Baba Mtakatifu Francisko wakati anatoa tafakari yake katika mkutano wa Jimbo Kuu Roma tarehe 9 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko wakati anatoa tafakari yake katika mkutano wa Jimbo Kuu Roma tarehe 9 Mei 2019 

Baba Mtakatifu na Jimbo la Roma:Tunahitaji kusikiliza kilio cha watu zaidi ya kuwa na mipangilio!

Katika Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane Laterano Roma,tarehe 9 Mei,Baba Mtakatifu Francisko anahimiza wanajimbo la Roma kufuata Roho Mtakatifu na kwamba hawawezi kufanya kitu kizuri na cha kiinjili ikiwa wanaogopa kutokuwa na usawa,hivyo wawe makini katika mageuzi,tabia ya kupenda kubadili kila kitu na kumbe hakuna lolote linalobadilika!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mada mbili msingi zimeweza kusikika katika Jimbo la Papa katika mchakato wa safari ya kichungaji, yaani mada ya kufanya “kumbukumbu” na  ile ya “mapatano”. Maparokia na hali halisi ya Kanisa la Roma yameweza kufanya tathimini ya safari yao  ya kichungaji hadi sasa kwa kutazama  mipango mingine ya mwaka ujao, ambayo wataifanyia uzoefu katika  mchakato wa hatua ya tatu watakayo jikita nayo inayoitwa:“kusikiliza mji”. Kutokana na hiyo tarehe 9 Mei 2019 wakati wa kuhitimisha shughuli ya mkutano wao wa siku hizi, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano Roma, majaria ya  saa 1.00 za usiku wameweza kusikiliza maneno ya Baba Mtakatifu Francisko. Shukrani kwa maelekezo yake na kutiwa moyo kwake kwa hakika wanaweza  kuanza kwa upya hatua yao ya wakati ujao.

Heri zinastahiki Nobel ya usawa, lakini kuwa makini dhidi ya udanganifu

Baba Mtakatifu Francisko akizungumza na wanajimbo  kuu la Roma amesema, “Injili ni mafundisho yenye msimamo. Heri za Bwana zinastahiki Nobel ya usawa. Kwa maana hiyo ameonya wawe waangalifu dhidi ya udanganyifu wa kutaka  usawa na vishawishi vya kupanga  na kuratibu jimbo, kwa kutaka  kuweka kila kitu mahali pake. “Hatupaswi kuanguka katika ukleri kleri, ambao ni usawa mzuri, wala kuangukia katika utendaji ambao ni ukoloni mpya wa kiitikadi unaotaka kutushawishi kwamba Injili ni mafundisho na  hekima lakini si tangazo”. amesema Baba Mtakatifu. Aidha akuongeza ameonya kwamba: “hatuwezi kufanya kitu kizuri na cha kiinjili ikiwa tunaogopa kutokuwa na usawa; kwa maana hiyo amesema: " kuna haja ya kuwa makini dhidi mageuzi, yaani tabia ya kupendelea kubadili  kila kitu na kumbe hakuna lolote linalobadilishwa". “Heri  ndiyo sahani ya chakula cha nguvu, anabainisha, lakini tunapaswa bado  kujifunza na kutafuta kuitoa kwa wananchi chakula ambacho kiwafanya wakue. Na hii  amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko, kama alivyo kuwa amefanya hivyo hata huko Firenze katika Kongamano la Kanisa. Amewaalika Kanisa la Roma kusoma kwa upya  Wosia wa Evangelii Gaudium na kurudi juu ya mchakato wa mageuzi ya kimisionari unaopendekezwa na hati hiyo!

Evangelii gaudium uwe ndiyo mpango wa jimbo la Roma

“Evangelii Gaudium,  anasema ni mpango wa Jimbo la Roma”,  hivyo anawakabidhi Jumuiya nzima ya Roma kwanza kufanya zoezi juu ya mtazamo wa kutafakari maisha ya watu wanaoishi katika mji, kwa kutafuta kila parokia uelewa wa watu wanavyoishi, wanahisi nini, wanafikiri nini, kwa kukusanya data za historia ya maisha yenye maana, kuzungumza na wazee ili waweze kuwa na harufu ya mizizi yao, na kwenda mbele wakiwa wamesimika mizizi na siyo hewa. Pili lazima kufanya zaoezi la kuwa na mtazamo wa kutafakari juu ya tamaduni mpya ambazo zinazaliwa ndani ya mji.

