Vatican News
Baba Mtakatifu ameadhimisha misa Takatifu katika uwanja wa Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu ameadhimisha misa Takatifu katika uwanja wa Mtakatifu Petro  (Vatican Media)

Papa katika Misa ya Pentekoste:Roho Mtakatifu bado anatia nanga ya matumaini!

Katika sikukuu ya Pentekoste tarehe 9 Juni 2019,Baba Mtakatifu ameadhimisha Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifru Petro akikazia juu ya maelewano ya wakati wetu ambao utafikiri umewekwa pembeni ijapokuwa anabainisha Roho Mtakatifu anajua kupangilia kila kitu kwa sababu ni mtaalam!Je anafanyaje?Baba Mtakatifu anaelekeza kwa tutawazame Mitume.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baaada ya siku hamsini Pentekoste iliwafikia wafuasi katika siku zisizo na uhakika. Kwa upande mwingine wakiwa wamejazwa na furaha walikuwa wamemwona Yesu Mfufuka, kumsikiliza na walikuwa pia wamekula naye. Kwa upande mwingine walikuwa bado hawajashinda ile hofu na wasiwasi kwa maana milango yao ilikuwa imefungwa (taz, Yh 20,19.26) wakiwa na matarajio madogo na wasio kuwa na uwezo wa kumtangaza anayeishi. Ndipo kwa ghafla akafika Roho Mtakatifu na wasiwasi ukapotea. Wafuasi hawakuwa na hofu tena, hata mbele ya yule aliyekuwa anakuja kuwakamata. Kwanza walikuwa na wasiwasi wa kuokoa maisha lakini  sasa hawaogopi tena kufa; kwanza walikuwa ndani wamefunga milango katika nyumba ya Karamu Kuu, sasa wanatangazia watu wote. Baba Mtakatifu Francisko amefafanua kuwa, hadi kupaa kwa Yesu, walikuwa wanasubiri Ufalme wa Mungu ufike (Mdo 1,6) na sasa hawana subiri kwani wanataka wafikie miisho isiyojulikana. Kwanza walikuwa hawajawahi kuzungumza mbele ya umati na kama walifanya hivyo, mara nyingi walitenda janga fulani kwa mfano Petro alimkana Yesu; na sasa wanazungumza kwa wote kwa lugha.

Mambo ya wafuasi yaliyokuwa yamesimama na sasa yanapyaishwa

Masuala ya wafuasi ambayo yalikuwa yanafanana kama ni kituo cha kusimama, kwa sasa yanapyaishwa na ujana wa Roho: Vijana wale waliokuwa kama kitoweo cha ukosefu wa uhakika, walihisi kufika sasa na walibadilishwa na furaha iliyowafanya kuzaliwa kwa upya. Roho Mtakatifu aliwafanya hivyo. Roho Mtakatifu siyo kama tunavyoweza kufikiria kuwa ni  kitu kisichokuwapo;  na kumbe ni mtu zaidi na aliye karibu zaidi  na ambaye anatubadili maisha, je anafanyaje? Baba Mtakatifu anaelekeza kuwa "Tutawazama Mitume". Hata hivyo Roho Mtakatifu hakuwafanyia mambo yaliyo rahisi hakutenda  kwao miujiza ya kushangaza, hakuondoa matatizo katikati yao na wapinzani wao. Roho Mtakatifu aliwaletea maelewana  wafuasi katikati yao ambayo yalikuwa yanakosekana maelewano yake, kwa sababu yeye ni maelewano.

Maelewano ndani ya mtu

Ndani ya moyo wa wafuasi walikuwa wanahitaji kubadilishwa. Katika historia yao inaonesha wazi kwamba hata kufikia kumwona Mfufuka haitoshi, iwapo hapokelewi kwa moyo. Haitoshi kumjua kuwa ni mfufuka iwapo hauishi kama Mfufuka. Na ndiye  Roho Mtakatifu anayefanya  kuishi kwa upya Yesu ndani mwetu na ambaye anafufuka kwa upya ndani mwetu. Kwa maana hiyo Yesu alipokutana na wake  anarudia kusema “ Amani kwenu” (Yh 20,19.21) na kuwavuvia Roho. Kuwa na amani hatokani na kuweka nje vizuri matatizo. Mungu haondoi mahangaiko kwa walio wake na mateso, badala yake ni katika kupokea Roho Mtakatifu. Ni amani ile waliyopokea mitume, amani isiyoondoa matatizo, bali ni  amani wanayopewa kila mmoja katika katika matatizo.

Amani ni kama iliyo tulia ndani ya kina cha bahari

Ni amani inayofanya moyo ufafanane na kina cha bahari ambayo daima ina utulivu wakati juu yake  kuna machafuko ya mawimbi. Ni maelewano ya kina ya namna hiyo yanaweza kukubadili kuwa heri hadi katika mateso. Ni mara ngapi kinyume chake tunabaki kijuu juu! Baba Mtakatifu anabainisha badala ya kutafuta Roho tunajaribu kubaki katika mashindano, kwa kufikiria kila kitu kitakuwa bora iwapo janga lile litapita, iwapo sitomwona yule mtu, iwapo hali ile itakuwa bora zaidi. Lakini hiyo ni kubaki katika hali ya kijujuu. Tatizo moja likiisha jua kuwa lingine linaanza na mahangaiko yanarudia tena. Siyo kwenda mbali na  hali halisi kwa kufikiria tutakuwa na utulivu au katika kusawazisha janga fulani la wakati, tutakuwa na amani. Mwamko ni amani ya Yesu, ni maelewano na Roho! Amesisitiza Baba Mtakatifu.

