Tafuta

CHARIS - Chombo cha huduma ya Chama cha Wakarismatiki Wakatoliki ( Catholic Charismatic Renewal International Service) kinafunguliwa rasmi katika Sikukuu ya Pentekoste 9 Juni 2019 CHARIS - Chombo cha huduma ya Chama cha Wakarismatiki Wakatoliki ( Catholic Charismatic Renewal International Service) kinafunguliwa rasmi katika Sikukuu ya Pentekoste 9 Juni 2019 

Papa Francisko kwa wakarisimatiki awaomba waungane katika Roho Mtakatifu kwa ajili ya Kanisa!

Baba Mtakatifu alipokutana na mjini Vatican tarehe 8 Juni 2019 na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa viongozi wa Upyaisho wa Wakaristimatiki Katoliki kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa CHARIS hapo Juni 9 ambayo ni hudma mpya kwa mujibu wa Baba Mtakatifu,amewahimiza kutoa ushuhuda wa upendo utokanao na nguvu ya Roho Mtakatifu na huduma si kutawala bali ni kuhudumia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 8 Juni 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa  CHARIS (Catholic Charismatic Renewal International Service- Charis) ambacho ni kitengo kinachosimamia na kuratibu shughuli za Chama cha Wakarismatiki Wakatoliki. CHARIS inazinduliwa rasmi wakati wa Sherehe ya Pentekoste, Jumapili tarehe 9 Juni 2019.  Katika kuanzisha chombo cha CHARIS ina maana kuwa Chama cha Udugu wa Kikatoliki na Huduma ya Uhamsho wa Kikatoliki Kimataifa, (ICCRS)  vilivyokuwa vinajulikana namna hiyo vinafungwa na kuwa na huduma moja  ambayo ni mwanzo mpya wa chombo kimoja cha Wakarismatiki Wakatoliki. Katika hotuba ya Baba Mtakatifu ameanza kusema: Wapendwa mimi ninapenda kama baadhi ya watu wanavyo salimiana katika kipindi cha Pasaka, kwani hawasemi, habari za Asubuhi, au za jioni, wanasema Yesu amefufuka. Wanasalimiana hivyo kwa pamoja Yesu… na wote wanajibu “amefufuka. Ndiyo Yesu anaishi! Asante kwa maana sasa mnatambua kuwa ninapenda hivyo na  wimbo ambao mmeimba wakati wa kuingia!

Miaka 52 iliyopita ilianzishwa karisimatiki

Katika Sikukuu hii ya Pentekoste inaanza na kipindi kipya cha safari iliyoanzishwa na upyaisho wa karismatiki miaka 52 iliyopita. Upyaisho wa Karismatiki umeendelea katika Kanisa kwa mapenzi ya Mungu ambayo kwa maneno ya Mtakatifu Paulo VI alisema “ni fursa kwa ajili ya Kanisa ( hotuba kwa washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Upyaisho wa karisimatiki katoliki 19 Mei 1975 ,Pentekoste). Baba Mtakatifu anawashukuru kwa jina la Kanisa  chama cha Huduma ya Uhamsho wa Kikatoliki Kimataifa, (ICCRS) na Chama cha Udugu wa Kikatoliki kwa ajili ya utume uliofanyika kwa miaka 30. Baba Mtakatifu Francisko anasema, leo hii ninyi mmeanza njia na kuwawezesha,katika njia ya  uaminifu ambao CHARIS leo  hii ni hali halisi. Asante! Anawashukuru hata  kikundi cha watu wanne ambao wamekabidhiwa kutimiza huduma hii mpya kuwa moja, ambayo ni Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha wakiongozwa na Rais wao Kardinali Farrell ambaye amewasindikiza. Baba Mtakatifu Francisko amesema: “Leo hii inaisha jambo moja na kuanza jingine. Hatua mpya inaanza katika safari hii. Hatua ambayo inajikita katika muungano kati ya wajumbe wa familia ya kikarisimatiki, mahali ambamo wanaonesha uwepo wa nguvu wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya wema wa Kanisa lote; Na mahali ambamo katika uwepo huo unawafanya kuwa sawa kila mtu. Kwa sababu wote na kila mtu wamezaliwa na Roho hiyo; wakubwa na wadogo, matajiri wa miaka na waliozaliwa sasa hivi, kujikita kwa ngazi ya kidunia na zaidi kila mahali kwa kuunda  kila kitu na ambacho ni kikuu kwa yote.

