Tafuta

Mkesha wa Pentekoste mjini Vatican tarehe 8 Juni 2019 Mkesha wa Pentekoste mjini Vatican tarehe 8 Juni 2019 

Mkesha wa Pentekoste:Papa anatoa wito kwa mji wa Roma na miji kuwa na ukarimu kama mama mzazi!

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika mkesha wa Pentekoste tarehe 8 Juni 2019 katika uwanja wa Mtakatifu Petro anajikita kutazama kilio na kwikwi za watu na hasa kwa kuutaja mji wa Roma ambao anaomba uwe na ukarimu kama wa Mama mzazi anayetambua kuwapokea watoto wake.Ili kuweza kusikiliza kilio cha mji wa Roma,amebainisha wote tunahitaji Bwana aweze kutushika mkono na kutufanya “tushuke” katikati ya ndugu wanaoishi katika mji wetu,kuwasikiliza mahitaji yao ya wokovu,kilio ambacho bado kinamfikia Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu ametoa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko  kwa kukazia juu ya kilio cha watu katika miji na hasa mji wa Roma wakati wa Misa ya Mkesha wa Pentekoste tarehe 8 Juni 2019 katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vaticani kwa waamini kutoka sehemu mbali mbali za dunia na zaidi wakiwa  ni washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa muungano wanakarisimatiki kutoka duniani kote. Na hii ni  katika harakati ya ufunguzi rasmi wa CHARIS ambacho ni kitengo kinachosimamia na kuratibu shughuli za Chama cha Wakarismatiki Wakatoliki. Baba Mtakatifu Francisko amesema: “Hata jioni hii ni mkesha wa siku ya mwisho ya kipindi cha Pasaka, sikukuu ya Pentekoste, Yesu yupo kati yetu na anatangaza kwa sauti kubwa kuwa mtu aonaye kiu na aje kwangu anywe na  kama vile maandiko yalivyonena, “mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. (Yh 7, 37-38). Ni mito ya maji hayo ya Roho Mtakatifu inayotoka katika Umbu la Yesu, kutoka katika ubavu wake uliochomwa na mkuki (Yh 19, 36) na ambao unaosha na kuzaa Kanisa,mchumba wake anayewakilishwa na Maria, Eva mpya chini ya miguu ya msalaba.

Wito wa mji wa Roma kulitambua Kanisa la makaribisho, kama nyumba ya mama mzazi

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri yake anasema Roho Mtakatifu anabubujika kutoka katika umbu la huduma ya Yesu mfufuka na kujaza umbu letu kwa kiasi kizuri kilichoshindiliwa na kusukwa sukwa hata kumwagika cha huruma (Lk 6,38) na kubadili Umbu la Kanisa ya huruma yaani  la mama mwenye moyo ulio wazi kwa wote! Hapa Baba Mtakatifu ametoa angalisho kuwa:  “Ni kwa jinsi gani ninataka watu wanaoishi Roma waweze kujua Kanisa, kujua zaidi huruma hiyo na zaidi hii  ya ubinadamu na huruma, ambapo kuna mahitaji mengi!  Wangehisi kama nyumba, “nyumba ya mama mzazi ”, mahali ambapo daima pamekuwa mahali pa makaribisho na mahali ambapo daima unahisi kurudi tena. Wangehisi kupokelewa, kusikilizwa, kutafsiriwa vema na kusaidiwa ili kupiga  hatua ya kwenda mbele katika mwelekeo wa ufalme wa Mungu.

