Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anasema,tunapojikita katika usikivu kumsikiliza kiukweli Bwana mawingu yanapotea,wasiwasi unaisha na kwa hakika kuacha nafasi, pia hofu zinaisha na kuwa na utulivu Papa Francisko anasema,tunapojikita katika usikivu kumsikiliza kiukweli Bwana mawingu yanapotea,wasiwasi unaisha na kwa hakika kuacha nafasi, pia hofu zinaisha na kuwa na utulivu  

Papa Francisko:Bwana anapokuja anapanga kila kitu na anatushangaza!

Tunapojikita katika usikivu wa kumsikiliza Yesu kiukweli,mawingu yanapotea,wasiwasi unaisha na kwa hakika ni kuacha nafasi;pia hofu zinaisha na kuwa na utulivu.Bwana daima anapokuja anapanga kila kitu vizuri hata kwetu sisi.Ni katika tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 21 Julai 2019 kwa waamini na mahujaji waliofika kiwanja cha Mtakatifu Petro Vatican

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumapili tarehe 21 Julai 2019 wakati wa Tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, katika  wa sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican amesema kuwa katika somo la Jumapili hii, mwinjili Luka anaelezea juu ya ziara ya Yesu katika nyumba ya Marta na Maria, dada zake Lazaro (Lk 10,38-42). Wao walimkaribisha na Maria akakaa chini ya miguu yake kumsikiliza, aliacha yote aliyokuwa akifanya ili kukaa na Yesu karibu. Hakutaka kupoteza katu maneno yake. Kila kitu kinawekwa pembeni kwa sababu Yeye anapokuja kutembea katika maisha yetu, uwepo wake na maneno yake ndiyo yanakuwa muhimu kabla ya yote. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha kwamba, “Bwana daima anatushangaza. Tunapojikita katika usikivu kumsikiliza kiukweli, mawingu yanapotea, wasiwasi unaisha na kwa hakika kuacha nafasi, hata hofu zinaisha na kuwa na utulivu; hali halisi mbalimbali za maisha zinapata mwafaka. Bwana daima anapokuja anapanga kila kitu vizuri hata kwetu sisi”.

Mtakatifu Luka anaonesha tabia ya sala ya mwamini

Katika kufafanua picha halisi ya Maria huko Betania, akiwa chini ya miguu ya Yesu Mtakatifu Luka, anaonesha tabia ya sala ya mwaamini, kuwa ambaya anajua kukaa katika uwepo wa Mwalimu wake ili kumsikiliza na kuwa na maelewano na yeye anasema Baba Mtakatifi. Hii ina maana ya kupumzika wakati wa siku, kutafakari kwa ukimya kwa muda wa kitambo ili kutoa nafasi kwa Bwana anayepita, na  ili kuweza kupata ujasiri wa kubaki kidogo pembeni na yeye na ili kuweza kurudia kuwa na utulivu na mwafaka katika mambo mengi ya kila siku. Akimsifu Maria aliyechagua, sehemu muhimu (Lk 10,42), Baba Mtakatifu Francisko amesema, Yesu utafikiri anarudia kwa kila mmoja wetu kusema: “usiache ukumbwe na mambo mengi ya kufanya, bali sikiliza hawali ya yote sauti ya Bwana, ili uweze kujikita kufanya kazi yako vizuri ya maisha uliyo kabidhiwa.

Mtakatifu Luka anasema ni Marta alimkaribisha Yesu     

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na tafakari anasema, kuna suala jingine la dada Marta. Mtakatifu Luka anasema kuwa ni yeye aliyemkaribisha Yesu (Lk 10,28). Labda Marta ndiye alikuwa dada mkubwa kati ya dada hao wawili, hatujuhi, lakini kwa hakika, mwanamke huyo alikuwa na karama ya ukarimu. Kwa dhati wakati Maria alikuwa anamsikiliza Yesu, yeye alikuwa anaangaikia huduma nyingi, amesema Baba Mtakatifu Francisko. Na kutokana na hiyo ndipo Yesu anamwambia: “ Marta, Marta , mbona unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi (Lk 10,41). Kwa maneno hayo lakini Yesu hakuwa na maana ya kumhukumu tabia ya huduma yake, anasema Baba yake zaidi ni ni kuhusu yale mahangaiko ambayo wakati mwingine anaishi. Hata kwa upende wetu,anathibtisha Baba Mtakatifu,  tunashirikishana wasiwasi wa Mtakatifu Marta, na kwa njia ya mfano wake, iweze kuwa  ni pendekezo ambalo katika familia zetu na katika jumuiya zetu ziweze kuishi kwa maana ya ukarimu, undugu na ili kila mmoja aweze kuhisi kuwa nyumbani, na kwa  kwa namna ya pekee wale walio wadogo na masikini wanapo bisha hodi katika milango, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.

Injili inatukumbusha hekima ya moyo inatokana na kutafakari na matendo

Injili ya leo, Baba Mtakatifu amaesema, inakumbusha kuwa, hekima ya moyo inatokana na kujua kuunganisha mambo mawili; kujua kutafakari na matendo ya dhati. Marta na Maria wanatuelekeza njia. Iwapo tunataka kuona maisha na furaha, tunapaswa kuunganisha tabia hizi mbili anasisitiza na kuongeza kusema: kwa upande mwingine ile tabia ya kukaa chini ya miguu ya Yesu ili kumsikiliza wakati anatuonesha siri za kila kitu. Na kwa upande mwingine kuwa wakarimu na ule utayari wa kukaribisha hasa  Yeye anapopita na kubisha hodi  milango yetu, kwa njia ya uso wa rafiki ambaye anahitaji muda wa kuhudumiwa na kidugu. Inahitajika ukarimu wa namna hiyo, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.

Mama Maria atupatie neema ya kupenda na kuhudumia Mungu na ndugu

Baba Mtakatifu akihitimisha tafakari yake, amesema, Maria Mtakatifu Mama wa Kanisa atupatie neema ya kupenda na kuhudumia Mungu na ndugu na mikono ya Marta na moyo wa Maria na kwa kubaki daima katika usikivu wa Kristo tunaweza kuwa wajenzi wa amani na matumaini. Hili ndilo jambo! Kwa njia ya tabia hizi sisi kiukweli tutakuwa wajenzi wa amani na matumaini.

22 July 2019, 09:15