Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha waamini na mahujaji waliofika katika sala ya Malaika wa Bwana tarehe 21 Julai 2019  juu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya binadamu kukanyaga mwezini Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha waamini na mahujaji waliofika katika sala ya Malaika wa Bwana tarehe 21 Julai 2019 juu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya binadamu kukanyaga mwezini  

Papa akumbusha miaka 50 tangu binadamu akanyage mwezini!

Jumapili 21 Julai 2019 mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji wote waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro,Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha kilele cha kumbukumbu ya miaka 50 tangu binadamu wa kwanza kukanyaga mwezini kunako tarehe 20 Julai 1969.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari ya neno la Mungu na sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili 21 Julai 2019 kwa waamini na mahujaji wote walionganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko amwakumbusha miaka 50 iliyopita tarehe kama ya 20 Julai kwamba mtu alikanyaga mwezini kwa kutimiza ndoto maalum. Lakini kumbukumbu hii kubwa Baba Mtakatifu amesema iweze kuwa kwa ajili ya ubinadamukatika kuwasha utashi wa kuendelea kwa pamoja katika matazamio yaliyo makubwa zaidi; zaidi kuwepo na hadhi kwa walio wadhaifu, haki zaidi kati ya watu na wakati endelevu ulio mzuri wa nyumba yetu ya pamoja.

Salam mbalimbali kwa mahujaji

Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia mahujaji wote  kutoka pande zote za dunia, kwa namna ya pekee manovizi wa Shirika la Bikira Maria mwombezi kutoka pande tofauti za dunia. Aidha amewasalimia kwa namna ya pekee baadhi ya wale ambao watakwenda Patagonia,na kwamba kuna mahitaji ya kufanya kazi kule! Salam kwa wanafunzi kutoka Paraguay, waseminari , vijana na wanalimu wao wa Shirika la Padre Guanella kutoka nchini Romania, wengine kutoka  Chiry-Ourscamp Ufaransa na waamini wa Cantù. Kwa wote amewatakia Dominika njema, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake!

22 July 2019, 09:14