Tafuta

Baba Mtakatifu amekutana na ndugu wadogo wa wakonventuali wakiwa katika fursa ya Mkutano wao Mkuu Baba Mtakatifu amekutana na ndugu wadogo wa wakonventuali wakiwa katika fursa ya Mkutano wao Mkuu 

Papa Francisko:lazima kushinda mantiki ya mafanikio ili kujenga amani!

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 17 Juni 2019 amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la ndugu wadogo wakonventuali na kuhimiza wawe wahudumu wa huruma,zaidi ameonesha umuhimu wa kusikiliza Injili na zawadi ya undugu.Amehimiza wawe watumishi kwa ajili ya kuwasindikiza wengine katika njia zinazo elekeza kwa Mungu na kwa kufanya hivyo itasaidia kuzuia bujiko la wengi wanaoacha maisha ya kikuhani na utawa.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 17 Juni 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika ndugu wadogo Wakonvetuali wa Mtakatifu Francisko a Assisi. Anamshukuru Mkuu wa Shirika mpya aliyechuguliwa Ndugu mgogo Carlos Trovarelli na kuwapongeza waliomchagua. Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa hivi karibuni Vatican imeridhia Katiba yao ya upyaisho wa Mkutano Mkuu maalum wa kiangazi kilichopita. Kwa kutambua upyaisho huo, kwa sasa wamejadili na kukubaliana na Kanuni mpya ambazo zinagusa baadhi ya mambo msingi ya udugu wao na umisionari ambao unajikita katika mafunzo, tamaduni nyingi, ushirikishwaji na uwazi katika uendeshaji kiuchumi. Hiyo ni kazi ngumu anasema Baba Mtakatifu lakini ugumu unafanyika vizuri! Katiba kwa hakika ni zana muhimu kwa ajili ya kuhifadhi urithi wa karama ya Taasisi na kuhakikisha uenezaji wa utume kwa wakati ujao.

Katiba inaelezea mtindo na namna ya kufuasa Kristo

Katiba kwa hakika inaelezea mtindo wa dhati wa  kumfuasia Kristo kwa njia ya mapendekezo  ya Injili, kanuni msingi wa maisha ya watawa wote kwa namna ya pekee wafuasi wa Mtakatifu Francisko wa Assisi, ambapo kwa kufunga  nadhiri, wanawajibika kuishi kwa mujibu wa mtindo wa Injili Takatifu (rej. barua ya 14 ya  Mtakatifu Francisko wa Assisi). Iwapo kila maisha ya wakristo yanazaliwa kutokana na kusikiliza Neno la Mungu na kukaribisha Injili kama kanuni ya Maisha (Soma Sinodi ya Maaskofu kuhusu Neno la Mungu, propositio 24), katika   maisha ya kifransikani na maonesho yake yote, yanazaliwa kwa njia ya kusikiliza Injili Takatifu kama anavyoonesha masikini akiwa katika  Kanisa dogo (Porziuncola), mara baada ya kusikiliza neno kuhusu ufuasi alisema: “ shemu hiyo ndiyo ninataka, ndiyo ninaomba iwe katika moyo wangu wote” (soma, Tomaso da Celano, Maisha ya kwanza, IX, 22).

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua zaidi juu ya  kanuni ya maisha yao anasema  ni udogo. Huo ndiyo uchaguzi mgumu kwa sababu unakwenda kinyume na mantiki ya dunia ya sasa ambayo inatafuta kujiulikana kwa kila gharama, kutamani kuchukua nafasi za kwanza, kufikiria kuwa kama bwana. Mtakatifu Francisko wa Asisi aliomba kuwa mdogo ka mfano wa Yesu ambaye hakuja kutumikiwa, bali kutumikia (Mt 20,27-28) na Yesu anatueleza: “anayetaka kuwa mkubwa kati yenu na awe mtumishi na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu  awe mtumishi wa wote (Mk 10,43-44). Ka maana hiyo anawashauri kwamba hili ndilo liwe shauku ya kuwa watumishi, ili kuhudumiana mmoja na mwingine. Kwa kuishi namna hii, ndipo unabii utaweza kutimizwa katika dunia hii, mahali ambapo kishawishi cha madaraka ni kikubwa sana, amesisitiza Baba Mtakatifu  