Ukosefu wa maelewana kwa nyakati zetu

Leo hii katika nyakati za haraka utafikiri maelewano yamewekwa pembezoni. Kwa kukimbilia katika maelfu ya mambo ya kufanya, ipo hatari ya kukosa uvumilivu ana kuendelea kutenda vibaya kwa kila kitu. Na kutafuta suluhisho la haraka ambalo ni kumeza tembe na kuendelea mbele kwa kuhisi kwamba unaishi. Lakini zaidi ya hayo tunahitaji Roho. Ni yeye anayeratibu kila hali. Yeye ni amani katika mahangaiko, imani  wakati wa kukata tamaa ni furaha katika huzuni, ujana katika uzee, ujasiri katika majaribu. Ni yeye ambaye kati ya pepo za dhoruba za maisha anatia nanga ya matumaini. Ni Roho ambaye kama asemavyo leo hii Mtakatifu Paulo ametuzuia kuangukia katika woga kwa sababu anafanya tuhisi kuwa  wana wa Mungu ( Rm 8,15). Ni mfariji ambaye anatuonesha ukarimu wa Mungu. Bila Roho maisha ya Kikristo yamefunguliwa na kukosa upendo ambao unaunganisha. Bila Roho ya Yesu yeye anabaki kama mtu maarufu wa nyakati zilizopita na Roho ni mtu aliye hai leo hii; bila Roho maandiko ya barua zinazo mhusu zimekufa, na kwa njia ya Roho ni Neno la Maisha.  Mkristo bila Roho ni maadili yasiyokuwa na furaha ; na kwa roho ni maisha ya kweli.

Roho Mtakatifu anaeleta maelewano ndani na nje kati ya watu

Roho Mtakatifu haleti maelewano tu ndani, bali hata nje, kati ya watu. Hii anaileza vizuri Mtakatifu Paulo akizungumzia juu ya Kanisa na kurudia kusema mara nyingi  juu ya “ tofauti” . Kuna karama tofauti, karama za shughuli na huduma tofauti (1Kor 12, 4-6). Sisi ni tofauti  katika ubora na wa zawadi, Roho anagawanya kwa njia ya ubunifu na kufurahisha, bila kufanisha. Na kutokana na utofauti huo anajenga umoja. Alifanya hivyo tangu uumbaji kwa sababu ni mtaalam katika kubadili mchangamano wa ulimwengu na kuweka katika maelewano. Leo hii dunia kuna ukosefu wa maelewano na kumegeuka mgawanyiko wa kweli. Kuna walio na vingi zaidi, na wasio kuwa na kitu. Kuna yule anayetafuta aishi miaka 100, kuna mwingine ambaye hawezi kuzaliwa katika mwanga wa jua. Katika nyakati za Computa, Baba Mtakatifu anathibitisha, wapo zaidi wanaiishi kwa umbali zaidi kwenye  mitandao badala ya kuishi katika  kijamii ya kweli .

Kuna haja Roho wa umoja ili tupyaishe tena kama Kanisa, kama watu wa Mungu na kama udugu wa kibinadamu. Daima kuna kishawishi cha kutaka kujenga viota na kujizungushia ndani ya kikundi binafsi, katika upendeleo binafsi, ufananisho bila kuchangamana na wengine. Ni kutoka katika kiota hadi kufikia kuibuka kwa dunia nyingine katika hatua fupi. Ni mara ngapi wanajieleza utambulisho wake dhidi ya mtu au dhidi ya kitu! Roho Mtakatifu badala yake anaunganisha walio mbali anawaleta pamoja wale waliopotea, anapoteza ndani mwake sauti tofauti na kuifanya katika umoja wa maelewano kwa sababu  yeye anaona wema zaidi na kutazama mtu kabla ya makosa yake, aidha  watu kabla ya matendo yao.

Roho anaumba kanisa na dunia kama sehemu ya wana na ndugu

Akiendelea na mahubiri yake Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa, kwa sasa kumekuwa na mtindo wa kutukanana. Na baadaye tunatambua kuwa inaumiza na kushutukia kuwa wathirika hawaishi tena vizuri. Anaye ishi kwa mujibu wa Roho badala yake analeta amani mahali pasipo na mapatano na maelewano palipo na migogoro. Watu wa kiroho wanatambua mema dhidi ya mabaya na hawajibu vibaya bali kwa upole hata wakati wa ukatili kwa wema, kielele kwa ukimya, masengenyo kwa sala na tabasamu mbele ya kusingiziwa. Aidha amebainisha hasivyo pendelea utamaduni wa kisasa wa kutukanana. Ili kuweza kuwa mtu wa kiroho na kuonja maelewano ya Roho inahitaji kujiweka katika mtazamo wake Mungu mbele yetu. Kwa njia hiyo mambo yanabadilika. Kwa njia ya Roho, Kanisa ni watu wa watakatifu wa Mungu, utume unaambukiza furaha kwa kaka na dada wapendwa wa Mungu mmoja. Bila Roho Kanisa ni kama chama chochote cha utume wa kipropaganda, umoja ni jitihada! Roho ndiyo mahitaji ya kwanza na ya mwisho wa Kanisa.

Kwa kuhitimisha na kuomba Roho Mtakatifu atujalie kuwa na maelewano

Baba Mtakatifu Francisko baada ya kukumbusha aliyosema amehitimisha akiomba tusali kila siku ili Roho Mtakatifu atuwezeshe kuwa na maelewano ya Mungu: Wewe unayebadili hofu na kuwa imani na kufungua kuwa zawadi, njoo kwetu. Utupatie furaha ya ufufuko na ujana wa moyo ya  milele. Roho Mtakatifu,maelewano yetu, Wewe unayefanya ndani mwetu mwili mmoja tujaze amani yako katika Kanisa na katika dunia. Tuwe wajenzi wa mapatano, wapanzi wa wema na mitume wa matumaini.

 

09 June 2019, 13:17