Tafuta

Vatican News
Misa ya Baba Mtakatifu Pentekoste 2019 Misa ya Baba Mtakatifu Pentekoste 2019  (Vatican Media )

Papa akumbuka Mwenyeheri Michele Giedroyc wa Cracow, Poland!

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu,amekumbusha waamini wote kuwa mjini Cracow nchini Polond tarehe 8 Juni 2018 wameathimisha misa ya shukrani kwa ajili ya kuthibitisha ibada ya Mwenyeheri Michele Giedroyc.Amewaombea watu wa Sudan ili waweze kusitisha migogoro kwa njia ya mazungumzo na pia kuwatakia sikukuu njema ya Pentekoste kwa mahujaji wote na waamini waliofika katika maadhimisho hayo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu, amekumbusha waamini wote kuwa mjini Cracow nchini Polond  tarehe 8 Juni 2018 waliadhimisha misa ya shukrani kwa ajili ya kuthibitisha ibada ya Mwenyeheri Michele Giedroyc, ambapo katika maadhimisho hayo walishiriki Maaskofu wa Poland na Lithuania. Baba Mtakatifu anasema tukio hilo linawatia moyo watu wa Poland na Lithuania ili kuimarisha mahusiano katika ishara ya imani na ibada kwa Mwenye heri Michele, aliyeishi huko Cracow katika karne ya 15, ambaye ni mfano wa unyenyekevu na upendo wa kiinjili.

Uchungu na wasiwasi wa habari za Sudan

Aidha Baba Mtakatifu Francisko ameonesha uchungu na wasiwasi kufuatia na habari zinazosikika kwa siku hizi nchini Sudan. Anawaombea watu hao ili waweze kusitisha ghasia na kutafuta wema wa pamoja kwa njia ya mazungumzo.

Salam kwa mahujaji

Baba Mtakatifu anawasalimia wote mahujaji kutoka Italia na sehemu mbalimbali za dunia ambao wameshiriki maadhimisho hayo kama makundi, vyama na waamini wote. Kwa hakika anawatia moyo ili waweze kujifungulIi  mwanga wa upole wa Roho Mtakatifu kwa kutoa karama mbalimbali duniani ambayo ni sura ya Mungu katika umoja. Na Bikira Maria kwa maombezi yake aweze kutujalia neema hii ambayo sisi tunamkimbilia kama watoto.

09 June 2019, 13:30