Cerca

Vatican News
Tarehe 9 Mei Baba Mtakatifu amekutana na maprofesa na wanafunzi wa Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia Tarehe 9 Mei Baba Mtakatifu amekutana na maprofesa na wanafunzi wa Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia 

Taasisi ya Kipapa ya Biblia:Upendo ni msingi wa mazungumzo ya kidini!

Tarehe 9 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa mkutano kuhusu maandiko ya biblia ya Kiyahudi,Katoliki na Kiprotestanti,unaoongozwa na tema:“Yesu na Mafarisayo:Mapitio ya kinidhamu”,ulioandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Biblia katika fursa ya kumbukumbu ya miaka 110 tangu kuanza kwa Taasisi hiyo.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 9 Mei 2019, Baba  Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wataalam kutoka nidhamu ya maandiko ya biblia ya Kiyahudi,Katoliki na Kiprotestanti wakiwa katika fursa ya  kumbukumbu ya miaka 110 tangu kuanzishwa kwa Taasisi  ya kipapa ya Biblia. Ni mkutano ulioandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya siku hizi za kujifunza na ambao umehitimishwa leo hii. Mkutano huo umechunguza asili na historia ya kikundi cha kidini cha Mafarisayo, ambao wanaonekana katika Maandiko Matakatifu, katika nyakati mbalimbali za Injili na maisha ya Yesu na ambapo mazoea hayo yamejitokeza katika matokeo tofauti hasi na kati  hayo ni pamoja na mapambano ya ubaguzi wa kiyahudi.

Ili kuwapenda wale walio karibu nasi tunahitaji kuwajua

Katika hotuba aliyowakabidhi Baba Mtakatifu Francisko, anatoa tafakari juu ya hukumu ambazo zinatuzuia kuwapenda majirani zetu kuanzia na sura ya “Farisayo”, ambapo anasema: " ili kuwapenda wale walio karibu nasi tunahitaji kuwajua na mara nyingi kutafuta njia za kushinda hukumu za kizamani". Hili ni wazo ambalo linakwenda sambamba na kauli mbiu ya mkutano wao unaongozwa: “Yesu na Mafarisayo:Mapitio ya kinidhamu”. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba aliyo wakabidhi washiriki wa kutano huo kutoka kwa wayahudi, waprotestanti na wakatoliki kutoka Marekani, Asia na Ulaya badala yake amependa kuwasalimia mmoja baada ya mwingine na kuwambia hawali ya yote miaka 110 ya Taasisi ya kipapapa ya Biblia, walioandaa mkutano huo na utume wake wa kuhamasisha mafundisho ya  Biblia pia kwa bahati nzuri tema ya Mkutano ikiwa ni tunda hata la uhusiano wa Kanisa na dini siziso za kikristo kama zinavyoonesha katika Hati ya Nostra Aetate zinakwenda katika  moyo wa masuala ambayo yanafunguwa kwa namna ya pekee kati ya Wakristo na Wayahudi.

Neno wafalisayo katika ulimwengu linajulikana vipi?