Unyenyekevu wa kusikiliza watu

"Mungu anapotaka kuongoka Kanisa lake", anasema Baba Mtakatifu, anamchukua mdogo na kumweka katikati na kwa maana ya mfano huo  anawaalika wote wawe wadogo wa  kunyenyekea kama Mungu alivyofanya. “Mageuzi ya Kanisa, huanza  kwa unyenyekevu na unyenyekevu huzaliwa na kukua kwa kujinyenyekesha na hivyo huondoa madai yetu ya kuwa na ukuu”. Akiendelea na tafakari yake, ameonya pia  hatari ya mtazamo kutoka juu kwenda chini kwa  kuwadharau wadogo”, akikumbuka kwamba, " inaruhusiwa tu kuangalia  kutoka juu kwenda chini ikiwa mtu anapotaka kumwinua na kumsaidia mwingine”. Kwa maana hiyo amesema: "ole wake anayetazama kutoka juu hadi chini na kuwadharau wadogo! Ni kwa yule tu anayemfuata Yesu kama mtoto mdogo anaweza kuingia katika Ufalme. Anayetafuta utukufu wake  anawezaje kumjua Yesu katika wadogo? anasema "hawezi kwa macho yake na wala kwa masikio ya wengine".

Onyo juu ya kupendelea na wasiwasi wa miundo

Baba Mtakatifu amesisitiza hatari ya kupendelea: “Tuna wasiwasi juu ya miundo yetu, juu ya makubaliano na mikataba, juu ya kile ambacho watu watasema, iwapo tunashughulikia Warom, wahamiaji au masikini, lakini sisi tumeshambuliwa na utawala ambao unatoa zoezi juu ya watu jirani zetu, tunakabiliana na kutaka kuwaondoa kondoo wale  wachache waliobaki katika zizi. “Wengi huacha kuwa wachungaji wa kondoo ili waweze kuwa wararua kondoo na mbapo hatuna ujasiri wa kutafuta wengine, wale ambao wamepotea". Na kumbe kila kitu, kinastahili kuwachwa na kutolewa sadaka kwa ajili ya wema wa utume. Lakini pia ni pamoja na ujasiri na uhuru wa wale ambao hawajafungwa na maslahi  na kwa ajili ya kuweka katikati maisha ya wengine, amesisitiza Baba Mtakatifu.

Kuwa na mtazamo wa kutafakari tamaduni mpya kwa maana ya Matukio ya vyama vya utamaduni vyenye ubaguzi Ulaya imeongeza hofu

Matukio ya kitamaduni Ulaya kuhusu vyama vyenye ubaguzi, vinazidi kukua na  kuongeza hofu. Amesema hayo Baba Mtakatifu na kuongeza kwamba, "hata katika ji wa Milele" katika  mantiki za sehemu za pembezoni huzaliwa tamaduni mpya za wema  lakini hata ubaya kama vile, vita kati ya maskini, rushwa na ufisadi, madawa ya kulevya manyanyaso, uharifu vita, ubaguzi na ubaguzi wa rangi, mara nyingi hawasikilizwi au wamesahuliwa kilio cha watu kwa sababu wameacha kuishi ndani ya moyo. Baba Mtakatifu amethibitisha:” tunaishi na mawazo, na mipango ya kijamii, na udadisi na ufumbuzi ulio tayari umefungwa kwenye vifurushi, lakini sisi  ni viziwi hatusikilizi kilio cha watu, na kusikiliza mji” . Kutona hiyo anawalika “kuweka mdogo katikati”. Kadhalika amesema kwamba siku hiyo  amekutana mjini Vatican na jumuiya ya Warom na ambao amesikiliza uchungu wao.Amehitimisha kwa kuwapa Baraka Takatifu.

10 May 2019, 10:24