Tafuta

Vatican News
Papa Francisko asikitishwa na vifo vya Mabaharia 14 waliokuwemo kwenye Manowari ya Kivita ya Urussi. Papa Francisko asikitishwa na vifo vya Mabaharia 14 waliokuwemo kwenye Manowari ya Kivita ya Urussi. 

Papa Francisko asikitishwa na vifo vya Mabaharia 14 wa Kirussi

Papa Francisko asikitishwa sana kuhusu taarifa za manoari ya kivita ya Urussi iliyoteketea kwa moto, Jumatatu tarehe Mosi, Julai 2019 huko Kursk na hivyo kusababisha mabaharia 14 kufariki dunia baada ya kuvuta hewa yenye sumu. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kutuma salam za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na kutikiswa sana na msiba huu mzito.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na taarifa za Manowari ya kivita ya Urussi iliyoteketea kwa moto, Jumatatu tarehe Mosi, Julai 2019 huko Kursk na hivyo kusababisha mabaharia 14 kufariki dunia baada ya kuvuta hewa yenye sumu. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kutuma salam za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na kutikiswa sana na msiba huu mzito. Manoari ya Kivita ya Urussi inasemekana imeteketea katika mazingira ya kutatanisha na kwamba, ilikuwa inatumiwa na Serikali kwa ajili ya kufanya tafiti za kisayansi.

Serikali ya Urussi imeunda tume maalum ili kuchunguza chanzo cha ajali hii. Wachunguzi wa mambo ya kivita wanasema, mara nyingi Manowari kama hizi zinatumika kwa ajili ya uchunguzi wa masuala ya kijeshi. Rais Vladimir Putin wa Urusi, ambaye anakutana na Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 4 Julai, baada ya taarifa ya ajali hii ya moto, alibadilisha ratiba yake na hivyo kukutana kwa dharura na Waziri wa Ulinzi, Bwana Sergey Shoigu.

Papa: Manowari
03 July 2019, 14:39