Tafuta

Vatican News
Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Kimisionari duniani 2019"ukiongozwa na kaulimbiu:Mmebatizwa na kutumwa. Kanisa la Kristo katika utume duniani". Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Kimisionari duniani 2019"ukiongozwa na kaulimbiu:Mmebatizwa na kutumwa. Kanisa la Kristo katika utume duniani".  (2019 Getty Images)

Ujumbe wa Siku ya Kimisionari duniani 2019:Mmebatizwa na kutumwa”. Kanisa la Kristo katika utume duniani

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Juni wakati wa sikukuu ya Pentekoste ametoa ujumbe wake wa Siku ya Kimisionari duniani kwa mwaka 2019 ukiongozwa na kauli mbiu sawa sawa na ile ya Mwezi maalum Oktoba wa Kimisionari isemayo:"Mmebatizwa na kutumwa”.Kanisa la Kristo katika utume duniani,kufuatia na Maadhimisho ya Miaka 100 tangu Papa Benedikto XV alipotangaza Waraka wake wa Kitume uitwao"Maximum Illud".

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 9 Juni 2019 ikiwa ni sikukuu ya Pentekoste, Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wa Siku ya Kimisionari duniani 2019 utakaoadhimishwa tarehe 20 Oktoba, ambapo anasema kwamba kwa ajili ya mwezi Oktoba 2019 yeye ameomba Kanisa zima kuishi kipindi maalum cha Kimisionari kwa ajili ya kufanya kumbukumbu ya miaka 100 tangu kutangazwa kwa Waraka wa Kitume wa Maximum Illud wa Papa Benedikto XV (30 Novemba 1919, waraka unaohusu shughuli za Kimisionari). Unabii wa muda mrefu wa pendekezo la kitume umemfanya Baba Mtakatifu atambue ni kwa jinsi gani hata leo hii kuna umuhimu wa kupyaisha jitihada za kimisionari za Kanisa, na kuboresha kwa maana ya kiinjili utume wake wa kutangaza na kupeleka duniani kote  wokovu wa Yesu Kristo aliyekufa na kufufuka, ameandika Baba Mtakatifu.

Mmebatizwa na kutumwa.  Kanisa la Kristo katika utume duniani

Baba Mtakatifu anasema kauli mbiu ya ujumbe huo ni sawa sawa na Tema ya mwezi Oktoba! Yaani “Mmebatizwa na kutumwa. Kanisa la Kristo katika utume duniani”. Katika kuadhimisha mwezi huo utasaidia hawali ya yote kujitafiti kwa maana ya kimisionari katika imani yetu kwa Yesu Kristo, imani ya bure tuliyoipokea kama zawadi katika ubatizo. Ushiriki kama wana wa Mungu siyo tendo tu la binafsi, bali daima ni la kikanisa, yaani kutoka katika muungano na Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, yanazaliwa maisha mapya pamoja na ndugu kaka na dada. Maisha haya ya Mungu siyo bidhaa ya kuuza, anabainisha Baba Mtakatifu, yaani sisi kufanya upropaganda bali, ni utajiri wa kutoa, kuhabarisha, kutangaza na ndiyo maana ya utume. Tumepewa bure zawadi hiyo na  bure tunashirikishane bila kubagua yoyote, anahimiza. Mungu anataka watu wote waokolewe ili waweze kufikia utambuzi wa ukweli na uzoefu wa neema ya huruma yake katika Kanisa,  sakramenti ya dunia ya wokovu  (taz, 1 Tm 2,4; 3,15; CONC. ECUM. VAT. II, Cost. dogm. Lumen gentium, 48).

Kanisa ni la Kitume duniani

Baba Mtakatifu akifafanua juu ya nini maana ya “Kanisa ni la kitume duniani” anasema, imani kwa Yesu Kristo inatupatia haki ya ukuu wa mambo yote kwa kufanya tutazame dunia kwa macho na moyo wa Mungu; matumaini yanatufungulia upeo milele wa maisha ya Mungu ambayo kweli tunashiriki; upendo ambao tunaonja katika Sakramenti na katika upendo kidugu, unatusukuma hadi miisho ya dunia (taz Mi 5,3; Mt 28,19; At 1,8; Rm 10,18). Kanisa linalotoka nje hadi miisho ya dunia linataka uongofu wa kuendelea wa kimisonari na wa kudumu, anaandika Baba Mtakatifu. Aidha amesema, ni watakatifu wangapi, wanawake na wanaume wa imani ambao wameshuhudia, wanaonesha uwezakano na  matendo ya ufunguzi usio na kikomo, kwenda na  huruma kama msukumo wa dharura ya upendo na mantiki zake za zawadi, za sadaka na kutoa bure (taz 2 Wakor 5,14-21)! Awe mtu wa Mungu anayehubiri Mungu (taz WarakaMaximum illud).

