Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 30 Agosti 2019 ametuma ujumbe wake kwa watu wa Mungu nchini Msumbiji, katika fursa ya maadalizi ya hija ya kitume kuanzia tarehe 4-10 Septemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko tarehe 30 Agosti 2019 ametuma ujumbe wake kwa watu wa Mungu nchini Msumbiji, katika fursa ya maadalizi ya hija ya kitume kuanzia tarehe 4-10 Septemba 2019 

Ziara ya Papa Francisko nchini Msumbiji:Tusali ili kuimarisha amani ya nchi

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa wanafamilia ya Mungu nchini Msumbiji kwa wakati huu anapojiandaa kufanya hija ya kitume nchini mwao.Baba Mtakatifu anasema hata kama hawezi kwenda mbali zaidi ya mji mkuu anawahakikishia watu wote sala zake ili ziwafikie na anawakumbatia wote kwa moyo,kwa namna ya pekee wale wote wanaoteseka!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuanzia tarehe 4 hadi 10 Septemba 2019, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kufanya hija ya kitume nchini Msumbiji pia kuelekea katika visiwa vingine vya Madgascar na Mauritius. Akiwa huko ataweza kukutana na watu wa Mungu na kwa namna hiyo, Baba Mtakatifu tarehe 30 Agosti 2019 ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa wanafamilia ya Mungu nchini Msumbiji, kwa wakati huu anapojiandaa kufanya hija hiyo ya kitume nchini mwao. Hawali ya yote anasema, hata kama hawezi kwenda mbali zaidi ya mji mkuu, moyo wake unawafikia na kuwakumbatia wote, kwa namna ya pekee wale wote wanaoshi katika matatizo! Vile vile Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwahakikishia kwa kusema:“ninyi nyote mpo katika sala zangu. Na pia nina furaha ya kuwatembelea na kukutana nanyi!

Shukrani kwa rais na maaskofu kwa mwaliko wao

Aidha Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video, anapenda kutoa shukrani kama yeye alivyozipokea, kufuatia na mwaliko wa Rais na ndugu zake maaskofu ili kuwatembelea, kwa maana hiyo, anawaalika watu wa Mungu wote kuanzia sasa waungane naye katika sala ili Mungu Baba wa wote aweze kuimarisha mapatano pia kuimarisha udugu wa Msumbiji na kwa Afrika nzima, kuwa na tumaini moja kwa ajili ya nguvu ya amani na ya kudumu.

Kushirikisha furaha moja kwa moja nao

Baba Mtakatifu Francisko vile vile ameonesha katika ujumbe wake atakavyo kuwa na furaha ya kushirikishana moja kwa moja nao, ambapo anathibitisha kuwa ni uhakika na hata kuona ni jinsi gani mbegu inakua, ile iliyopandwa na mtangulizi wake Mtakatifu Yohane Paulo II. Ziara hiyo aidha anasema inamruhusu kukutana na jumuiya katoliki na kuwatia moyo katika ushuhuda wa Injili, ambayo inafundisha hadhi ya kila mwanaume na mwanamke na anaomba kufunguliwa kwa mioyo yao kwa ajili ya wengine, hasa walio masikini na wenye kuhitaji.

Utambuzi wa maandalizi ya nguvu ya kumpokea

Baba Mtakatifu  katika ujumbe wake kwa njia ya video anahitimisha kwa wanafamilia ya Mungu akisema kwamba, anatambua kuhusu watu wengi sasa hivi wanavyofanya kazi kwa ajili ya kuandaa ziara yake, ikiwemo hata sadaka kwa ajili ya sala zao, anawashukuru kwa moyo wote. Anawaombea baraka kutoka kwa Mungu na kwa ajili ya nchi yao na ulinzi wa Mama Yetu Bikira Maria!

30 August 2019, 09:39