Hubirini kwa amani kama salam inayo watofautisha “Shalom we tob”

Baba Mtakatifu akiendela na hotuba yake anawashauri wahubiri kwa amani. Katika salam ya kifaransiskani inawatofautisha wakisalimiana,  “amani na salama” yaani “shalom we tob” katika lugha ya kihebrania na ambayo anasema, tunaweza kuitafisri na mapatano. Kijipatanisha wewe binafsi, Mungu na wengina na kazi ya uumbaji. Ni mapatano ambayo yanatafuta kuwa sehemu ya moyo na kutanda katika ulimwengu wote, lakini kwa hakika ni kutoka katika sehemu ya Moyo wa Mungu na katika moyo wa Kristo. Mapatano ni mwanga wa amani ambao Yesu mwenyewe alituachia, (rej, Yh 14,27). Amani ambayo haimanishi kutokuwa na matatizo, bali itokanayo na uwepo hai wa Mungu ndani mwetu na kujionesha yote kwa kile ambacho sisi tunatenda na kusema. Baba Mtakatifu amesema kuwa, wao wanaweza kuwa wajumbe wa amani zaidi ya yote katika maisha na kwa maneno. Kila wakati wanaweza kuwa chombo cha msamaha na huruma. Maisha yao katika jumuiya yawe mahali ambamo wanafanya uzoefu wa huruma, kama anavyoomba Mtakatifu Francis katika barua yake kwa makuhani: “Katika hili ninataka kujua kama wewe unampenda Bwana na mimi mtumishi wake na wako, iwapo unakwenda kadiri ya matakwa yake yaani pasiwepo na frateli yoyote duniani mwenye dhambi  na iwapo atatetenda dhambi  machoni pako hasirudi bila kuwa na msamaha iwapo atakuomba; na iwapo ataomba msamaha, basi wewe muulize kama anataka kusamehewa. Na hata kama atakosea mara elfu, mbele ya macho yako, mpende zaidi yangu na ndiyo wewe unaweza kumpeleka kwa Bwana; uwe mwenye huruma kwa ndugu kama hao (Barua ya mtakatifu Francis kwa mafrateli 9-11)”. Baba Mtakatifu  Francisko ameongeza kusema “hakuna amani bila mapatano, na bila mapatano hakuna huruma.  Ni kwa yule tu aliyejipatanisha anaweza kuwa mhudumu wa huruma na mjenzi wa amani”.

Mafunzo yanayostahili katika mchakato wa kumfuasa Kristo

Na kwa yote hayo ni lazima kuwa na mafunzo yanayo stahili. Ni mchakato wa safari ya mafunzo ambayo yanakuza ule urahisi wa ndugu ulio mkamilfu wa mafunzo ya Kristo. Ni mafunzo fungamani ambayo yanakita mantiki zote za binadamu. Ni mafunzo binafsi na ya kudumu kama mchakato unaodumu maisha yote. Ni mafunzo ya moyo ambayo yanabadili namna ya kufikiri, kuhisi na mwenendo. Ni mafunzo ya imani, kwa kutambua leo hii tunavyoishi katika utamaduni wa mpito ambapo uksema ndiyo ya kudumu inakuwa ni ngumu sana na zaidi kuwa na uchaguzi wa mwisho ni kama kusema umepitwa na wakati.

Katika mantiki hiyo, Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa ni lazima walimu wawe na msimamo na wewe wataalam wa kusikiliza na kuwa na  njia ambazo zinaelekeza kwa Mungu na kuwa  wasindikizaji wa wengine katika mchakato wa safari hiyo (Rej, Mtakatifu Yohane II,Wosia kuhusu maisha ya watawa,65-66); kuwa walimu ambao wanatambua sanaa ya mang’amuzi na kusindikiza. Ni kwa njia hiyo tunaweza kutunza angalau sehemu ya bubuko la kuacha maisha ya ukuhani na utawa.  Na kwa kuhitimisha amewabariki kwa baraka ya kitume wao na jumuiya zao. Anasali kwa ajili yao na kuwaomba pia wasali kwa ajili yake .

 

17 June 2019, 14:20