Baba Mtakatifu Francisko amemzawadia Patriaki Bartolomeo wa kwanza masalia ya Mtakatifu Petro. Baba Mtakatifu Francisko amemzawadia Patriaki Bartolomeo wa kwanza masalia ya Mtakatifu Petro. 

Masalia ya Mtakatifu Petro, zawadi kwa Patriaki Bartolomeo wa kwanza!

Ilikuwa ni tarehe 26 Juni 1968 siku mbili tu kabla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Mtakatifu Paulo VI alipotangaza matokeo ya utafiti wa mambo ya kale kuhusu masalia ya Mtakatifu Petro. Utafiti ulianzishwa na Papa Pio XII kunako mwaka 1939 na kukamilika mwaka 1950. Mtakatifu Paulo VI akatangaza kwamba, watafiti waliweza kugundua kaburi la Mtakatifu Petro.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ujumbe wa Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Costantinopol katika maadhimisho ya Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo Mitume na miamba wa imani tarehe 29 Juni 2019 ni alama makini katika mchakato mzima wa majadiliano na hija ya kiekumene; umoja na udugu, kielelezo cha neema ya Mungu katika Makanisa haya mawili! Baba Mtakatifu Francisko katika Sherehe hizi amemzawadia Patriaki Bartolomeo wa kwanza masalia ya Mtakatifu Petro, zawadi aliyopewa Mtakatifu Paulo VI baada ya utafiti wa kina uliofanywa na mtaalam wa mambo ya kale Margherita Guarducci.

Ilikuwa ni tarehe 26 Juni 1968 siku mbili tu kabla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Mtakatifu Paulo VI alipotangaza matokeo ya utafiti wa mambo ya kale kuhusu masalia ya Mtakatifu Petro. Utafiti huu ni matunda ya kazi iliyokuwa imeanzishwa na  Papa Pio XII kunako mwaka 1939, utafiti huu ulidumu kwa takribani miaka 10 na kunako mwaka 1950 Mtakatifu Paulo VI akatangaza kwamba, watafiti waliweza kugundua kaburi la Mtakatifu Petro lililoko chini ya Altare ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, mahali ambapo masalia ya Petro, mwamba wa Kanisa yamehifadhiwa.

Watafiti hao waligundua maandishi ya lugha ya Kigiriki yaliyoonesha kwamba, “Petros eni”, yaani hapa ni mahali alipozikwa Mtakatifu Petro. Katika maadhimisho ya kufunga Mwaka wa Imani, tarehe 24 Novemba 2013, Baba Mtakatifu aliweka masalia haya kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko na Patriaki Bartolomeo wa kwanza wanaendelea kuimarisha udugu wao katika imani kwa Kristo Yesu kama njia ya kuimarisha na kudumisha majadiliano ya kiekumene, changamoto na mwaliko uliovaliwa njuga na Mtakatifu Paulo VI katika maisha na utume wake.

Papa: Masalia

 

02 July 2019, 14:39