Hali inayotugusa kwa karibu ni kutumwa

Baba Mtakatifu Francisko anasema kutumwa kunatuguswa kwa karibu, kwa maana mimi daima ni mtume: wewe daima ni mtume ; kila mbatizwa ni mtume. Anayependa haachi kamwe kutembea na amesukumwa kutoka  nje yake, anavutiwa na kuvuta , anajitoa kwa wengine na kujifungulia mahusiano ambayo yanazaa maisha. Hakuna hasiye hasiyefaa na bila kuwa na maana kwa ajili ya upendo wa Mungu. Kila mmoja wetu ni mtume katika dunia kwa sababu ni tunda la upendo wa Mungu. Baba Mtakatifu anatoa mfano kkwamba:” Hata kama baba yangu na mama yangu wananisaliti kwa upendo wa ulaghai, chuki na ukosefu wa uaminifu, lakini hatuwezi kuondoka kamwe katika  zawadi ya maisha yenye hatima ya kila mwana wake na dunia  katika maisha ya Mungu na milele (taz Ef 1,3-6). Maisha haya yanathibitishwa  na Ubatizo ambao unatupatia imani katika Yesu Kristo mshindi wa dhambi na kifo,na kutufanya kuwa mfano na sura ya Mungu na kutuingiza katika mwili wa Kristo ambaye ni Kanisa. Kwa maana hii, Ubatizo ni wa lazima kweli kwa ajili ya wokovu kwa sababu unatuhakikishia kuwa sisi ni wana. Daima na kila mahali, kamwe  hakuna aliye yatima  wageni au watumwa katika nyumba ya  Baba.

Kile ambacho kweli ni hali halisi ya sakramenti tunayo itimiza ni Ekaristi anabainisha Baba Mtakatifu, ambayo inabaki  kuwa wito na hatima ya kila mwanaume na mwanamke katika kusubiri uongofu na wokovu. Ubatizo kwa hakika ni ahadi iliyotimizwa na zawadi ya Mungu kwa kufanya mwanaye awe binadamu na Mwana. Sisi ni watoto wa wazazi  asili, lakini katika Ubatizo tumepewa asili ya ubaba na umama wa kweli: Haiwezekani kuwa na Mungu kama Baba bila kuwa na  kuwa na Kanisa kama Mama (Taz, Mtakatifu Ciprian ; Umoja wa Kanisa, 4). Kwa njia hiyo katika ubaba wa Mungu na katika umama wa Kanisa unajikita mzizi wa utume wetu, kwani katika Ubatizo umewekwa mhuri wa kutumwa kilelezo cha Yesu wakati wa Pasaka: “Kama baba alivyonituma mimi hata mimi nawatuma mkiwa mmejazwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya uongofu wa dunia (Yh 20,19-23: Mt 28,16-20). Kwa Mkristo anapewa zoezi la kutumwa ili pasiwepo yoyote hasiye tangaziwa wito wake wa kuwa mwana, uhakika wa hadhi yake binafsi na thamani zake za kuwa na maisha ya binadamu tangu kutungwa kwake hadi kifo chake cha kawaida.

Kuenea kwa mawazo ya ulimwengu yanazuia udugu wa kweli

Katika kuenea sana kwa mawazo ya kiulimwengu dhidi ya uchanya na utamaduni wa shughuli za ubaba wa Mungu katika historia yetu, unazuia kila udungu wa kweli wa dunia ambao unajieleza kama upamoja, kulingana na maisha ya kila mtu. Bila Mungu wa Yesu Kristo, kila tofauti inaleta hatari na kutowezesha kila ya aina ya mapokezi kindugu na umoja wa kina unaozaa ubinadamu. Hatima ya dunia ya wokovu ulioletwa na Mungu katika Yesu ulimfanya Papa Benedikto XV aweze kushinda kila aina ya kujifungia kitaifa na kikabila. Hata katika Tangazo la Injili wakati wa nguvu ya ukoloni na upendeleo  wa kiuchumi  na kijeshi. Katika Waraka wake wa Kitume Maximu Illud, Papa anakumbusha kuwa ulimwengu wa Mungu katika utume wa Kanisa unahitaji kutoka nje, nje ya nchi yake, hata ukoo wake binafsi. Ufunguo wa utamaduni na jumuiya ya mapya ya wokovu wa Yesu Kristo unahitaji kushinda kila aina ya vizingiti hivyo. Hata leo hii Kanisa linaendelea kuwa na mahitaji ya wanaume na wanawake ambao kwa karama ya utabitizo wao wanaweza kwa kuitikia wito wa kuacha nyumba zao na familia zao, nchi zao, lugha zao na Kanisa lake mahalia. Hawa wametumwa kwa watu katika dunia ambayo bado haijafikiwa na Sakramenti za Yesu Kristo na za Kanisa lake Takatifu.

