Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kurejea mjini Roma, amekwenda moja kwa moja kumshukuru Bikira Maria kwa ulinzi na tunza yake ya kimama! Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kurejea mjini Roma, amekwenda moja kwa moja kumshukuru Bikira Maria kwa ulinzi na tunza yake ya kimama!  (ANSA)

Hija ya Kitume Romania: Shukrani ulinzi na tunza ya B. Maria!

Baba Mtakatifu Francisko baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume nchini Romania, akiwa njiani amewatumia Marais na wakuu wa nchi ambazo amepita juu yake, akiwatakia heri, baraka, ustawi, amani na maendeleo fungamani kwa wananchi wao. Alipowasili mjini Roma, amekwenda moja kwa moja kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria Mkuu, kumshukuru B. Maria kwa ulinzi na tunza yake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha hija ya 30 ya kitume kimataifa nchini Romania ilioanza tarehe 31 Mei hadi 2 Juni 2019 iliyokuwa inaongozwa na kauli mbiu “Twende pamoja” ili kujenga na kudumisha umoja na mshikamano wa kitaifa; kwa kufuata nyayo za mashuhuda wa imani, waliomimina maisha yao kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake! Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kutoka Romania kurejea mjini Vatican, Jumapili jioni tarehe 2 Juni 2019, amemtumia ujumbe wa matashi mema, heri na baraka Rais Klaus Werner Iohannis wa Romania ili kumshukuru kwa ukarimu na mapokezi makubwa waliyompatia wakati wa hija yake ya kitume.

Baba Mtakatifu akiwa kwenye anga la nchi ya Serbia,  Bosnia Herzegovina, Croatia na Montenegro ametuma salam na ujumbe wa matashi mema akiwaombea na kuwatakia mema, ustawi na maendeleo na baraka kwa wananchi wao. Akiwa kwenye anga la Italia, Baba Mtakatifu amemwambia Rais Sergio Mattarella wa Italia kwamba, alikuwa anarejea kutoka katika hija yake ya kitume, iliyomwezesha kutembelea Romania na kwamba, alikuwa anawapatia baraka zake za kitume, wananchi wote wa Italia. Baba Mtakatifu alipowasili mjini Roma kwenye Uwanja wa Ciampino, majira ya saa 12:11 za jioni, alikwenda moja kwa moja kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria Mkuu, kutoa shukrani zake za dhati kwa ulinzi na tunza ya Bikira Maria, “Salus Populi Romani” yaani Bikira Maria, Afya ya Warumi!

Papa: Salus Popoli
03 June 2019, 11:47