Tafuta

Vatican News
Misa ya ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya SECAM huko Kampala Uganda Misa ya ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya SECAM huko Kampala Uganda 

Papa atuma ujumbe katika maadhimisho ya miaka 50 ya SECAM!

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa maaskofu wa Afrika waliunganika nchini Uganda kwa ajili ya Mkutano Mkuu 18 wa Mwaka na ambao pia unaadhimisha Jubilei ya dhahabu ya SECAM.Ujumbe uliotiwa sahini na Katibu wa Vatican Pietro Parolin umesomwa Jumapili tarehe 21 Julai 2019 katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu huko Lubaga na Balozi wa Vatican nchini Uganda,Askofu Mkuu Luigi Bianco

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa maaskofu wa Afrika ambao wameunganika nchini Uganda katika Mkutano Mkuu wa 18 wa SECAM na maadhimisho ya Jubilei ya dhahabu yaani ya  Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki na Madagascar (SECAM). Ujumbe huo umetumwa kwa Askofu  mkuu Gabriel Mbilingi, C.S.Sp., wa Jimbo Kuu la Lubango. Ni katika Mkutano ulionza tarehe 21 na utamalizika 28 Julai 2019, kwa kuongozwa na kauli mbiu:“Kanisa, familia ya Mungu Barani Afrika; Sherehekea Jubilei yako! Mtangaze Kristo Yesu Mkombozi wako”. Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa maaskofu ambao umetiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, umesomwa tarehe 21 Julai 2019 na Balozi wa Vatican nchini Uganda, Askofu Mkuu Luigi Bianco, katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu huko Lubaga, Kampala Uganda.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu matashi mema ya uinjilishaji

Katika ujumbe wake Baba Mtakatifu Francisko anayo furaha kubwa ya maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu wa Afrika ya Mashariki  na Madagascar (SECAM) na anawaomba kwa ukunjufu wamfikishie salam kwa washiriki wote wa tukio hilo, kwa kuungana nao katika kushukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya neema nyingi walizopokea SECAM na kwa ajili ya muungano kindugu ambao anasema, ni tabia ya kazi yake katika miaka hii 50 ya mwisho. Katika ujumbe wake Baba Mtakatifu Francisko aidha unasema, wajumbe wake waweze kuongeza nguvu zao katika shughuli ya utume kimisionari; kwa ajili ya kazi ya uinjilishaji na ambao unajikita katika jitahada za kufanya Injili iweze kupenya kila mantiki ya maisha yetu na kwa maana hiyo, anaongeza kusema, sisi kwa mara nyingine tena tunaweza kuwapelekea wengine. Na katika mtindo huo Baba Mtakatifu emesema kuwa, SECAM itaendelea kuwa katika huduma yenye thamani kwa ajili ya Makanisa mahalia na kwa ajili ya kupeleka msaada katika bara lote la Afrika. Katika ujumbe huo anahitimisha kwa kusema kwamba: kwa wote wanao shiriki maadhimisho hayo, kwa njia ya maombezi ya Maria, Mama wa Kanisa, anawapa baraka ya kitume kama ahadi ya amani na furaha ya Bwana.

22 July 2019, 12:06