Mpya

Huduma mpya ya kipekee na ya umoja:Tunakwenda kuelekea umoja na ndiyo njia ya Roho. Baba Mtakatifu  Francisko akifafanua juu ya neno mpya anakumbusha kuwa, kama alivyokuwa amesema mwaka jana, mpya inaweza kudhoofisha. Mwanzo kuna hisia za kutokuwa na uhakika hasa wa mabadiliko yanayoweza kuletwa na mapya.  “Wakati mwingine mmoja anapendelea abaki jinsi alivyo kwa kujitenge na  umoja. Hiki ni kishawishi cha shetani. Kila mara mmoja anahisi kutaka kilicho chake na kukataa cha mwingine, au mimi ninapendelea ya kizamani na mapya siyataki, lakini hapo ndipo kuna shetani kwa sababu ananitenganisha na umoja”, Baba Mtakatifu amebainisha. Hata hivyo anasema, huo ni ubinadamu kuwa na hofu ya mapya, lakini siyo kesi ya mtu wa kiroho kwa maana: “ninafanya mambo yote mapya”, anasema Bwana katika Kitabu cha Ufunuo 21, 5. Lakini Mungu wetu ni Mungu wa mambo mapya. Mambo mapya ya Mungu daima ni baraka, kwa sababu yanafuata upendo wake. Japokuwa daima  kuna kishawishi cha kusema: “ tupo tunaishi hivi vizuri , mambo yanakwenda vizuri na kwa nini kubadili? Tuache jinsi ilivyo kwa maana tunajua jinsi tunavyofanya”. Mawazo ya namna hiyo  Baba Mtakatifu Francisko anabainisha  hayatokani na Roho, hata kwa kusema kutoka kwa Roho Mtakatifu, labda ni kutoka katika roho ya dunia… Kutokana na hivyo, amewahimiza kwamba “ msiangukie katika makosa hayo”, kwa maana “ Ninafanya mambo yote kuwa mapya”, anasema Bwana.

Ya kipekee

Baba Mtakatifu Francisko  akiendelea na ufafanuzi juu ya upekee, anasema, ni huduma moja ya kipekee kwa ajili ya hali halisi ya karismatiki ambayo Roho ameiweka katika dunia. Siyo kiungo ambacho kinahudumia baadhi ya hali halisi, yaani kiungo kingine ambacho kinahudumia hali nyingine na ya tatu na kuendelea. Vile vile amefafanua juu ya huduma kwamba: huduma si kutawala, bali ni kuhudumia. Akitoa mfano amesema kwamba wakati mwingine inatoka katika vyama vya kibinadamu, viwe vya kilei au kidini, kuwa na kishawishi cha kuependelea daima kutafuta faida binafsi; Tabia ya kutaka kuonekana, kuongoza  na fedha; na  mara nyingi namna hii inatokea. Hapa rushwa inaingia namna hii au hapana? Ameulizwa…..Huduma daima ni huduma. Kutoa huduma haina maana ya kupata faida anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Shetani anaingia mifukoni. Huduma maana yake ni kutoa!

Muungano 

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua juu ya muungano amesema wote kwa roho moja unaotazama Baba ili kuweza kutoa ushuhuda wa umoja katika utofauti. Utofauti wa karama ambao Roho amezewesha kwa miaka hii 52. Kuongeza kamba za hema kama anavyosema Isaya (taz 54 2), kwa sababu wanaweza kukaa watu wote kama familia moja. Katika familia ambamo yupo Mungu Baba, Bwana Yesu Kristo peke yake na Roho anayepyaisha. Katika familia ambamo wajumbe waliomo siyo tu muhimu zaidi ya mwingine, kunzia na umri, au akili na walio na uwezo, kwa sababu wote ni wana wapenda wa Mungu mmoja. Mfano wa mwili ambao Mtakatifu Paulo anasema, una maana hiyo (taz. 1 Wakorinto 12,12-26).

Vijana wawakilishi katika huduma ya kimataifa

Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa, “katika Huduma ya Kimataifa ya Muungano, kuna vijana wawakilishi. Hili linanipa furaha!" Vijana ni wakati uliopo na wakati endelevu wa Kanisa. Ninayo furaha ya kwamba wamewapatia mwonekano wao na zoezi la uwajibikaji ambao unawahusu, kuwaona wapo kwa macho na kuwatazama wakati wao endelevu.Aidhaameelezea kwamba ametambua  kuwa “CHARIS tangu leo hii anayo haki ya kutangaza hata Hati za Malines. “Rais amenizawadia nakala moja ya lugha ya kisipanyola, asante! Hata hivyo amenongeza kusema: “Ni jambo jema. Jitahidi ziweze kufahamika! Nimewapatia fursa nyingi ambazo zipo katika Hati ya kuwasindikiza katika siku hii ya neema”.

