Tafuta

Vatican News
Papa FRancisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Vituo vya Kitaifa kwa ajili ya miito wa Makanisa ya Ulaya Papa FRancisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Vituo vya Kitaifa kwa ajili ya miito wa Makanisa ya Ulaya  (Vatican Media)

Papa:Kristo anatualika tuwe hai na wito ni safari inayodumu maisha yote!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Vituo vya Kitaifa kwa ajili ya miito ya Makanisa ya Ulaya.Hotuba yake amewakabidhi yenye baadhi ya mambo msingi ya kuweza kujikita nayo kuhusiana na safari ya wito ambapo anasema Kristo anataka tuwe hai na wito ni safari inayodumu maisha yote.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, amekutana  washiriki wa Mkutano Vituo ya kitaifa kwa ajili ya  miito ya Makanisa ya Ulaya, kwa maana nyingine ni wa wahusika wa  kichungaji kwa ajili ya miito barani Ulaya  tarehe 6 Juni 2019 mjini Vatican. Kwa kupendelea kuzungumza nao moja kwa moja, hotuba yake amewakabidhi. Na katika hotuba aliyowakabidhi ina  anawasalimia washiriki wa  Mkutano huo ambao anasema, unataka kusaidia kukuza hali halisi  ya Sinodi ya Maaskofu iliyokuwa ni ya vijana. Anawashukuru kwa kazi yao wanayopeleka mbele kulingana na makambi yao utoaji wa huduma, hata jitihada katika kutiana moyo na kushirikishana uzoefu. Kwa upande  huo amependa kutoa baadhi ya mambo muhimu yaliyomo ndani ya moyo wake. Katika Wosia wake wa Kitume wa Christus vivit anasema, anawatia moyo hata wao ambao wanafanya kazi, kama wasemavyo "katika bara la kizamani" ili kuamini kuwa kila kinachoguswa na Kristo kiweze kuwa kijana na kujaza maisha (Christus vivit n.3). Katika kufafanua zaidi ametumia maneno matatu kama ufunguo wa kutoa maana ya safari ya maisha. Maneno hayo ni:Utakatifu, umoja kama “Humus” ya miito ya Kanisa; wito,  kama  ufunguo wa neno la kuhifadhi na kuunganisha na mengine kama vile furaha, upamoja; na mwisho kujikita katika  kuelezea maisha ya  wakfu maalum. 

Utakatifu

Akianza kufafanua juu ya mambo hayo matatu, ameandika kuwa, suala la wito daima hupelekea kufikiria vijana kwa sababu vijana ni kipindi mwafaka cha uchaguzi wa maisha na kuweza kutoa jibu kwa wito wa Mungu ( Mhutasari wa mwisho wa Sinodi ya Maaskofu juu ya Bijana 140). Kwa maana hiyo ni vizuri, lakini hatupaswi kusahamu kuwa wito ni safari inayo dumu maisha yote. Kwa hakika wito unatazama kipindi cha ujana kadiri ya mwelekeo na chukua hatua baadaye ya kutoa jibu kwa mwaliko wa Mungu na inatazama maisha ya utu uzima katika mwelekeo wa kutoa matunda na mang’amuzi ya wema wa kutimiza. Maisha yanaundwa kwa ajili ya kutoa matunda katika upendo, lakini hiyo inatazama wito wa utafakatifu ambao Bwana anawataka  wote, kila mmoja kupitia njia yake ( Gaudet et exultate, 10-11). Mara nyingi tumefikiri wito kama jambo binafsi kwa kuamini kuwa linatazama “mimi” na siyo hawali ya yote “sisi”.  Anabainisha Baba Mtakatifu. Lakini katika hali halisi, hakuna anayeweza kujiokoa mwenyewe, bali ni kugeuka kuwa watakatifu pamoja (Gaudet et exulte 6). Maisha ya mmoja yanahusiana na maisha ya mwingine ( Mw 44,30) na ni lazima kutunza utakatifu wa watu kwa pamoja.

Umoja

Uchungaji hauwezi kuwa sinodi, ikiwa na maana ya kuwa na uwezo wa kutoa mwafaka wa  kutembea kwa pamoja  (Christus vivit, 206). Na upamoja ni mwana wa umoja. Hii ina maana ya kuisha kama wana na undugu, ili kukuza heshima ya pamoja na kuthamanisha utajiri wa kila mmoja, kuamini kwamba mfufuka anaweza kutenda maajabu hata kwa njia ya majeraha na udhaifu ambao ni sehemu ya historia ya wote. Kutoka katika umoja wa Kanisa miito mipya itazaliwa Baba Mtakatifu amesisitiza. Mara nyingi katika jumuiya, katika familia, katika ukuhani, tumefikiria na kufanya kazi na mantiki ya kidunia ambayo imegawanya na kusambaratisha. Hii inahusika hata baadhi ya masuala ya utamaduni wa sasa na mateso ya kihistoria ya siasa ya Ulaya ambayo ni onyo na kuchangamotisha. Ni kwa njia ya utambuzi wa jumuiya ya kweli tu ambayo imefunguliwa, inaishi na kushirikisha, itawezesha kugeuka kuwa na uwezo wa wakati ujao. Na hii ndiyo vijana wana kiu anasisitiza Baba Mtakatifu!

Wito

"Neno Wito halijaanguka, anasema Baba Mtakatifu. "Na tumelianzisha katika Sinodi ya mwisho na wakati wa michakato yote.. Lakini hatima yake inabaki katika watu wa Mungu, katika mahubiri na katekesi hasa katika kukutana binafsi ambayo ndiyo kipindi mwafaka cha tangazo la Injili (taz. Evangelii gaudium, 127-129). Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa anajua hata  baadhi ya jumuiya zilizo chagua zisitaje neno wito” katika mapendekezo yao kwa vijana, kwa sababu wanafikiri kwamba vijana wana hofu na hawataki kishiriki katika shughuli zao.  Lakini  huu ni mkakati wa kushindwa anasema Baba Mtakatifu Francisko, kwani unaondoa neno la imani yaani  Wito” . Na katika kuliondoa ni kukimbilia hatari ambayo mapema au baadaye haitatambua wito. Badala yake, kuna wanaume na wanawake, walei na watawa wenye moyo wenye shauku kwa ajili ya kukutana na Mungu na kubadili jumuiya zao, kuwa na uwezo wa kutunza furaha itokanayo na wito".

06 June 2019, 14:21