Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amekutana na Shirikisho la Kimataifa la Madaktari katoliki na kuwahimiza kuwa tabibu kwa mfano wa Yesu! Papa Francisko amekutana na Shirikisho la Kimataifa la Madaktari katoliki na kuwahimiza kuwa tabibu kwa mfano wa Yesu!  (Vatican Media)

Papa Francisko:Madaktari ni wahudumu wa maisha kuanzia mwanzo hadi mwisho!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Madaktari Katoliki,kwa kuwakilishwa na kikundi cha watu karibia 500.Kwao amependekeza mtindo wa Yesu tabibu na mtindo wake wa kukaribia wagonjwa kwa ajili ya kuwaponesha mwili na roho!Kuponya ni mwanzo wa safari ya kutuliza,ya kufariji,ya kupatanisha na kuponya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 22 Juni 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Madaktari Katoliki mjini Vatican. Mara baada ya salam kwa Kardinali Peter Turkison, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu, ametoa pongezi kwa tendo la kujitoa wakfu walilofanya wanachama hao kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu. Na baadaye kuwashirikisha baadhi ya tafakari kunzia na mtazamo ambao mara nyingi unafafanuliwa kikristo uliokuwa unawakilishwa na Yesu kama “tabibu” wa  kuweka umakini na huruma kwa wale wote walio kuwa wanateseka kwa sababu ya ugonjwa.

Ukaribu wa Yesu kwa wahitaji na masikini zaidi

Yesu alikuwa anawakaribia watu wagonjwa na walemavu hasa wale ambao kutokana na hiyo walikuwa wanadharauliwa na kubaguliwa. Yeye alikuwa anashutumu vikali wale waliokuwa wanawahukumu wagonjwa, na kama  wadhambi na ukaribu wake ulikuwa unaonesha upendo usio na kikomo wa Mungu Baba kwa watoto wake wenye kuhitaji.  Kwa hiyo, huduma ya wagonjwa inaonekana kama moja ya vipimo vya utume wa Kristo; na kwa sababu hii imebaki vile vile hata  katika Kanisa lile.Katika Injili inaonesha wazi uhusiano kati ya kuhubiri kwake Yes una ishara za uponyaji  alizokuwa anatimiza kwa wale waliokuwa wanateswa na magonjwa na maumivu mbalimbali,kama vile  pepo, kifafa na kupooza (Mt 4,24)..

Kutibu maana yake ni kuingia uhusiano na mtu

Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kwa namna gani Yeus alikuwa anatibu wagonjwa na wanaoteseka. Alikuwa anawagusa na kuacha aguswe, hata katika kesi nyingine ambayo ilikuwa ahiruhusiwi. Kwa ke yeye kutibu maana yake ni kukaribia mtu na hata kufikia kuuliza anataka nini afanye kwa ajili yake. Inawezekana kushangaza kuwa daktari anaomba mtu anayeteseka ni kitu gani anasubiri kwake. Lakini hali hiyo inaweka mwanga ulio wazi wa thamani ya neno na majadiliano katika uhusiano wa tiba. Kutibu kwa mujibu wa Yesu maana yake ni kuingia katika majadilino ili kuweza kukuza ile shauku  ya kuwa binadamu na utamu wa nguvu ya upendo wa Mungu inayojionesha katika Mwanaye. Na hiyo ni kusema kutibu maana yake ni kutoa mwanzo wa safari, safari ya kutuliza, ya kufariji, ya kupatanisha na kuponya.

Umakini, tahadhari na heshima kwa mgonjwa

Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena anabainisha ni kwa  jinsi gani  Yesu kamwe hukuponya sehemu moja tu, lakini mtu mzima, umoja wa roho, roho na mwili, na ili kumponya kwa ukamilifu. Tiba yake inamwamsha mtu n amara nyingi anamtuma, ni watu wengi ambao mara baada ya kupona, wamegeuka kuwa wanafunzi wake. Kwa wote yeye anaimarisha uhusiano binafsi wa wenye utajiri, huso siyo wa kimitambo anasema Baba Mrakatifu na wale sio wa mbali! Na ndiyo hii shule ya Yesu kwa daktari na ndugu wa wanaoteseka na ambao wao wanaitwa kuwa madaktari waamifu ndani yake, wanachama wa Kanisa lake. Kuitwa  ili kuweza kuwa karibu na wale ambao wanakabiliwa na kipindi cha majaribiu kwa sababu ya ugonjwa. Wanaitwa watoe tiba kwa makini na heshima ya hadhi na ufungamanisho wa kimwili na wa akili za watu. Wao wanaitwa  kusikiliza kwa uangalifu, kujibu kwa maneno yanyaotsheleza na ambayo yanaambatana na ishara ya utunzaji kwa kuwafanya inayowafanya kuwa wanadamu zaidi na namna hivyo pia inafaa zaidi.

Daktari ni mtumishi siyo bwana wa maisha

Baba Mtakatifu amewambia kwamba wamadaktari wanaitwa kutoa matumanini na matumaini yanayotoka kwa Mungiu hata wale ambao wanafanya kazi katika utafiti wa kidaktari na ambao wanapongezwa. Zaidi ya miaka mia iliyopita, maendeleo yamekuwa makubwa sana. Kuna tiba mpya na matibabu mengi yamefanyiwa utafiti na majaribio. Tiba hizi zote hazikufikiriwa katika vizazi vilivyopita. Tunaweza na lazima kupunguza mateso na kuelimisha kila mtu kuwa na wajibu zaidi kwa ajili ya  afya zao binafsi  na afya za majirani na ndugu wengine. Lazima pia tukumbuke kwamba uponyaji ina maana ya kuheshimu zawadi ya uzima tangu mwanzo hadi mwisho. Sisi si wamiliki wa  uhai bali sisi tumekabidhiwa maiosha na madaktari ni watumishi wake.

Kutokana na Roho Mtakatifu kuna zawadi ya mang’amuzi

Baba Mtakatifu Francisko amewaelezea kuwa utume wao ni muhimu sana wa kuwanya wahisi kuwa Mungu ni Baba yetu, ina maana ya kika mmoja ana  maisha na upendo. Kila daktari mkatoliki anapaswa kuwa  na taaluma uvumilivu, nguvu ya kiroho na mshikamano kidugu, na zaidi taalam , uwezo wa kushirikiana na udhati wa kimaadili . na hatimaye Baba Mtakatifu Francisko amewashaui wachote kutoa Neno la Mungu na Sakramenti na Roho Mtakatifu  ambaye anawapatia zawadi ya kufanya mang’amuzi kwa ajili ya kukuabiliana na hali halisinyeti na ngumu ya kusema maneno wakati unao faa, kuwa kimya cha haki wakati unaofaa.

22 June 2019, 14:21