Wazo hili  la uzazi wa Kanisa Baba Mtakatifu amesema linafanya  akumbuke miaka 75 iliyopita ya tarehe 11 Juni 1944, ambapo Papa Pio XII  anasema, alifanya tukio moja maalum la kushukuru na kuomba Bikira kwa ajili ya kulinda mji wa Roma. Alifanya hivyo katika Kanisa la Mtakatifu Ignatius, mahali mbapo walikuwa wamepeleka Picha ya Mama Maria wa Upendo wa Mungu. Upendo wa Mungu ni Roho Mtakatifu, ambaye anabubujika katika moyo wa Kristo. Yeye ni “mwamba wa kiroho“ anayesindikiza watu wa Mungu katika jangwa, kwa sababu katika kuchota miji hai waweza kumaliza kiu ya muda mrefu katika safari (Wakor 10,4). Katika kichaka kisicho ungua, sura ya Bikira Maria na Mama wa Kristo Mfufuka ambaye anazungumza nasi  na kutuhabarisha na moto wa Roho Mtakatifu, anatualika kushuka katikati ya watu ili kuwasilikiza kilio chao, anatualika kufungua mipaka ili kutembea kwa uhuru ili kufika  katika nchi ya ahadi ya Mungu.

Hata leo hii wapo wanaotafuta kujenga mnara wa  ili kufika mwisho wa mbingu

Baba Mtakatifu Fracisko amesema kuwa:Tunatambua hata leo hii kama ilivyo kwa kila nyakati kuna anayateka kujenga mji na manara  wa kufika mbinguni,  (taz Mw, 11,4). Ni mipango ya kibinadamu, hata mipango yetu  inayofanywa  kwa “mimi” na  daima ni kubwa kuelekea katika mbingu mahali ambamo hakuna nafasi  kwa ajili ya Mungu. Mungu anatuacha kidogo tufanya kwa namna ya kufanya uzoefu hadi kufikia kikomo cha ubaya na huzuni ambao tuna uwezo wa kufikia bila kuwa na Yeye…  Lakini Roho wa Kristo, Bwana wa Historia anatamani muda  ufike ili aweze  kuangusha yote katika upepo na kutufanya tuanze upya! Baba Mtakatifu anaongeza kusema, daima ni kama vile sisi tunao ufinyu wa maono  na wa moyo; kwa kujiachia katika hilo, sisi wenyewe tunaishia kupoteza mwelekeo; tunafikia  wakati mwingine kujiaminisha  kwamba tumeelewa kila kitu, pia kuwa tumezingatia yote yanayo wezekana na kuwa na matazamio ya  yote ambayo yatatokea na jinsi yatakavyo tokea…Yote hayo ni ujenzi unao danganya wa kutaka kugusa mbingu. Badala yake Roho anaipasua dunia kutoka juu, katika umbu la Mungu, mahali ambapo Yesu alitoka na kufanya mambo yote kuwa mapya! amesema Baba Mtakatifu Francisko.

Je leo hii tunaadhimisha nini katika mji wetu wa Roma?

Baba Mtakatifu Francisko anatoa swali: Je leo hii tunaadhimisha nini, kwa pamoja katika mji watu wa Roma? Tunaadhimisha mwanzo wa Roho ambaye anatufanya tuwe bubu mbele ya mipango ya Mungu isiyotarajiwa na baadaye ni kujazwa na furaha: na kumbe ndiyo ulikuwa mpango wa  Mungu kutoka katika umbu kwa ajili yetu!” Ni  safari hiyo ya Kanisa, ni  hatua hiyo ya Kutoka, inafika katika nchi ya ahadi, mji wa Yerusalema kutoka daima  katika milango iliyofunguliwa kwa wote, mahali ambao lugha mbalimbali za watu zinasikika katika umoja wa Roho, kwa sababu Roho ni maelewano. Siyo huduma yetu sisi binafsi na wala upendeleo wetu, kama vile  ndoto nyingi za madaraka, hapana . Ni katika huduma hiyo ambayo Bwana anafanya na katika maajabu hayo anayofanya Mungu! Iwapo tunazingatia uchungu wa sasa wa kuzaliwa, tunatambua kuwa kilio chetu na kile cha watu wanaoishi katika mji huu, na kilio cha uumbaji wote, siyo  kilio kingine zaidi ya kilio cha Roho. Ni kuzaliwa kwa dunia mpya.