Kutangaza Neno la Mungu

Baba Mtakatifu anafafanua juu ya kazi  za kimisionari kuwa: kutangaza Neno la Mungu, kushuhudia Injili na kuadhimisha maisha katika Roho ni mwaliko wa uongofu, kwani wanabatiza na kutoa wokovu kwa wakristo kulingana na uhuru wa kila mtu binafsi, katika mazungumzo na utamaduni ,na dini za watu ambao wametumwa huko. Utume wa watu (missio ad genetes) daima ni wa lazima katika Kanisa, kwa kuchangia kwa namna msingi ya mchakato wa kudumia shughuli za uongofu wa wakristo wote. Imani ya Pasaka ya Yesu Kristo, ya kutumwa kwa Kanisa iliyobatizwa na kwenda mbali na utamaduni wake, nyumba yake, mahitaji ya wokovu dhidi ya dhambi na uhuru dhidi  ya ubaya binafsi na kijamii, vinahitaji utume hadi mwisho wa dunia .

Baba Mtakatifu amesema kuwa zawadi ya Mungu haikukosekana katika maadhimisho ya Sinodi  Maalum ya Makanisa ya Amazon, ambayo anasisitza kama utume uliokabidhiwa na Yesu na zawadi ya Roho yake  ambayo bado ipo hata sasa na ya lazima, hata katika ardhi zile na wakazi wake. Ni upyaisho wa Pentekoste inayofungua milango ya Kanisa ili pasiwepo na utamaduni wowote uliojifungia binafsi na pasiwepo watu wowote ambao wanabaki wamejibagua, lakini wamejifungulia katika umoja wa ulimwengu mzima katika imani. Hakuna yoyote abaki amefungia binafsi, kujitosheleza na kabila lake na dini. Pasaka ya Yesu ipasue vizingiti vikubwa vya dunia, dini na utamaduni, kwa kuwaalika kukua kulingana na hadhi ya mwanaume na mwanamke kuelekea katika uongofu uliojaa daima ukweli wa Bwana Mfufuka ambaye anatoa maisha ya kweli kwa wote. 

Maneno ya Papa Mstaafu Benedikto XVI katika mkutano wa Aparecida

Kufuatia na mapendekezo hayo Baba Mtakatifu Francisko anakumbuka  maneno ya Papa mstaafu  Benedikto XVI, mwanzoni wa Mkutano wao wa Maaskofu wa Amerika ya Kusini huko Aparecida nchini Brazil kunako 2007. Ni maneno ambayo amependelea yawe kama ya kwake yaliyokuwa yanasema : Nini maana ya kukubali imani ya kikristo kwa nchi za Amerika ya Kusini na Carribien? Kwa wao yana maana ya kujua na kupokea Kristo, Mungu hasiye julikana na ambaye mababu zao bila kujua walikuwa wanamtafuta katika utajiri wao wa utamaduni wa kidini. Kristo alikuwa Mwokovu na ambaye alionekana kwa ukimya. Ina maana pia ya kupokea kwa maji ya Ubatizo, maisha ya Mungu ambayo yaliwafanya wana wa Mungu; wa kupokea pia Roho Mtakatifu ambaye alizaliwa katika utmaduni wao, kuwatakasa  na kuendeleza idadi kubwa za vichipukizi. Ni yule  Neno lililofanyika mwili likawa w kwao kwa kuwalekekeza katika njia ya Injili (…) Neno la Mungu aliyefanyika mwili katika Yesu Krito alifanya hata historia na utamaduni. Na kwa Mama yetu Maria tumkambidhi utume wa Kanisa. Yeye aliyeungana na mwanae tangu kutungwa mimba na Bikira hadi kujikita katika mchakato wa safari. Alijiachia kabisa  kuhusika katika utume wa Yesu; katika utume ambao hata chini ya msalaba ulikuwa ni utume wake. Kushirikiana kama Mama wa Kanisa kwa kuzaliwa na Roho na katika imani ya wana wapya wa Mungu.

Maana ya shughuli za kipapa za kimisionari POM

Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha na maneno mafupi kuhusiana na shughuli za kipapa za kimisionari (POM) zilizo pendekezwa tayari na Maximu Illud kama chombo cha kimisioanari. POM inajieleza katika huduma ya Papa kwenye shughuli zake za Kanisa kwa ngazi ya kitaifa ni kuhifadhi uhai wa roho ya kimisionari kwa njia ya kuhamasisha, na mafunzo ya kimisionari; kutia moyo katika sala; kukukuza mafunzo ya kimisonari; kukuza kwa namna ya pekee utoaji na makusanyo ya sadaka kwa ajili ya Siku ya Kimisionari duniani; na kushirikiana na Shirika la habari za kimisionari Fides, kiungo muhimu cha kutoa habari za POM. Baba Mtakatifu hatimaye kwa wamisionari wote duniani na wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wanashiriki kwa nguvu za ubatizo utume wa Kanisa anawatumia baraka yake.

SIKU YA KIMISIONARI 2019
09 June 2019, 14:12