Papa akumbusha miaka 50 tangu binadamu akanyage mwezini!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Mara baada ya tafakari ya neno la Mungu na sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili 21 Julai 2019 kwa waamini na mahujaji wote walionganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko amwakumbusha miaka 50 iliyopita tarehe kama ya 20 Julai kwamba mtu alikanyaga mwezini kwa kutimiza ndoto maalum. Lakini kumbukumbu hii kubwa Baba Mtakatifu amesema iweze kuwa kwa ajili ya ubinadamukatika kuwasha utashi wa kuendelea kwa pamoja katika matazamio yaliyo makubwa zaidi; zaidi kuwepo na hadhi kwa walio wadhaifu, haki zaidi kati ya watu na wakati endelevu ulio mzuri wa nyumba yetu ya pamoja.
Salam mbalimbali kwa mahujaji
Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia mahujaji wote kutoka pande zote za dunia, kwa namna ya pekee manovizi wa Shirika la Bikira Maria mwombezi kutoka pande tofauti za dunia. Aidha amewasalimia kwa namna ya pekee baadhi ya wale ambao watakwenda Patagonia,na kwamba kuna mahitaji ya kufanya kazi kule! Salam kwa wanafunzi kutoka Paraguay, waseminari , vijana na wanalimu wao wa Shirika la Padre Guanella kutoka nchini Romania, wengine kutoka Chiry-Ourscamp Ufaransa na waamini wa Cantù. Kwa wote amewatakia Dominika njema, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake!