Tafuta

Vatican News
Katika Jukwa la XI la Vijana duniani,wanaalikwa kujiandaa vema kwa tafakari ya Christus vivit na njia ya mchakato baada ya Sinodi 2018 ili kufikia siku ya vijana duniani 2022 hu Katika Jukwa la XI la Vijana duniani,wanaalikwa kujiandaa vema kwa tafakari ya Christus vivit na njia ya mchakato baada ya Sinodi 2018 ili kufikia siku ya vijana duniani 2022 hu 

Papa na vijana:ninyi muwe ujumbe wa umoja katika dunia inayogawanya!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Jukwaa la Kimataifa la XI la Vijana lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha na kuwahimiza vijana wawe taa katika giza nene la vijana wenzao ambao bado hawamjuhi Yesu.Na Mada itakayoongoza Siku ya Vijana duniani mwaka 2022 huko Lisbon inasema:“Maria aliamka na kwenda kwa haraka”.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kama baba anayewalekeza wanae njia ya kufuata, kama mchungaji anayesaidia zizi lake, kiongozi anayewasha mioyo kwa neema ya mwanga wa Kristo, ndivyo Baba Mtakatifu Francisko tarehe 22 Juni 2019 alivyofanya wakati wa kukutana mjini Vatican na kundi hili la washiriki wa Jukwaa hili kutoka pande zote za dunia. Ni vijana waliounganika kwa siku tatu katika Jukwaa la XI la Kimataifa huko Sassone Ciampio karibu na Roma kwenye jumba la Shirika la Wakarmeli. Ni katika Mkutano uliondaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, kwa lengo la kuhamasisha zaidi matendo hai  ya Sinodi ya 2018 iliyokuwa inaongozwa na mada: “ vijana, imani na mang’amuzi ya miito. Baba Mtakatifu katika hotuba yake kwa lugha ya kisipanyola amewakumbusha kuwa wanaitwa wawe taa  katika giza la vijana wenzao wengi ambao bado hawajatambua furaha ya maisha mapya katika Kristo. Ni mwaliko wa kusambaza ndani mwao moto wa Kristo ambao umo tayari ndani mwao na kutembea pamoja kwa sababu wao ni leo ya Mungu na leo ya Kanisa!

Vijana wa matendo katika Kanisa la kisinodi pia kuwa taa katika giza

Baba Mtakatifu Francisko amefafania juu ya umuhimu wa Jukwaa na kusema kuwa  linawafanya kuwa vijana na kuwa mstari wa mbele katika safari ya uongofu wa kichungaji ambao ni matarajio ya mababa wa Sinodi. “Ninyi ni vijana katika matendo hai ya Kanisa la Sinodi, na juu ya hili ninyi mmetafakari na katika siku hizi za mwisho”. Na kwa upande wa Wosia wake wa mwisho kwa ajili ya vijana  Christus Vivit, anawakumbusha tukio la mitume wa Emau, kama  mfano wa wa kuzingatia katika utume ambao wamekabidhiwa  vijana wa leo. Kwa  kumtambua  Yesu ambaye leo hii anafungua mioyo ya vijana amezungumza nao, ili wajikite katika hatua za safari hata katika usiku lakini bila kuogopa  kwenda, kwa sababu Kristo anawaangazia maisha yao. Baba Mtakatifu amesema, “ hata sisi siku moja tulikutana na Bwana katika njia zetu. Na kama mitume wa Emau, tunaitwa kuchukua mwanga wa Kristo katika giza la dunia. Ninyi vijana manitwa kuwa mwanga katika giza la vijana wenzenu ambao bado hawatambui furaha ya maisha mapya katika Yesu”.

Huzuni na moto unaowaka

Kuna haja ya kutengeneza jumuiya, furaha ya kukaa pamoja na baadaye hata huzuni wakati wa kuagana kurudi nyumbani. Hata hivyo Mitume wa Emau na vijana wa Jukwa wamefanya uzoefu kwa kuishi katika hatua hizi, japokuwa  Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha kuwa, Yesu siyo hazina ya kufungia ndani, bali ni fumbo la kushirikishana  na kadiri wanavyo mpeleka zadi kwa wengine wengi, ndivyo wataweza kuhisi zaidi uwepo wao katika maisha ya kila mmoja. “Nina uhakika kwamba mtafanya hivyo mtakaporudi katika maeneo yenu ya asili”, amesema Baba Mtakatifu. Katika maelezo kuhusu Emau ni kwamba, Yesu aliwasha moto katika mioyo ya mitume. Na kama mjuavyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, ili moto husiweze kuzima inabidi kuuchoche upanuke na kuenea. Kwa maana hiyo pashweni na moto wa Kristo ambaye yumo ndani mwenu”.

Kanisa linawahitaji ninyi

Baba Mtakatifu Francisko akiendela na hotuba take aidha amewakubusha vijana wawe wajumbe wa umoja katika dunia ambayo imegawayika na kwamba wawe “viungo vya mwili mmoja, vinavyoungana na wengine kwa kuongozwa na upendo wa Kanisa na kutembea kwa pamoja, huku mkichukua mwanga wa moto wa Yesu katika giza la ulimwengu huu”. “Ninyi ni leo ya Mungu, leo hii ya Kanisa! Siyo wa wakati ujao, bali leo hii”. “Kanisa linahitaji ninyi kujiaminisha wenyewe. Kama Kanisa ninyi ni Mwili wa Bwana Mfufuka aliyepo duniani”. Baba Mtakatifu  Francisko ameomba wakumbuke daima kwamba wao ni wajumbe wa mwili mmoja. Wao wanafungamana mmoja na mwingine na pekee yao hawawezi kuishi. Wanahitaji  msaada ya kila mmoja ili kufanya kweli utofauti katika ulimwengu unaojaribiwa na mgawanyiko.

Siku ya Vijana duniani katika umbu la Maria

Baada ya kumaliza hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko ametangaza mada iliyochaguliwa ya Siku ya Vinana duniani huko Lisbon 2022: Maria alifunga safari akaenda kwa haraka “ na kuwashauri  kuanzaia sasa watafakari katika miaka hii miwili juu ya Injili isemayo “ kijana nakuamuru amka ! Amka! Ninakuweka kuwa  shahidi katika mambo uliyoyaona! Na ili kuweza kufikia siku ya vijana wakiwa wamejiandaa vema nchini Ureno. Baba Mtakatifu anatamani kwa  mara nyingine tena kuwa maandalizi hayo yawe  mchakato mkubwa wa maendeleo kuelekea Siku ya Vijana huko Lisbon na kutembea katika njia ya baada ya Sinodi. Amewahimiza wasidharau sauti ya Mungu ambayo inawasukuma waamke na kufuata njia ambayo Bwana amewaandalia. Kama Mama Maria pamoja naye, kila siku wao ni wachukuzi wa furaha yake na upendo wake.

22 June 2019, 13:05