Tafuta

Vatican News
Tarehe 11 Mei 2019 Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Kituo cha Michezo Italia katika fursa ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Chama hicho Tarehe 11 Mei 2019 Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Kituo cha Michezo Italia katika fursa ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Chama hicho 

Baba Mtakatifu Francisko:Mchezo ni shule kubwa inayofundisha thamani na mipaka!

Baba takatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Kituo cha mchezo Italia,Chama kinacho karibisha idadi kubwa ya vyama vya kijami,na makundi ya michezo ya maparokia,katika fursa ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwaa kwake 1944-2019.Katika hotuba yake anasema mchezo ni shule,kubwa inayofundisha thamani na mipaka kujitoa naushupavu

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 11 Mei 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Kituo cha Michezo nchini Italia  wakiwa katika fursa ya maadhimisho ya miaka 75 tangu  kuanzishwaa kwa chama hicho 1944-2019. Katika hotuba yake anasema Mchezo ni shule, hali ambayo inahusishwa katika kujithibitisha  na kuheshimu mwingine, katika wajibu wa kijiborehsa zaidi ili kufundisha kujitoa, ushupavu  katika mazoezi ambayo hafanyi upoteze tabasamu na hata mazoezi hata katika kukubali majaribu.

Baba Mtakatifu katika hotuba yake  anasema mashindano na shughuli ambazo wanaanda,kwa namna ya pekee inayowatazama vijana, lakini pia iliyofuguliwa kwa kila rika inakumbatia idadi nyingi za nidhamu, zaidi ya miamoja! “Sina  uwezo wa kuzichanganua idadi kubwa hiyo ya nidhamu tofauti na hivyo hiyo inaniacha nibaki kwa kutafakari juu ya wingi wa mapendekezo yenu na ukuu wa ubunifu katika dunia ya mchezo, mahali ambapo kila mmoja anaweza kupata  fursa ya kuwa na  mtindo anao utaka” amesema Baba Mtakatifu.

Mchezo ni shule ya kuheshimu wengine na kujiboresha

Kwa njia ya jitihada hizi kubwa za kuendesha michezo  katika Kituo cha cha Mchezo Italia wanachopeleka mbele utume wake, kwa ajili ya kuwafundisha vijana kwa njia ya mchezo, mtindo wa maisha bora, na chanya ambao unasimamia msingi wa maono ya mtu kikristo na katika jamii. Mchezo ni shule, hali ambayo inahusishwa katika kujithibitisha  na kuheshimu mwingine kwa wajibu wa kijiborehsa zaidi ili kufundisha kujitoa, uthabiti  katika mazoezi ambayo hayafanyi upoteze tabasamu, mazoezi na hata ya kukubali kukabiliana na majaribu. Ni somo kubwa zuri la mchezo ambalo linatusaidia kukabiliana hata na ugumu wa mafunzo na kazi kama vile kuwa na uhusiano na wengine ambao wanaweza kugeuza kuwa  katika timu ya kanuni zilizo nzuri  ambazo zimewekwa. Kwa hakika iwapo katika mashindano mmoja anakataa kuheshimu kanuni, anakuwa nje ya mchezo, au anakimbia kabla ya wakati au mshika bendera kupeperusha kabla, machindano hayawezi kuwapo, bali ni huduma za  kibinafsi tu na zisizo na mpangilio.

Badala yake wanapokabiliana na mashindano, ni kujifunza kanuni ambazo ni msingi wa kuishi kwa pamoja, ni furaha ambayo haipatikani bila utaratibu, bali kwa kufuata kwa uaminifu malengo binafsi, pia wanajifunza kwamba huwezi kujifunza iwapo uhisi kuwa uhuru na kuwa na mipaka bali kwa njia ya mipaka inayotolewa kwa kiasi kikubwa. Baba Mtakatifu ameuliza swali: Je tunapaswa kuwa mabwana au Bwana?, sisi na mipaka yetu siyo watumwa wa mipaka yetu!

Je ni maono gani yanafunguliwa katika dunia ya mchezo?

