Tafuta

Tarehe 21 Julai ameaga dunia Kardinali José Manuel Estepa Llaurens, Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo la Kijeshi nchini Hispania Tarehe 21 Julai ameaga dunia Kardinali José Manuel Estepa Llaurens, Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo la Kijeshi nchini Hispania 

Papa Fracisko anakumbuka huduma ya ukarimu ya Kardinali Estepa Llaurens!

Katika telegram ya salam za rambirambi,Papa Francisko anaelezea uchungu wake kwa ajili ya kuondokewa na Kardinali José Manuel Estepa Llaurens,aliye kuwa Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo la Kijeshi nchini Hispania.Alikuwa na umri wa miaka 93.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa njia ya telegram kufuatia na kifo cha Kardinali José Manuel Estepa Llaurens, kilichotokea tarehe 21 Julai 2019 akiwa na umri wa miaka 93. Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha huduma yake kichungaji kwa ukarimu kwa ajili ya Kanisa!

Ukaribu wa Papa kiroho

Katika salam za rambi rambi alizotumwa kwa Askofu Mkuu Juan del Río Martín, ambaye kwa sasa ni Askofu Mkuu  wa Castrense ya uhispania, Baba Mtakatifu Francisko anakumbuka sura ya Marehemu Askofu Mkuu mstaafu José Manuel Estepa Llaurens aliye kuwa ni msimamizi wa Jimbo la Kijeshi katika nchi  ya Hispania na kwa shukrani ya matunda ya jitihada zake. Baba Mtakatifu wakati huo katika barua hiyo  amemwomba Askofu Mkuu amfikishie salam zake za rambi rambi na ukaribu wake kiroho kwa ndugu wa marehemu Kardinali Estepa, mapadre na waamini wote wa jimbo la kijeshi. Baba Mtakatifu aidha anasali kwa ajili ya roho ya marehemu na kuwatumia wakati huo huo baraka ya kitume kama ishara ya imani na matumaini katika Kristo Mfufuka.

22 July 2019, 15:37