Tafuta

Vatican News
Tarehe 5 Juni Bwana Mungu amemwita kwake Kardinali Elio Sgreccia Tarehe 5 Juni Bwana Mungu amemwita kwake Kardinali Elio Sgreccia 

Telegram ya Papa kufuatia na kifo cha Kard.Sgreccia

Tarehe 5 Juni 2019 asubuhi huko Santangelo Ancona Bwana Mungu amemwita kwake mtumishi wake Kardinali Elio Sgreccia na Rais Mstaafu wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha.Katika telegram ya Papa anaonesha masikitiko makubwa na kuwapa salam za rambi rambi wana familia na wote wanaoombolezwa kutokana na msiba huo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma telegram yake kwa Professa Palma Sgreccia  kufuatia ka Kifo cha Kardinali  Elio Sgreccia kilichotokea tarehe 5  Juni 2019 asubuhi  huko Santangelo Ancona. Kardinali alikuwa ni Rais Mstaafu wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha.  Katika telegram  hiyo anaonesha masikitiko makubwa kwa baba yake mdogo Kardinali Elio Sgreccia na kuwapa salam za rambi rambi wana familia na wote wanaoombolezwa kwa ajili yake. Anamkumbuka kwa shukrani kubwa kwa moyo wa ukarimu katika huduma ya Kanisa hasa thamani msingi ya utetezi msingi wa thamani ya maisha ya binadamu, wakati akiwa hai kwenye matendo ya utafiti, wa mafunzo ya uinjilishaji. Baba Mtakatifu anaiombea roho ya marehemu ili Bwana kwa maombezi ya Bikira Maria aipokee kama mtumishi wa Injili katika furaha na amani ya milele. Anawatumia baraka yake ya kitume kwa wote wanaoshiriki uchungu kutokana na kuguswa na msiba huo.

Kardinali  Sgreccia alikuwa ni mtetezi msingi wa thamani ya maisha ya binadamu

Kardinali , na rais mstaafu wa Taasisi ya Kipapa la Elimu ya Maisha alikuwa amezalia kunako tarehe tarehe 6 Juni 1928 huko Nidastore ya  Arcevia, Ancona nchini Italia. Na hivyo tarehe 6 Juni alikuwa anatimiza miaka 91. Katika telegram ya Baba Mtakatifu Francisko kwa professa Palma mkufunzi  wa Elimu ya Maisha katika Chuo cha Kipapa cha Laterano anakumbushwa jinsi gani Kardinali alikuwa ni mtetezi wa maisha katika Taasisi hiyo.

Huduma ya kwanza alikuwa msimamizi wa vijana wa Chama Katoliki Italia

Alijikita katika kulinda maisha matakatifu ya binadamu tangu kuzaliwa hadi kifo cha kawaida. Majiundo yake ya kuwa kuhani yalianzia katika Seminari ya Fano na kupewa daraja la upadre tarehe 29 Juni 1952. Kama Padre kijana alipewa majukumu ya kuwasimamia vijana kiroho wa chama Katoliki cha vijana na baadaye kufuata kuwa kaimu Gombera wa Seminari ya Kanda. Akiendelea na majiundo yake alipata shahada ya masomo ya maandiko katika Chuo Kikuu cha Bologna na kuchaguliwa  kuwa Mkuu wa Seminari ya Kipapa ya Fano ambapo baadaye akahamishiwa katika Jimbo la Fossombrone.

Jitihada ya mafunzo ya elimu ya maisha

Mwaka 1973 katika kitivo cha madawa na ubingwa, cha Chuo Kikuu cha Moyo Mtakatifu Roma waliamua kuongeza nguvu ya huduma ya kichungaji kwa ajili ya jumuiya ya maprofesa na wanafunzi makuhani  na akachanguliwa  kuwa kama sura  ya  usimamizi wa Jumuiya ya Chuo Kikuu hicho. Baada ya miaka 19 akapewa tena majukumu ya kufundisha kuhusiana na masuala ya maadili katika elimu ya maisha na madawa. Tangu mwaka 1985 – 1992 alikuwa mkurugenzi wa kitivo cha maisha na Madawa ya Chuo Kikuu Katoliki. Ni mada nyingi  za Mafundisho ya  madawa na  mashirika na Taasisi nyingi kwa ngazi za Ulaya alizoshirikishana. Katika miaka ya 8 alikuwa  ni msimamizi wa Vatican katika Tume ya Maadili ya Baraza la Ulaya. Tangu 90-2006 alikuwa ni mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Italia  kwa ajili ya Elimu ya madawa na maisha!

Tangu 2005 ni Rais wa Taasisi ya kwa ajili ya maisha

Tarehe 5 Novemba 1992 alichaguliwa kuwa Askofu na Katibu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia. Akapewa daraja la uaskofu na Mtakatifu Yohane Paulo I,I tarehe 6 Januari mwaka uliokuwa unafuata. Kuanzia mwaka huo akiwa katika Baraza la Kipapa la familia hadi miezi ya  kwanza ya 1996 alianza kujikita kwa kina ndani ya ofisi hiyo kama  makamu rais wa taasisi hiyo na tangu tarehe 3 Januari 2005  hadi 2008  alikuwa rais wa taasisi hiyo ya kipapa ya maisha. Ni Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto alimchagua kuwa Kardinali tarehe 20 Novemba 2010. Kardinali ametoa mchango kubwa sana hata katika baadhi ya mada zinazohusu elimu ya maisha, utoaji wa viungo na sehemu zake zinazoishi nk. Kwa kifo cha Kardinali  Elio Sgreccia, Baraza la makardinali linabaki na jumla ya  220 na kati yake 120 wanaweza kuchaguliwa na 100 hapana.

06 June 2019, 13:03