Papa na kanisa wanategemea nini katika hduma ya CHARIS?

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake amesema: “Mmeniomba kuwaeleza ni kitu gani Papa na Kanisa wanasubiri katika Huduma mpya kutoka Charis na Upyaisho mzima wa Karisimatiki”. Kwanza iweze kushirikisha Ubatizo katika Roho Mtakatifu na watu wote wa Kanisa. Ni neema ambayo ninyi mmeipokea: Ishirikisheni na siyo kujitunzia binafsi. Pili: iweze kuhudumia muungano wa Mwili wa Kristo ambao ni Kanisa, jumuiya ya waamini katika Yesu Kristo na Bwana. Hii ni muhimu sana kwa sababu Roho Mtakatifu ndiye anayefanya umoja wa Kanisa lakini pia hata anayefanya utofauti.Ubinadamu wa Roho Mtakatifu ni wa kushangaza anasema Baba Mtakatifu. Yeye hufanya tofauti nyingi zaidi za karama, lakini pia  hufanya hata kama hivi  kwa maelewano na hatimaye hupatikana  umoja huo. Kwa sababu, kama asemavyo Mtakatifu Bazil kwamba:“Roho Mtakatifu ni umoja” ambaye anatoa maelewano, katika Utatu, pia hata kwetu sisi”

Na tatu ili  iweze kuhudumia masikini, wenye kuhitaji zaidi kwa kila mahitaji ya  kiroho na kimwili. Hii haina maana kama wengine wanaweza kufikiria: hivi Upyaisho huu sasa umefanya Comunisti? Hapana umeundwa kiinjili na  hiyo ipo katika Injili” amebainisha Baba Mtakatifu Francisko. Mambo hayo matatu: Ubatizo katika Roho Mtakatifu, umoja wa Mwili wa Kristo na Huduma kwa masikini ndiyo ushuhuda muhimu kwa ajili ya unjilishaji duniani na ambapo wote tunaalikwa kwa ajili ya ubatizo wetu. Unjilishi ambao siyo propaganda, bali msingi wake ni ushuhuda. Kushuhudia upendo kwa maana,  “tazameni jinsi wanavyo pendana” ndiyo  ulikuwa mtazamo wa makini ulioneshwa kwa wote waliokutana na wakristo wa kwanza. “Tazameni kama wapendanavyo” .  Ha hivyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba “mara nyingine katika jumuiya nyingi wanaweza kusema, tazama jinsi gani wanavyo sengenya! Hii siyo Roho Mtakatifu. Bali ni “Tazama jinsi gani wanavyopendana”.

Kuinjilisha ni kupenda

Kushirikishana upendo wa Mungu kwa kila binadamu, kwa maana inawezakana kuunda vyama vya unjilishaji, wanaweza kutengeneza mipango ya ubunifu na kutafiti kwa makini. Lakini kama hakuna upendo, kama hakuna jumuiya  haisaidii kitu.  “Bali ni Tazameni jinsi wanavyopendana”. Hii ndiyo Jumuiya. Katika  barua ya Pili ya Yohane kuna onyo sura ya 9 isemayo kuweni makini na wale  ambao wanazunguka hapa na pale katika jumuiya hawana roho nzuri. Labda mwingine anaweza kuwa na kishawishi cha kusema labda tusifanye chama kama hiki…  Tutengeneza jumba la namna hii au lile… Na wote pale… Lakini kabla ya yote ni upendo. Katika itikadi za mawazo na mitindo ya namna hiyo ni kuzidisha kipimo cha jumuiya, anasema Yohane “hiyo ndiyo roho ya dunia na siyo roho ya Mungu, “tazameni jinsi gani wanavyopendana”. Upyaisho wa Karismatiki ni tukio la neema ya Roho Mtakatifu, na hivyo wawe mashuhud wa upendo huo.

Baba Mtakatifu Francisko amependa kusali dk 25 kabla ya muda wa ajili ya wito wa sala ambayo leo hii Kanisa zima  limealikwa kusali kwa kukaa  kimya ya sala kwa ajili ya amani. Kwa sababu gani? Leo hii ni tukio  kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu marais wa Serikali ya Palestina na Israeli walipokutana mjini Vatican. Walisali pamoja kwa ajili ya amani na kwa  njia hiyo leo hii duniani kote wanasali saa 7 Mchana kwa ukimya. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesali nao na kuwashukuru kwamba.”Asante kwa kuwa na  Jumuiya iliyopishwa na sura ya ukimya, ndiyo ushujaaa! Asante…( wote wamecheka ) na kuwabariki, wakati huo huo akiomba wasali kwa ajili yake.

08 June 2019, 14:51