Tafuta

Vatican News
Baba  Mtakatifu amekutana tarehe 10 Mei 2019 na kundi la Papal Foundation wakiwa katika hija yao mjini Roma Baba Mtakatifu amekutana tarehe 10 Mei 2019 na kundi la Papal Foundation wakiwa katika hija yao mjini Roma   (Vatican Media)

Baba Mtakatifu:Papal Foundation ni mashuhuda wa kweli katika Kanisa!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Papal Faundation wakiwa katika fursa ya hija yao mjini Roma ambapo anawashukuru kwa ushuhuda wao wa kujikita katika ukarimu,upendo na ufadhili wao kwa waamini walei,mapadre na watawa duniani kote!ni mashuhuda wa kweli wa Kanisa kuhamasisha maendeleo fungamani ya familia ya kibinadamu

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 10 Mei 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Papal Faundation (Chama cha Kipapa) wakiwa katika fursa ya hija yao mjini Roma. Anaonesha furaha yake kukutana nao na kuelezea shukrani zake kwao kwa ukarimu wa msaada wao wanao utoa kwa ajili yake na kwa ajili ya Kanisa la ulimwengu mzima. Hiki ni chama cha wafadhili kutoka Marekani ambacho kwa zaidi ya miaka 20 wanajikita katika mchakato wa safari ya Muungano wa pamoja na Baba Mtakatifu.

Bwana awatulize kwa nguvu za Roho Mtakatifu na kuwaongezea imani katika Bwana na Kanisa

Baba Mtakatifu Francisko amesema: “Wakati wa kipindi chote hiki cha Pasaka, tunaungana pamoja kuadhimisha ushindi wa Bwana dhidi ya dhambi na kifo, zawadi ya maisha mapya, uumbaji mpya na kuja kwa Roho Mtakatifu”. Furaha ya kufufuka kwa Bwana inaweza kutuliza mioyo yao na hija yao ya kuja kusali katika Makaburi ya Watakatifu na Wafiadini, inaweza kuwaongeza nguvu ya imani yao kwa Bwana na Kanisa.

Jitahada zao zinasaidia kuendeleza maendeleo fungamani ya kibinadamu

Tangu kunzishwa kwa Chama chao katika mchakato wa miaka yote hiyo, Baba Mtakatifu anathibitisha ni kwa jinsi gani wameweza kufanya kazi sana katika kuhamasisha roho ya kidugu na amani. Kwa njia ya msaada wake na mipango ya elimu, upendo na utume, kama vile ufadhili wa masomo ambayo yamewezesha waamini wengi walei, watawa na mapadre. Kwa upande wao ni mashuhuda wa kweli wasio choka wa Kanisa kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo fungamani ya familia ya kibinadamu. Katika dunia ambayo kwa bahati  mbaya inaonesha huzuni wa kutumia nguvu na migogoro, kutoka umasikini wa vitu na kiroho, hadi kufikia  mara nyingi sintofahamu za wengi, lakini  huduma yao inasaidia kupeleka ujumbe wa Injili ya matumaini, ya huduma kwa wale wote wanaofadhiliwa na jitihada zao  na kwa ukarimu wao. Baba Mtakatifu Francisko kutokana na jitihada hizi anawashukuru sana na kuwaomba wajipyaishe katika mapendekezo ya kuchangia na kujenga Kanisa katika umoja na kulifanya liendelee na upendo wake kwa ajili ya kaka na dada walio wa mwisho.

Utume wa Papal Foundation ni wa mshikamano na Mfuasi wa Mtume Petro

Utume wa Papal Foundation unajikita kwa namna  ya pekee na mshikamano na Mfuasi wa Mtume Petro, anasema Baba Mtakatifu na kuongeza: “ Ninawaomba kwa maana hiyo kuendelea kusali kwa ajili yangu na kusali kwa ajili ya utume wangu, kwa ajili ya mahitaji ya Kanisa, kwa ajili ya kueneza Injili na uongofu wa mioyo. Ninawakabidhi pamoja na familia zetu kwa upendo na maombi ya Maria, Mama wa Kanisa”. Kwa moyo  wote amewabariki kwa baraka ya kitume na kama jitihada ya furaha na amani katika Kristo mwokozi wetu.

10 May 2019, 10:09