli kwa ajili ya kuwapa salam na ambazo ni kielelezo cha ukaribu wangu kindugu na kwa Kanisa zima katoliki. Ninasali kwa ajili yenu ili kwa siku hizi za mkutano katika sala na tafakari zenu mnaweza kufanya uzoefu hai katika Roho Mtakatifu ambaye anaendesha na kutoa nguvu ya ushuhuda kikristo".

Baba Mtakatifu Francisko anaungana nao katika sala

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko anaonesha kuungana na sala zao, hata kuomba kwa Bwana juu ya msimamo wa  roho ya kiekumene kati ya wakristo na kama pia kukua kwa umoja kati ya makanisa yetu. Aidha amesema kwamba,“tunaalikwa kuendelea katika jitihada zetu katika safari ya kujuana pamoja, kuelewana na kushirikiana kwa ajili ya kushuhudia Yesu na Injili ya Upendo.

Kama wafuasi wa Kristo lazima kutoa jibu la pamoja dhidi ya mateso

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake amesema, “Na kama wafuasi wa Kristo, tunaweza kutoa jibu la pamoja dhidi ya mateso ambayo yanawasibu watu wengi hasa walio masikini zaidi na wadhaifu na huku tukihamasisha haki na amani. Na hatimaye anawatakia Sinodi njema na huku akiwapa baraka ya Bwana na kuwaomba wasali kwa ajili yake.

Sinodi itahitimishwa kwa uchaguzi wa mchungaji mkuu

Kuhusiana na sinodi hiyo ni kiungo cha uamuzi wa Umoja wa Makanisa ya Kimetodisti na Wavaldese ambao watahitimisha mkutano huo kwa kufanya uchuguzi wa viongozi wao wa Makanisa hayo.

25 August 2019, 15:38