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema je ni maono gani yanafunguliwa katika dunia ya mchezo na matokeo mangapi yanye faida kwa ajili yenu na kwa ajili ya jamii katika mazoezi ya mchezo unaofanywa uzoefu kama furaha ya kukutana, ya kukua na kidungu? Tazama ndiyo maana katika Kanuni yenu inasema kuwa: Katika Kituo cha Mchezo cha Italia ,lengo lale ni kishuhudia thamani za mchezo kama chombo kwa ajili ya kuhamasisha makaribisho, afya, kazi,  fursa, kutunza mazingira, kulinda watoto na vijana, kushirikishana na ushirikishwaji kijamii.

Mnaweza kujiuliza jinsi gani mnaweza kutumaini katika mchezo uwe chombo cha kutatua matatizo mengi na kuwezesha mabadiliko ya kina katika jamii yetu? Tunaweza kujibu kuwa mchezo unaweza kuboresha watu, unaweza kusaidia utamaduni wa mazungumzo na kukutana kwa heshima. Mapambano kati ya  wapinzani katika mashindano ya mchezo daima yamefafanuliwa kama mkutano na siyo kugombana kwa sababu mwisho wa mchezi ni ule wa kushinda, kwa maana nyingine ya kila mmoja. Na ndiyo ndiyo maana ya dunia ambayo tunaota na ambayo ni yenye msimamo tunaotaka kuujenga juu ya msingi wa mchezo ambao ni  safi na daima unao kwenda hata mashindano na rafiki na ndugu.

Huo ndiyo moyo wa maono ya mkristo ambapo kwao Baba Mtakatifu maethibtisha kwamba  ni msingi wa shughuli za mchezo. Kwa tabia hiyo, kwa moyo huo mpangilo wa  kila shughuli ya mchezo unaweza kuitwa mchezo . Wanacheza watoto, mchezo ni shughuli ya furaha daima. Ni akuanzia na msingi huo tu tunaweza kufuata mawzo yaliyo ya  juu na mazuri. Maono ya mkristo ni kujifunza kutazama wengine na ili kumwona kwa  macho yake Yesu; kwa macho yake Mungu na kwa macho yake ambayo Mungu anatazama mimi: kumwona kama alivyokuwa anaona Yesu, kumwona kama anavyoona Mungu. Ina maana ya kusikiliza maneno yake na kutambua kwa hisia na kutafuta kuisha ishara zake.

Tofauti zetu siyo sababu ya kugawanyika bali katika kukua na kusaidiana

Baba Mtakatifu amesema wawe na uhakika kwamba kuanzia katika Injili inatoyoka nje, dunia inakuwa nzuri na yenye haki, mahali ambapo utofauti za wengine siyo sababu ya kuleta migawanyiko bali ni sababu ya  kukua na kusaidiana. Baba Mtakatifu anawatia moyo ili waishi kwanjia ya roho hiyo katika vituo vyao vya  kiparokia, wanapofanya kazi na kulinda imani ambayo mungu aliwajalia na ambayo ni tunu msingi wa maisha yao. Wanaweza daima kushukuru kwa yule anaye wafundisha na kuwasindikiza kama vile: walimu wao, wazazi wao na ndugu zao. Wanaweza pia kuwasindikza kwa urafiki na msaada kwa wale wote kati yao wanaojikita na shughuli ya mipango ya kujitolea katika mchezo wa kimataifa na ambao wamewezesha mipango mingi kati nchi mbalimbali  kuwakilisha tunu kuu ya wakati wetu. Hii ndiyo kujitoa bure. Shughuli yao lazima iweze kuigwa kwa njia ya kujitoa bure na kwa maana hiyo ni muhimu katika mchezo kuhifadhi ukuu wa kujitoa. Ni muhimu sana kwa sababu inahifadhi hali ya kujitoa bure na kuwa mtoaji!

Anahitimisha kwa kuwatakia daima wawe na furaha katika maisha yao ya chama na kugeuka kuwa wamisionari katika mazingira wanamoishi na kuonesha furaha ya kuwa bora kila siku, kuwa makini daima kwa wale wote wanaowazunguka wakimbwa kuwapa mkono wa urafiki kwasaidia. Bwana awabariki katika safari yao, hata kubariki yeye. Amewaomba wasali kwa ajili yake.

11 May 2019, 14:07