Mungu ambaye ni baba na mama, Mungu ni mkunga, Mungu ni kilio, Mungu ni mwana aliyezaliwa katika dunia, sisi na Kanisa tupo katika huduma ya uzazi huo. Iwapo majivuno na kujidai kimaadili havitatuziba masikio na kutambua kuwa chini kuna  kilio cha watu wengi, hakuna kilio kingine zaidi ya kile cha Roho Mtakatifu. Ni Roho anayetusukuma bado kwa mara nyingine tusifurahie na badala yake kujikita katika safari ambayo ni Roho itakayo mwokoa kila maisha ya kutaka kujitosheleza kijimbo ( Hotuba ya Mkutano wa Jimbo 9 Mei 2019). Ni hatari ya kutaka kuchanganya mapya ya Roho na mtindo wa kujitengenezea kila kitu. Hiyo siyo Roho ya Mungu. Roho ya Mungu anajikita kwa kila kitu na tusienzie mwanzoni, bali kuanza na safari mpya. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo anasema, tujiachie ili tushikwe mikono ya Roho na atupeleke katikati ya moyo wa mji ili kusikiliza kilio na kwikwi zake. Mungu alimwambia Musa kuwa, kilio kilichofichika cha watu, kimemfikia hadi yeye: Yeye alisikia na kuona kusongwa na mateso ya watu... Na alimua kuingilia katikati kwa kumtuma Musa aweze kutoa chachu na kukuza ndoto za uhuru wa wana wa Israeli na kuwaonesha kwamba ndoto yao ndiyo utashi sawa na utashi wake. Kuwafanya wana wa Israeli wawe watu uhuru, watu wake walioungana naye kwa mkataba wa upendo, wanao waitwa kushuhudia imani ya Bwana mbele ya watu wote.

Kwa nini Musa hakutumiza utume wake binafsi na anashuka na Mungu katikati ya waisraeli

Lakini kwa nini Musa hakuweza kutimiza utume wake binafsi na badala yake Mungu anataka ashuke na Yeye katikati ya waisraeli. Baba Mtakatifu anabainisha kwamba moyo wa Musa lazima ugeuke kama ule wa Mungu, ulio makini na kuguswa na mateso na ndoto za watu, kilio kile kilichofichika wakati wakiamsha mikono yao mbinguni, kwa maana hawana wa kuweza kuwashika mikono katika nchi. Ni kwikwi za Roho na Musa lazima asikilize kwa moyo na siyo kwa sikio bali kwa moyo! Leo hii anatuomba sisi wakristo kujifunza kusikiliza kwa moyo. Na Mwalimu wa kusikiliza ni Roho. Na kuufungua moyo kwa sababu Yeye anatufundisha kusikiliza kwa moyo  na kuufungua!

Kwa kuhitimisha mahubiri yake, Baba Mtakatifu amesema ili kuweza kusikiliza kilio cha mji wa Roma, hata sisi tunahitaji Bwana aweze kutushika mkono na kutufanya “tushuke” katikati ya ndugu ambao wanaishi katika mji wetu, kuwasikiliza mahitaji yao ya wokovu, kilio ambacho kinafika hadi kwa Mungu, na ambacho kwa kawaida hatusikilizi. Hii haina maana ya kuelezea katika mambo ya kiakili, mawazo ya kiitikadi; Baba Mtakatifu ametoa mfano kwamba anahisi masikitiko anapoona katika Kanisa ambalo linaamini kuwa ni aminifu kwa Bwana, na linajisasisha wakati likitafuta njia za utendaji  na wakati ni  njia ambazo hazitokani na Roho wa Mungu. Kanisa hili halishuki na iwapo halishuki, Roho anaamuru”.Amesisitiza Baba Mtakatifu. Hii ina maana ya kufungua macho na masikio, lakini zaidi moyo, kusikiliza kwa moyo. Kwa kufanya hivyo tutajikita katika safari ya kweli. “Na kwa kufanya hivyo tutahisi ndani yetu, moto wa Pentekoste ambao unatusukuma kupaza sauti kwa wanaume na wanawake wa mji huu, kwamba utumwa wao umekwisha na kwamba Kristo ni njia inayopeleka mbinguni.  Kwa kufanya hivyo inahitaji imani na hivyo kaka na dada tuombe kila zawadi ya imani kwa ajili ya kwenda katika njia hii”.

 

08 June 2019, 19:45