Akifafanua zaidi juu ya neno la wafalisayo anaandika kuwa: "Miongoni mwa Wakristo na katika jamii za kidunia, neno Mfarisayo linamaanisha mtu mnafiki au anayejidai, hata kama kwa Wayahudi wengi, Mafarisayo ni waanzilishi wa Walimu wa Uyahudi” anaandika Baba Mtakatifu.Kwa maana hiyo tupo mbele ya ya kushughulikia historia ya ufafanuzi ambayo, hata bila msingi halisi katika Injili, ilikuza “picha hasi za Mafarisayo" na mara nyingi walio changia ni Wakristo”. Katika ulimwengu wetu, maoni mabaya kama hayo kwa bahati mbaya ni ya kawaida sana. Mojawapo ya ukawaida huo wa kizamani wa kuharibu zaidi ni ule wa “Farisayo”, hasa  unanapotumia kuwaweka Wayahudi katika nuru mbaya. Baba Mtakatifu Francisko anaandikia kuwa:Utafiti wa hivi karibuni unatambua kuwa leo tunajua kitu kidogo juu ya  Mafarisayo kuliko walivyokuwa walivyokuwa vizazi vilivyopita. Hiyo ni kwa sababu anaongeza, "hatuna uhakika zaidi wa asili yao na wingi wa mafundisho yao na mazoea yao". Kwa njia hiyo, utafiti wa kinidhamu juu ya masuala ya masomo ya kimaandishi na ya kihistoria ya Mafarisayo yaliyokabiliwa katika mkutano huu yatatusaidia kupata maono zaidi ya kweli ya kikundi hiki cha dini, pia kusaidia kupambana na ubaguzi wa kiyahudi".  Vile vila Baba Mtakatifu anaandika: Mtume Paulo alisema juu ya sheria, Mfarisayo na Yesu, kwamba  walikuwa wanahusiano na Mafarisayo katika majadiliano, imani katika Ufufuko, tafsiri ya Torati, bila kutaja moja ya wakati mwafaka wa Injili ya Yohane, yaani, katika mkutano wa Yesu na  mmoja wa viongozi wa Kiyahudi, Mfarisayo Nikodemu ambaye alimtetea na baadaye akamsaidia katika mazishi na ambaye hakuna hata ukawaidwa wa kuzungumzia juu yake.

Kanuni ya dhahabu kati ya Wayahudi na Wakristo

Baba Mtakatifu anaandika kuwa, lakini dhamana kubwa ni katika kile kinachojulikana: “ kanuni ya dhahabu”: mpenda jirani yako kama unavyo jipenda, ambayo Yesu angeweza kuwapatia, kwa mujibu wa Injili ya Mathayo, na iliyo tafsiriwa na mmoja wa waandishi na  Mfarisayo. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu  Francisko anaandika kuwa: inaonesha  heshima kubwa ambayo Yesu alikuwa nayo kwa viongozi hao wa kidini waliokuwa karibu sana na ufalme wa Mungu”. Hata hivyo uthibitisho unatokea pia kutoka kwa mmoja wa walimu maarufu zaidi wa karne ya pili, mrithi wa mafundisho ya Mafarisayo, Mwalimu Aqiba, “anayeoneshwa katika kifungu cha Mambo ya Walawi 19, 18: umpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe, ni  kanuni kuu msingi wa Torati. Kwa mujibu wa utamaduni, yeye alikufa kama shahidi na akiwa na Shema  mdomoni mwake ambayo inajumuisha amri ya kumpenda Bwana kwa moyo wote, roho na nguvu.

Ushirikiano kati ya Yesu, Walimu wa kiyahudi na Mafarisayo wa wakati uliopita na wa sasa

Kwa ujumla maelewano kati ya Yesu, walimu wa kiyahudi na Mafarisayo wa wakati uliopita na wa sasa ni kwamba, upendo wa jirani ni kiashiria kikubwa ili kutambua uhusiano kati ya Yesu na Wafarisayo wake na kwa hakika hufanya msingi muhimu kwa kila mazungumzo yoyote, hasa kati ya Wayahudi na Wakristo, hata leo. Kiukweli, kupenda jirani zetu vizuri, tunahitaji kuwajua, na ili kujua ni nani mara nyingi tunapaswa kutafuta njia za kushinda chuki za na hukumu za kizamani. Kwa sababu hiyo, Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha katika hotuba yake aliyo wakaibidhi washiriki wa mkutano unaoendelea katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana  wenye roho ya nidhamu ya kidini, kwamba: mafunzo hayo na utafiti huo utatuwezesha kuwasilisha Mafarisayo kwa ufanisi zaidi katika kufundisha na kuhubiri na itasaidia mchango chanya wa mahusiano kati ya Wayahudi na Wakristo kwa mtazamo wa mazungumzo daima ya kina na kindungu zaidi!

09 May 2019, 14:51