Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu amekutana na Upatriaki wa Lungro  wenye asili ya Albania na Italia Baba Mtakatifu amekutana na Upatriaki wa Lungro wenye asili ya Albania na Italia  (ANSA)

Papa akutana na watu asili ya Albania na Italia wa Upatriaki wa Lungro:Wao ni mashuhuda wa kidugu!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na watu zaidi ya 6000 washiriki wa hija mjini Roma wenye asili ya Albania na Italia kutoka kusini mwa Italia wanaounda upatriaki wa Lungro katika eneo la Calabria wilayani Cosenza.Papa amesema kuwa wao ni mashuhuda wa kidugu na kuwasihii waendeleze utamaduni wao wa kidini na kuurithisha kizazi na kizazi

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 25 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa hija ya Upatriaki wa Lungro asili ya Italia na Albania wanaoishi nchini Italia ya Kusini. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu anawasalimia na kuwakaribisha kwa shangwe katika fursa yao ya maadhimisho ya miaka100 tangu kuanzishwa kwa Upatriaki wao kwa Katiba ya kitume ya Papa Benedikto XV iitwayo:“Catholici fideles kwa waamini wa Upatriaki wa Lungro. Baba Mtakatifu amesema wamefika Roma wakiwa na Mchungaji wao Donato Oliveri ili kuonesha mbele ya Kanisa zima Katoliki imani na umoja wa jumuiya pendevu, amewashukuru kwa ziara yao na ushuhuda wao wanao uonesha.

Waraka wa   Catholici fideles unahitimisha miaka 100

Miaka 100 iliyopita wakati dunia inalemewa na vita ya kwanza  ya dunia, Babab Mtakatifu amesema kwamba, Mtangulizi wake aliweza kusikiliza historia  na mahitaji muhimu ya lazima kisheria, kama vile hata ujasiri wao wa safari ya kiroho yenye tabia ya imani za kiutamaduni, licha ya matatizo na mateso. Papa Benedikto XV alikuwa na moyo mkuu kwa Kanisa la Mashariki na kutafakari ni nini kilikuwa kinapaswa kufanya kwa ajili ya kukabiliana na mahitaji  pia haki ya Kanisa la ulimwengu na makanisa mengine maalumu. Na kwa maana hiyo aliweza kutangaza kisheria Hati  kwa haraka ya jimbo la ibada ya kigiriki katika ardhi ya Calabria  kwa Waraka wa  Catholici fideles.

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba, tukio hili muhimu ni fursa ya kumshukuru Bwana kwa mema yote, na huruma ambayo ameitendea jumuiya yao katika karne hii ya mwisho. Na zaidi  anawaalika kuishi Jubilei hiyo, si tu kama matazamio ya kufika bali zaidi ni kama fursa moja  na mwamko katika jitihada za kibindamu na katika  mchakato wa safari ya kikristo. Kwa maana hiyo ni lazima kujikita  kwa kina kutafakari wakati uliopita na kushukuru sana kumbukumbu hiyo  na ili kuweza kupata sababu ya matumaini na kutembea kwa pamoja katika kuelekea wakati ujao ambao Mungu atapenda kuwajalia.

Kakaribisha  daima  upendo wa Bwana, kisima na sababu ya matumaini na furaha, kwa kushiriki Sakramenti

Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo wa kukaribisha  daima  upendo wa Bwana, kisima na sababu ya matumaini na furaha, kwa kushiriki Sakramenti na kuonesha ukaribu wa kila familia, kuwa makini kwa masikini zaidi na wanaohitaji, kuwasindikiza vijana kizazi kipya chenye kuwa na changamoto kubwa ya elimu na ambapo anasisitza kuwa wote tu wanahusika! Hata hivyo ameongeza kusema kuwa hayo ndiyo mambo makuu zaidi ya kutunza katika utumaduni wao kama vile ushiriki wa Kristo na Kanisa lake. Wote wanaitwa kuishi kama wakristo, wakishuhudia upendo ulio mzuri zaidi ya chuki, ambapo urafiki ni mzuri zaidi ya uadui na udugu kati ya wote ni mzuri zaidi ya migogoro!

Sala na shukrani kwa wale waliotangulia mbele

Sala na shukrani zetu leo hii Baba Mtakatifu Francisko  amesisitiza ni pamoja na kuwakumbuka wale ambao wanafurahi wakiwa kule mbinguni. Wote ambao waliwaonesha imani na maisha yao lakini zaidi ya maneno yao Baba Mtakatifu, kwa namna ya pekee anawafikiria maaskofu, mapadre, watawa, wazazi na babu na bibi waliowatangulia na ambao kwa imani walitunza na kueneza utajiri wa uzuri wa utamaduni wao. Anawaomba waige mifano yao na kuendeleza kwa kizazi na kizazi urithi wa kitasaufi unao unawatambulisha. Anawasindikiza katika safari yao kila siku kwa ulinzi wa Mtakatifu Maria Mama wa Mungu “Odegitria. Yeye ni mjakazi mwaminifu ambaye alipokea neno la Bwana na awajalie kuwa wapole wa kupokea mapenzi ya Baba na chombo cha ukarimu wa ishara ya wokovu. Amewashukuru kwa upya na kuwabariki wote lakini wakati huo huo akiomba wasisahau kusali kwa ajili yake!

25 May 2019, 13:38